zubedayo_mchuzi
JF-Expert Member
- Sep 2, 2011
- 4,873
- 1,217
Hizi kabali tunaweza kuweka kwenye magrupu manne
1.Kabali ya mbele
2.Kabali ya nyuma
3.Kabali ya kushoto kabali ya kulia
Achilia mbali kabali za chini, ambazo anaeweza piga kabali hiyo ni lazima atakua na elimu hiyo, hizi kabali za chini huwa zipo kwenye michezo na michezo ya martial arts.
Dhumuni langu kubwa ni kabali ambazo hutumika sana hasa kwenye kupora vitu, iwe usiku au mchana na kabali hiyoo unaweza pigwa na mtu mmoja huku akikusachi au akakupiga mmoja wengine wakakusachi ila wakisha hakikisha umetulia baada ya kupigwa kabali hiyo
1.Kabali ya mbele
Kabali hii mtu ukabwa kwa mbele na adui au mtu anaejiamini kuwa akikukaba hutakua na uwezo wa kumfanya chochote.
Kabali hii mara nyingi hukabwa wanyongwe,ni mara chache sana kutumika kwenye uporaji.
STEPU YA KWANZA UMEPIGWA KABALI YA MBELE
STEPU YA PILI UNAPANGUA KABALI YA MBELE
Kama picha zinavyoonekana, unapopangua kabali ya adui wako kuna mambo mawili, unaweza kushika mikono yake nakuitoa shingoni kwako na usiweze kuitoa kama itatokea amekuzidi nguvu.
Hatua ya kwanza utapangua mikono yake na kubonyea kidogo, anapokubali kubonyea na kukufata basi utaamua wewe kupiga kifuti cha kwenye tumbo au utaamua kushambulia ikulu yake.
Ukumbuke unajihadhari na hatari ya kabali, ambayo kama utairuhusu unaweza kuuwawa kabisa, ni lazima matukio hayo uyaamue kwa haraka zaidi.
Kama picha dada huyo inavyoonekana, amepangua kabali na kutoa pigo kali kwenye makende.
Kama watakua wawili, endapo mmoja atapata shambulio na mwenzake akiona, huyo mwingine atakimbia hawezi kuja .
2. Kabali ya nyuma
Kabali ya nyuma ni kabali zinazo waliza wengi sana, ni kabali inayofanywa kwa timing kubwa mno. Inapotekea umekabwa iwe kwa mikono kama inavyoonekana.
Stepu ya kwanza ni kupangua kabali na kushambulia.
Kama picha zinavyoonyesha, unapo peleka mikono yako nyuma kutoa kabali hiyo una step mguu wa kulia kupata balance, pili unapangua mkono wake mmoja, huku uki utwist then moja kwa moja unapeleka mkono wako unakamata groin zile unazifuta, lazima atabonyea basi utamshambulia kwa kipepsi usoni, shingoni kadri utakavyoweza.
Yaani kitendo hiki hufanyika kwa haraka zaidi anapokuvisha mikono yake nawe muda huo huo unavua mikono hiyo, ikitokea umeshindwa kuitoa na umeshindwa kukamata groini zake, step forward, inama kidogo then piga teke la nyuma kwa nguvu kwenye goti lake hapo lazima atapoteza stability basi utamshambulia haraka.
Kwa leo naishia hapa.
Ni yule yule Zubedayo_mchuzi mzee wa kutembea umbali mrefu.