Selcom na meseji zenu za Lotto mnakera!

R Mbuna

JF-Expert Member
Dec 30, 2015
2,283
5,359
Habari zenu wanajamvi

Naomba kama kuna mtu anafanya kazi selcom anifikishie huu ujumbe ofisini kwao kuwa msg zao za kununua tiketi ya lotto zinanijazia memory ya simu yangu. Hivi hizi msg huwa mnatumia vigezo gani kuwatumia watu kwanza mimi situmii huduma za selcom kwa nini kila baada ya masaa kadhaa nakuta hizo msg zenu.

Kama mnausoma huu ujumbe naomba muache mara moja kunitumia hizo jumbe zenu yaani mimi naacha kufanya kazi za maana najua ujumbe wa maana ndio umeingia kumbe ..

690469695b1a0c95b0c167946ace42c4.jpg
.......

Nawasilisha
 
Kwanza ndio kina nani hao selcom,naona msg zao tu zinaingia twiii twiii
 
Dah afadhali ata umesema mimi yamenikera hayo majitu, mimassage yenyewe sisomi, wananijazia tu nokia yangu ya tochi na uwezo wake mdogo wa kutunza sms.
 
Kweli kabisa mkuu wanakera sana. Kuna wakati umetulia unatafakari au unafanya ishu muhimu ghafla mesiji inaingia unaacha shughuli zako unahangaika kutoa simu daaaaaa kumbe Loto/selcom
 
Dah afadhali ata umesema mimi yamenikera hayo majitu, mimassage yenyewe sisomi, wananijazia tu nokia yangu ya tochi na uwezo wake mdogo wa kutunza sms.
Dah hii kero kumbe ipo kwa watu wengi aisee. mi nilitaka kuwapigia voda simu niwaambie hii kero ila wakawa hawapokei simu, hii mamabo ina kera, wapuuzi sana

Pia kuna namba hii +255 901 76 1234 inakera sana inanipigia simu mara nyingi sasa
 
Nashauri tuanzishe chama cha watumia sim haya makampuni ya sim naona kama wanatunyanyasa sana na matangazo ya kila saa na hatuna wa kututetea TCRA ni kama branch yao vile.
 
Weka namba yako kabisa waione maana humu wapo, ili waufanyie kazi ujumbe wako! Pia wengine wenye hii kero namba zao ziwekwe ili wakome kabisa kuzitumia ujumbe hizo namba....
 
Umenunua tiketi yako ya LOTTO kwa droo ya kesho?Kadirio la fuba ni hadi 110m unaweza ukawa Mshindi!Nunua tiketi kupitia Wakala wa Selcom, Tigopesa au Mpesa sasa
 
Nashauri tuanzishe chama cha watumia sim haya makampuni ya sim naona kama wanatunyanyasa sana na matangazo ya kila saa na hatuna wa kututetea TCRA ni kama branch yao vile.
Mkuu tuanzishe kweli ila nshawahi utunza hazina
 
Habari zenu wanajamvi

Naomba kama kuna mtu anafanya kazi selcom anifikishie huu ujumbe ofisini kwao kuwa msg zao za kununua tiketi ya lotto zinanijazia memory ya simu yangu. Hivi hizi msg huwa mnatumia vigezo gani kuwatumia watu kwanza mimi situmii huduma za selcom kwa nini kila baada ya masaa kadhaa nakuta hizo msg zenu.

Kama mnausoma huu ujumbe naomba muache mara moja kunitumia hizo jumbe zenu yaani mimi naacha kufanya kazi za maana najua ujumbe wa maana ndio umeingia kumbe .......

Nawasilisha
Bora waambiwe. Wananikera sana mimi. SIZITAKIIII
 
Message zao kweli zimekuwa kero sana. Hivi hamna sheria inayozuia kampuni za simu kumtumia mteja matangazo ambayo hajajiunga nayo?
 
Ni kweli mkuu, na wanachouthi zaidi kila ukifanya transaction yeyote ya M pesa lazima wakutumie izo meseji!!!

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom