Sengerema, Mwanza: Wakurugenzi watafuna hela za michango ya maendeleo, Wananchi wagoma kuchanga

mshale21

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
2,049
4,904
Baraza la madiwani halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza limemtaka mkurugenzi wa halmashauri hiyo kuwachukulia hatua baadhi ya watendaji waliopewa dhamani ya kukusanya fedha kwa ajili maendeleo na kuzitafuna.

Kutafunwa kwa fedha hizo zinazochangwa na wananchi kwa ajili ya maendeleo kumesababisha waanze kugoma kuchanga.

Diwani wa Buhama, Petro Mbunde amesema wananchi wa kata yake wamegoma kuchanga michango ya maendeleo kutokana na watendaji wa vijiji na kata kutuhumiwa kutafuna fedha hizo.

"Watendaji wamekuwa kikwazo cha maendeleo hivyo halmashauri inatakiwa kuwawajibisha kuhusu jambo hili ili wananchi wawe na imani, " amesema Mbunde.

Tuhuma hizo pia zimeelekezwa kata ya Bulyahike ambako fedha za michango zimetafunwa na watendaji kitendo kilkchowakera wananchi.

Diwani wa Bulyaheke, Bagetu Ngele amesema watendaji wa vijiji na kata kwenye kata wamekuwa kikwazo cha maendeleo na kwamba wanapaswa kuondolewa na kurudisha fedha za wananchi wanazodaiwa kutafuna.

Masumbuko Bupamba ambaye ni diwani wa Bupandwa ameiomba halmashauri hiyo kupeleka mkaguzi wa ndani kwenye baadhi ya kata ambazo watendaji wake wanatuhumiwa kutafuna fedha za wananchi ili afanye ukaguzi na ukweli ujulikane.

Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Buchosa, Brono Sangwa amekiri baadhi ya watendaji kulalamikiwa kutafuna fedha zinazochangwa na wananchi kwa ajili ya maendeleo.

Amemwagiza mkaguzi wa ndani kwenda kata ya Buhama na Bulyaheke kufanya ukaguzi na kuwasilisha taarifa ya atakachobaini.

"Watendaji mnatuhumiwa kutafuna fedha zinazochangwa na wananchi kwa ajili ya maendeleo lazima tuchukue hatua ili kurejesha imani kwa wananchi, " amesema Sangwa.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Buchosa, Idama Kibanzi amesema wanaotafuna fedha hizo inatakiwa wafutwe kazi
 
Heading "WAKURUGENZI" ndani ya taarifa hakuna mkurugenzj anayeoneshwa nali ni watendaji
 
Endeleeni tu kuwachangia,wao waendelee kuponda maisha

Ova
 
Kufanya kazi kwenye hizi Halmashauri ni shida. Majungu kila uchwao.
 
Back
Top Bottom