Sentensi 10 ambazo zinaweza kubadili maisha yako

chaUkucha

JF-Expert Member
May 28, 2012
3,382
1,212
1. Katika ushindani wa kupata mafanikio kwenye maisha, kazi, elimu, biashara hakuna mtu ambaye anakuchukia ila kila mtu anajipenda yeye binafsi na anataka kufanikiwa yeye kwanza.

2. Pambana kufanikiwa sio ili dunia ikuone lakini kwa sababu kufanikiwa ni sehemu ya kukamilisha ubinadamu wako. Hukuumbwa ili usifanikiwe.

3. Unajifunza zaidi pale unaposhindwa kuliko pale unapofanikiwa. Kushindwa kusikurudishe nyuma, hukupa funzo la kusonga mbele.

4. Jambo la hatari kuliko yote katika maisha: kujinyima kufanya jambo unalopenda kufanya sasa hivi ukihisi kwamba baadaye utakuwa na uhuru zaidi wa kulifanya. Uwepo wako kesho chini ya jua hauna uhakika nao. Fanya sasa.

5. Nenda unapoona uwepo wako unathaminiwa. Usiende mahali ambapo uwepo wako unavumiliwa tu.

6. Mtu ambaye utakaa naye maisha yako yote ni "wewe mwenyewe" . Tumia muda wako kadiri uwezavyo kuwa bora kwa ajili yako wewe mwenyewe.

7. Ukikubali sehemu uwezo wako unapoishia unaweza kujipanga kwenda mbele zaidi ya hapo. Jua jambo gani unaweza, lipi huwezi na jipange. Usijifanye kuweza jambo usiloweza. Utashindwa kujifunza.

8. Hakikisha unazungukwa na watu wanaoamini katika kushinda.

9. Kila mtu unayekutana nae kwenye maisha ana kitu anakiogopa, ana kitu anakipenda na ana kitu ameshawahi kukipoteza. Usijione wewe peke yako ndiye unapitia hayo.

Kuridhika ni adui wa kusonga mbele. Kama unataka kusonga mbele kutoka 90 kwenda 100 lazima kwanza nafsi yako isiridhike kuwa kwenye 90.
 
Aksante mkuu kwa ujumbe murua hasa pale uliposema uende mahali uwepo wako unapothaminiwa na kutokaa mahali uwepo wako usipothaminiwa.

Watu wamepoteza vitu vya thamani kwa kulazimisha kuishi na watu wasiowathamini.
 
5 na 6 imenigusa sana hasa tano mpk moyoni kabisa
hakika namba tano imeamsha kitu kipya nafsini mwangu


ningekuwa na dada ningekuozesha buleeeeree hakika umenigusa sanaa
 
5 na 8 zimegonga mfupa!hilo la 5 lilishawahi kunikuta recently,hiyo sehemu nikakimbia faster baada ya kuona sina thamani kwao,na iyo 8 ndo naiishi now,most of people ambao nahang nao kwa sasa ni wale wenye real enthusiasm,hawaamini katika kitu kushindwa wakati wanayaendea majambo yao...hii inanipa sana hamasa ya mimi kuwa na the same spirit too.
Ahsante mkuu!
 
5 na 8 zimegonga mfupa!hilo la 5 lilishawahi kunikuta recently,hiyo sehemu nikakimbia faster baada ya kuona sina thamani kwao,na iyo 8 ndo naiishi now,most of people ambao nahang nao kwa sasa ni wale wenye real enthusiasm,hawaamini katika kitu kushindwa wakati wanayaendea majambo yao...hii inanipa sana hamasa ya mimi kuwa na the same spirit too.
Ahsante mkuu!
Vizuri mkuu pamoja sana.
 
Back
Top Bottom