Sekondari ya Isimani yafungwa kwa walimu kukataa kutumiwa na Mheshimiwa Lukuvi

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,726
32,818
Shule ya Sekondari Isimani imefungwa,hapa ndipo yalipo makao makuu ya Tarafa ya Isimani na ilipokuwa ngome ya Chama cha Mapinduzi.Uchaguzi huu na wimbi la mabadiliko limeipitia mpaka Isimani, Upinzani dhidi ya CCM na makuwadi wake umeshika hatamu.

Mbunge wa miaka 20 mfululizo toka mwaka 1995 anayetafuta ridhaa ya kwenda mwaka wa 25 anakabiliwa na upinzani mkubwa sana.Hali ni tete kwa #WilliamLukuvi na chama cha Mapinduzi.

Wiki iliyopita Lukuvi ameamua kuishinikiza Serikali na mamlaka husika kuifunga Shule ya Sekondari Isimani baada ya walimu na mkuu wake wa shule kukataa kutumika kisiasa kwa kuibeba CCM na walimu wake kutumika kuipigia chapuo CCM na wagombea wake wa ngazi ya Jimbo.Walimu wamekataa kutumika kugawa kofia na T-shirt ili kuhudhuria mikutano ya CCM na kujaza "nyomi" mahali Lukuvi anapohutubia.

Hali hii imefanya mkuu wa Shule ya Sekondari Isimani ndugu AIDAN KAPINGA kuvuliwa ukuu wa shule na "kutupwa" kuwa mwalimu wa kawaida katika shule ya Sekondari LYANDEMBELE huko Ifunda Iringa Vijijini.

Baada ya tukio hilo walimu na wanafunzi waligoma kwa siku kadhaa kushinikiza mwalimu wao mkuu arudishwe sbb anaonewa na hana makosa,hali hiyo ikalazimu Lukuvi aamrishe shule hiyo kufungwa na watoto warudishwe nyumbani bila kujali kuwa Vijana wa kidato cha nne wapo ktk maandalizi ya Mitihani yao ya mwisho ya Taifa.

Mpaka sasa hali si shwari katika eneo la Isimani na Vitongoji vyake.Serikali ya CCM na Lukuvi wasiingize "siasa" katika mambo ya elimu na uhuru wa watu kujiamlia mambo yao,Wananchi wa Isimani wanakabiliwa na matatizo mengi sana. watatumia tukio hili la watoto wao kunyimwa nafasi ya kujiandaa na mitihani kuiadabisha Serikali na chama chake.

William Lukuvi asitumie nguvu kuyazuia mabadiliko bali atumie nguvu kuonyesha maendeleo.Bring back our Children to School
 
Ndo madhara ya viongozi wa serikali wasio na elimu,Lukuvi shule hajaenda ndo mana haoni umhimu wa shule,
Msimpe kura kwa namna yoyote ile
 
Ndiyo maana tunataka mabadiliko!!!!!!!! Miaka 54 ya utawala, imewafanya Viongozi wa Serikali ya CCM, kama Lukuvi, kulewa madaraka. CCM tupa kuleeeeeeeee! Lukuvi tupa kuleeeeeeeeee! Rais wetu ni Lowassaaaaaaaaaaaa, na wabunge na madiwani kutoka UKAWA! PIGA KURA, LINDA KURA!!!
 
Teh teh ismani sio ngome ya lukuvi tena, madiwani wa ccm wa napumulia mashine, OPERATION ONDOA CCM
 
Makosa ni ya wananchi wenyewe, lakini bado wananchi wana nafasi ya kurekebisha makosa yao hapo kesho kwa kupigia kura zao kwa lowassa na ukawa
 
Shule ya Sekondari Isimani imefungwa,hapa ndipo yalipo makao makuu ya Tarafa ya Isimani na ilipokuwa ngome ya Chama cha Mapinduzi.Uchaguzi huu na wimbi la mabadiliko limeipitia mpaka Isimani, Upinzani dhidi ya CCM na makuwadi wake umeshika hatamu.

Mbunge wa miaka 20 mfululizo toka mwaka 1995 anayetafuta ridhaa ya kwenda mwaka wa 25 anakabiliwa na upinzani mkubwa sana.Hali ni tete kwa #WilliamLukuvi na chama cha Mapinduzi.

Wiki iliyopita Lukuvi ameamua kuishinikiza Serikali na mamlaka husika kuifunga Shule ya Sekondari Isimani baada ya walimu na mkuu wake wa shule kukataa kutumika kisiasa kwa kuibeba CCM na walimu wake kutumika kuipigia chapuo CCM na wagombea wake wa ngazi ya Jimbo.Walimu wamekataa kutumika kugawa kofia na T-shirt ili kuhudhuria mikutano ya CCM na kujaza "nyomi" mahali Lukuvi anapohutubia.

Hali hii imefanya mkuu wa Shule ya Sekondari Isimani ndugu AIDAN KAPINGA kuvuliwa ukuu wa shule na "kutupwa" kuwa mwalimu wa kawaida katika shule ya Sekondari LYANDEMBELE huko Ifunda Iringa Vijijini.

Baada ya tukio hilo walimu na wanafunzi waligoma kwa siku kadhaa kushinikiza mwalimu wao mkuu arudishwe sbb anaonewa na hana makosa,hali hiyo ikalazimu Lukuvi aamrishe shule hiyo kufungwa na watoto warudishwe nyumbani bila kujali kuwa Vijana wa kidato cha nne wapo ktk maandalizi ya Mitihani yao ya mwisho ya Taifa.

Mpaka sasa hali si shwari katika eneo la Isimani na Vitongoji vyake.Serikali ya CCM na Lukuvi wasiingize "siasa" katika mambo ya elimu na uhuru wa watu kujiamlia mambo yao,Wananchi wa Isimani wanakabiliwa na matatizo mengi sana. watatumia tukio hili la watoto wao kunyimwa nafasi ya kujiandaa na mitihani kuiadabisha Serikali na chama chake.

William Lukuvi asitumie nguvu kuyazuia mabadiliko bali atumie nguvu kuonyesha maendeleo.Bring back our Children to School

Jiandae kwenda kuchunga ng'ombe tu.
 
Huyu AIDAN KAPINGA nampata sana huyu jamaa,Tulikuwa nae UDSM miaka hiyo,Jamaa wa misimamo sana sana,bila shaka amekataa kuburuzwa,safi sana Kapinga,endelea kusimamia kile unachokiamini,wanasiasa wapo tu na wanapita,lkn taaluma yako itadumu...Jenga heshima na historia yako,Historia itakukumbuka
 
Well said mkuu
 
Safi sana,mwl ameitendea haki taaluma yake!.
MZAZI ALIEMSOMESHA hajutii ada yake aliyomlipia
 
Back
Top Bottom