BLUE BALAA
JF-Expert Member
- Nov 30, 2010
- 1,222
- 786
Fafanua, umetumia nguvu nyingi kwenye backgroud lkn kwenye main body umeweka vimifupa viwili tu.
Ili pesa iliwe inabidi ujustify,AG aanze kufanya uchunguzi maana naona ambao ujenzi ulikuwa umekwama sasa majengo yanaenda kwa kasi,watu wanajua kuila nchi.mimi nahisi ni maandalizi ya kutohoa pesa za uchaguzi wa 2015,
ukizingatia mradi wa ujenzi wa bot na epa pesa zilitumika ktk kampeni za 2005,kuna miradi kama ya mabasi ya kasi dsm,ujenzi wa kigamboni city,upanuzi wa bandari,na hili la sensa yote ni kwa ajili ya lengo la kukusanya na kuhalalisha matumizi makubwa yasiyo ya lazima. SEnza ingefanywa kwa mfumo wa wtu kujitolea ,i.e volunteers wapo wengi tu na kila mjumbe wa mtaa angeweza kupata japo watu watatu kujitolea ktk mtaa wao
Naambiwa budget ya sensa ya mwaka huu ni Tshs160 Billion. Jana nikakutana na Mwenyekiti na Katibu Mtendaji wakaniambia mpaka sasa hawajalipwa na hata wakilipwa haitazidi shs 150,000 kwa mtu. Najaribu kupiga hesabu na kugundua kwamba hela nyingi imetumika katika administration and logistics. Na siku ya mwisho anaehesabu watu ni watu wa chini kabisa. Mimi leo nimehasabiwa na sijaona hata swali moja ambalo ni very technical kumshinda balozi kuniuliza.
JE? Ni kwanini Sensa isingerudishwa kwa Mkurugezi wa maendeleo wa wilaya na yeye aka delegate kwa WEO na kufika mpaka kwa mabalozi? Je isingetumia muda mdogo na pesa kidogo?
Tanzania bhana, we acha tu! Tunajua tuna walimu wangapi na tumeshindwa kuwahudumia, tukijua watanzania wote halafu iweje?