Dullo
JF-Expert Member
- Oct 24, 2009
- 251
- 64
Kwa wale ambao ni mawakala wa Selcom Paypoint tumekumbwa na wizi wa mchana unaofanywa na kampuni hiyo kwa kushirikina kampuni ya TIGO bila kupatiwa ufafanuzi wowote.
Nini kimetokea?
Awali ilikuwa unapata asilimia 2.5 kwa wakala anayeuza umeme kupitia Selcom Paypoint hii ikimaanisha kwamba unapata 2500/- pindi unapouza umeme wenye thamani ya 100,000/- ambayo ndiyo faida na hii ilikuwa imewekwa kwa wale wanaoongeza salio kwa kutumia TIGOPESA ambapo makato ya kuongeza salio hilo ilikuwa ni bure kwa mujibu kwa maelekezo toka ofisi za Selcom ambayo ilisema kuwa gharama hiyo inabebwa na kampuni.
Lakini kuanzia jana tarehe 23 Januari imekuwa tofauti, pindi unapoongeza salio lenye thamani ya 100,000/- unakatwa 2500/- ambayo ndiyo faida unayostahili kupata pindi unapouza umeme umeme wenye thamani hiyo.
Tumejaribu kupiga simu kwa wahusika lakini hakuna majibu ya maani.
Hivyo kama kuna mamlaka zinazohusika tunaomba msaada kutokana na wizi huu unaofanywa.
Nawasilisha!