Senegal wameweza, Zambia waliweza. Wa Tanzania tunashindwa nini?

Wa kusoma

JF-Expert Member
Jul 30, 2011
3,454
2,975
Wakuu matokeo ya urais yametangazwa nchini Senegal na mpinzani mkuu wa rais aliyekuwa madarakani kwa muda mrefu ametangazwa mshindi.

MY TAKE:
Zambia waliweza, hawa tena wameweza tena wameshindana na marais walioko madarakani, je sisi TZ tutashindwa nini kukitoa CCM madarakani itakayokuwa imevurugika na makovu kibao ya mbio za rais?
 
Mkuu hiyo ingewezekana kabisa Tz iwapo watz tungekuwa hatukubali wenyewe kwa ujinga wetu kufanywa mandondocha ya ccm.
 
Hata sisi tunaweza ndio maana tunataka tubadilishe mkataba wa kukubali kutwaliwa aka kuongozwa na hao viongozi
 
Mujwahuzia:
Hilo litawezekana tu kwa Watanzania wengi wenye kupenda kuvaa Nguo za kijani na Njano katika mambo ya Siasa watakapo tambua chama ambacho kinatusababishia Maumivu ni hicho kinacho wapa magwanda ya Kupumbaza akili zetu.ndipo tutakapojikwamua lakini leo hii natumai watanzania tulio wengi bado tupo gizani tunanyemelewa na ufukara zaidi na hatutaki kubadilika.
 
Kwa sababu CCM ndio chama dume pekee
Wengine wasindikizaji tu
OTIS
 
Wakuu matokeo ya urais yametangazwa nchini Senegal na mpinzani mkuu wa rais aliyekuwa madarakani kwa muda mrefu ametangazwa mshindi.

MY TAKE:
Zambia waliweza, hawa tena wameweza tena wameshindana na marais walioko madarakani, je sisi TZ tutashindwa nini kukitoa CCM madarakani itakayokuwa imevurugika na makovu kibao ya mbio za rais?

kumbuka senegal watu walilala mtaani kumpinga Wade na Dakar kuwaka moto kabla ya ngwe ya kwanza ya uchaguzi, wade akaogopa kuiba katika ngwe ya pili.

Kwa upande wetu Watz hawateweza kufanya hivi, ni watu wa kulalamika tu na kuendelea na maisha kama yalivyo ili mradi kunakucha. good luck watz
 
Watanzania tulishaamua labda hayo Maswali uwaulize Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
 
Hakuna chama serious cha upinzani Tz. Yapo makampuni na NGOs za watu fulani fulani.

NGO/Kampuni mojawapo iitwayo CDM ni ya Wachagga, ukiwa mwanachama wao kutokea mkoa mwingine,... wewe ni msindikizaji tu, unatumiwa tu, ni mtu wa kujibu 'hewala Mwenyekiti' wakati wote.

Ukithubutu kuonesha nia ya kugombea uongozi wa juu wa nchi au wa chama au KUB ..... demokrasia inasiginwa, unaonekana msaliti. Unatukanwa saana. Utajuta kutaka kugombea nafasi za wenye NGO/kampuni.

Kwa hiyo Tz vyama vya upinzani baaado, na inavyoonekana CCM itaendelea kutawala kwa miongo mingi ijayo.
 
Wakuu matokeo ya urais yametangazwa nchini Senegal na mpinzani mkuu wa rais aliyekuwa madarakani kwa muda mrefu ametangazwa mshindi.

MY TAKE:
Zambia waliweza, hawa tena wameweza tena wameshindana na marais walioko madarakani, je sisi TZ tutashindwa nini kukitoa CCM madarakani itakayokuwa imevurugika na makovu kibao ya mbio za rais?

Tuna woga wa kuthubutu. Pia wanaojiita wakereketwa wengi wao si wapiga kura! Watanzania wanao jitokeza kupiga kura (ukiondoa maeneo machache ya nchi) ni wachache sana ukilinganisha na waliojiandikisha!

Hamasisheni watu wajitokeze kupiga kura; itasaidia kuleta picha halisi ya nani atuongoze
 
Kumbuka pia kwamba wapinzani wooote waliamua kumpigia kura candidate mmoja wa upinzani huko Senegal...

Ni mpaka hapo viongozi wa upinzani wa TZ watakapoacha uchu wa madaraka na uroho wa ruzuku na kuamua kusimamisha candidate mmoja wa upinzani kwa ngazi ya uraisi na hata ubunge kwa baadhi ya majimbo, ili kupambana na Magamba mmoja ndo tutatambua nguvu ya umma maaana yake nini. Vinginevyo kuwa na "madovutwa" kibao mpaka kufikia kumi kwa ngazi ya uraisi ni sawa na kumpigia mbuzi gitaaa, Magamba yataendelea kukomaa madarakani mpaka yaamue yenyewe kwamba sasa yamechoka, yanataka kujivua!!!!

Hili ni somo kubwa kwa wapinzani wa kweli kuamua kufanya kweli 2015...Napenda tuwe na wagombea si zaidi ya watatu kwa ngazi ya uraisi....Inawezekana, tuamue tuone!!!
 
Back
Top Bottom