Mwaka wa 2017 umeisha kukiwa na matukio mengi ya wanasiasa hasa wabunge na madiwani kuhama vyama vyao. Huenda pia mwaka huu matukio kama hayo yakatokea tena kuliko hata ya mwaka jana.
Nimekaa na nikiwaza na nashindwa kupata majibu ya kina. Wanasiasa hawa wanapohama watu wengi husema ni haki yao ya kikatiba kufanya hivyo, na hakuna mamlaka yoyote ile inayowapinga au kuwazuia kufanya hivyo, kwa sababu wanatumia haki yao ya kikatiba na uhuru wa kujieleza na kutoa maoni yao. Lakini wanapojivua nyazifa zao walizopewa na wananchi hawarudi tena kwa wananchi kusema wanajiudhuru nyazifa na imani waliyopewa na wanachi. mbaya zaidi hawaoni kuwa wanawabebesha wananchi mzigo wa gharama za kurudia uchaguzi, kwa pesa za kodi za wananchi.....
Jambo kubwa lililonifanya nitafakari ni hiki kitu cha uhuru wa kutoa maoni na kupata habari ambayo pia ni haki ya kikatiba ya kila mtu. Sasa inakuaje mtu anapotoa maoni yake au anapohitaji kupata au kutoa habari anatafasiriwa kuwa ni mchochezi anatoa maneno ya uchochezi? sasa hii haki ya kikatiba ya uhuru wa kutoa maoni iko wapi? au waliopo kwenye serikari zote ndo huwa wanahii haki tu? je hii haki haipo kwenye katiba imefutwa? au kuna katiba mpya ambayo hairuhusu watu kutoa maoni?
WHERE IS THE RIGHT OF FREEDOM OF SPEECH?