Separate mita nyumba za kupanga inawezekana? Nishachoka kununua umeme

toplemon

JF-Expert Member
Mar 26, 2017
4,581
4,631
Hivi inawezekana kila nyumba kuwa na mita yake?Maana hapo nilipo tupo saba nyumba mbili

Nyumba ya kwanza ni ya vyumba vya ndani ambayo humo kuna vyumba vinne na kila chumba kina sebule na chumba cha kulala na huko wanakaa wapangaji na familia zao na wasichana wao kazi

Nyumba ya pili ni vyumba vya nje na tupo watatu tu wote ni mabachela na hatuna matumizi makubwa ya umeme wote tuna tv,redio na feni.

Wale kule wapo familia wana hadi mafriji na wanashinda nyumbani muda wote mafriji yanalia

Tunanunua umeme wa elfu 70 unakaa siku 18 tu....Sasa imekua ni changamoto kweli kweli

Sisi wa nyumba vya nje tupo watatu wote hatushindi nyumbani ni watu wa kurudi jioni tu lakini unaisha tu umeme wa elfu kumi siku mbili ushaisha

Mimi naombeni mnijuze utaratibu wa Separate mita unakuaje

Sisi wa vyumba vya nje watatu tunataka tuwe na mita yetu wenyewe, na wa ndani nao wawe na yao wenyewe nia ni kuhakikisha tunakuwa na two separate mita japokua mita kuu itakuepo

Swali jee hili linawezekana?Utaratibu upoje?Na jee umeme ukiisha vp?
 
Yani hapo kitakachotokea ni ugomvi mkubwa 😅!

Ni sahihi kuwa na separate Unit Counter ila walimwengu hawawezi kuwaelewa hasa kama mwenye nyumba anaishi humo humo. Sababu itaonekana nyie mmetumia umeme wa buku 3 nyote ilihali wenzenu wanalipishana buku 5/5 itaanza vita kuu ya 3 ya dunia!
 
Daaah nyumba za kupanga bana , umeme na maji hua ni kero kuu, Mara nyingi huleta mparaganyiko na wapangaji kuto kuelewana
 
Yani hapo kitakachotokea ni ugomvi mkubwa 😅!

Ni sahihi kuwa na separate Unit Counter ila walimwengu hawawezi kuwaelewa hasa kama mwenye nyumba anaishi humo humo. Sababu itaonekana nyie mmetumia umeme wa buku 3 nyote ilihali wenzenu wanalipishana buku 5/5 itaanza vita kuu ya 3 ya dunia!
Hii kitu usiombe kabsa kuishi kwny nyumba ya namna hiyo...unaweza kuyachukia maisha lkn pia kukiwepo nyungeza ya BOmBa la maji ...unaweza kujuta bili ya maji na umeme zinatokea tar18 kabla salary haijatoka ...

Yaan umeme 70k + 50 ya bili ya maji..
 
Hii kitu usiombe kabsa kuishi kwny nyumba ya namna hiyo...unaweza kuyachukia maisha lkn pia kukiwepo nyungeza ya BOmBa la maji ...unaweza kujuta bili ya maji na umeme zinatokea tar18 kabla salary haijatoka ...

Yaan umeme 70k + 50 ya bili ya maji..
Mkuu yani ni shida tabu na mateso! Niliwahi kupanga nyumba nzima umeme haukuwa shida ila maji doh! Bill inakuja elfu 15,000 kwa mwezi niko mwenyewe tu! Ilifikia stage nilisepa!

Nyumba ya awali nilipanga geto tu ndio ilikuwa kichefu chefu yani balaa! Tsh5000 kila baada ya siku 3 yani ikafikia stage kwa mwezi nalipa 25,000 ya umeme pekeangu! Ilikuwa balaa!
 
Hizi nyumba bana, kuna nyumba mbili nyumba moja naishi mimi na bachela mwenzangu pia wote ni watu wa safari uzuri tuna mita yetu ya umeme ma tunatumia zero unit.

Kisanga kinakuja kwenye maji maana tunatumia wapangaji wote wanne, unaweza usiwepo hata mwezi watu bill ya maji ikija wanakutumia tu hivyo hivyo na huko nyumba nyingine ni watu na watoto wadogo na familia kubwa. Tuna mpango tutafute mita yetu sababu sina mpango wa kutoka hapo anytime soon.
 
Endelea kukaa hapo ili wakupe motisha ya kujenga. Maisha ya kupanga yakiwa smooth unaweza kuzeekea hapo.
 
Back
Top Bottom