real G
JF-Expert Member
- Feb 7, 2013
- 5,227
- 5,296
Sengerema. Mlinzi wa kampuni binafsi ya ulinzi ya Nyuki, Seleman Buyoga ameuawa na watu wasiojulikana akiwa lindoni baada ya kuvamiwa.
Mlinzi mwingine, Charles Guli amejeruhiwa vibaya katika tukio hilo lililotokea Kijiji cha Sima wilayani Sengerema usiku wa kuamkia leo Alhamisi.
Ofisa Mtendaji Kata ya Sima, Tamali Lukonge amesema tukio hilo limetokea saa 9:00 alfajiri leo baada ya watu wasiojulikana kuwavamia na kuwashambulia walinzi hao wakiwa lindoni.
Katibu Tawala Wilaya ya Sengerema, Alen Augustine ambaye yuko eneo la tukio muda huu akiongozana na maofisa wa polisi amesema tayari vyombo vya dola vimeanzisha msako dhidi ya waliohusika na tukio hilo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema jeshi hilo linamshikilia kwa mahojiano mlinzi, Mashauri Philipo aliyekuwa na wenzake lindoni, lakini yeye hakushambuliwa na wavamizi.