Seiko 5 original japan 200000

Zinauzwa Posta pale round about,,,mi nilikua nayo sema imeshaisha ila nimehamia humu ss hivi


Sent from my iPad Air using JamiiForums mobile app
 
Seiko 5 original zinapatikana round about ya posta, nilipoenda kuulizia mara ya mwisho zilikuwa ni laki nne na sitini na nane (468,000), watu wengi hawazifahamu hizi saa, hizi ndizo saa walizotumia mababu zetu kipindi hicho, ni roho ya paka, haziingii maji, hazitumii betri, ni automatic, unapoishika na kuitingisha ringi yake ya ndani inazunguka, ringi ikizunguka saa inaanza kutembea, unatumia na kumrithisha mwanao, na yeye anatumia na kumrithisha mtoto wake, hutoadaiwa betri wala kuona imesimama, hapa mjapan alitulia kutengeneza hizi saa
 

Ya kwangu hiyo tokea niirithi ni mwaka wa nne sasa, hakuna nilichobadilisha, isahau ndani hata mwaka, ukiishika na kuitingisha tu unakuta mashine inaanza kutembea, siiuzi kwa kweli, muundo kama huu kwa sasa huzipati madukani zimeshapotea.
 

well said mkuu...mimi mzee wangu alinunua mwaka 1990 ameitumia akaja kuniachia mm mwaka 2008 nkaitumia mpaka leo hii ipo inafanya kaz ila sema tu imechakaa ndio maana nmeamua kuiacha hizi saa cjapata kuona kwa kweli.
 
Seiko 5 na Rolex zimemwagwa nyingi sana feki wakuu kuweni makini sana, uthibitishaji wa hizi saa kama ni feki au original unaiweka kwenye ndoo ya maji hata nusu saa, ukiona imeingia maji ujue ni feki ya kutupa, na feki zinasumbua sana, za rangi ya gold zinapauka haraka sana na hazichelewi kusimama, original unatumia miaka mia moja, unarithisha na mtoto wako naye anamrithisha mwanae. Unaweza ukauziwa saa ya Rolex 150,000 ukaona umepata kumbe umepatikana, huwezi kuipata Rolex kwa 150,000, kama unaweza mwambie muuzaji kama ana uhakika ni original achukue ndoo ya maji atumbukize saa yake, baada ya dakika kumi ikitoka iko safi hiyo saa lakini ukiona ukungu wa maji kwenye kioo tupa mbali hakuna kitu feki hiyo.

KUWENI MAKINI SANA JUU YA ROLEX ZIMEMWAGWA NYINGI SANA FEKI!!! ANGALIZO!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…