Seif Khatib: Kuzomewa Ni Gharama Ya Siasa

Kweli mambo yamekuwa magumu Bongo. Siasa za Kudanganya watu sasa zimeanza kuwa issue. Kama Komba ameanza kulazimisha watu washangilie kwenye supu imeingia nyongo.
 
Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Mh. Seif Khatib yuko Iringa. Yeye na msafara wake wamekuja Iringa katika kile kinachoitwa mkakati wa chama tawala kuwatuma makada wake nchi nzima kuondoa sumu waliyopewa wananchi kutokana na ziara za viongozi wa vyama vinne vya upinzani nchi nzima wakiongozwa na Mbunge Zitto Kabwe ambayhe hoja yake ya Mkataba wa Madini wa Buzwagi ilimwacha akionyeshwa mlango wa kutokea nje ya Bunge na hatimaye kumpa umaarufu mkubwa kama mwanasiasa.

Jioni ya jana pale Ukumbi wa Siasa ni Kilimo, Waziri Khatib aliongea na Wajumbe wa kamati ya siasa Mkoa, Wajumbe wa Halmashauri Kuu na watendaji wa kata.

Mh. Seif Khatib anasema:

-Kiongozi kuzomewa ni gharama ya siasa. Ukiingia kwenye mchezo wa siasa hujiandae kwa hilo.
-Sisi tuna kazi ya kufanya, wapinzani hawana kazi
-Sisi tuna maswali ya kujibu 2010, wapinzani hawana
-Wapinzani hawapendi tufanikiwe
-Msiingie kwenye mtego wa wapinzani
-Wapinzani wapuuzeni, simamieni ilani ya chama
-Tuna ilani inayotekelezeka


Kwa habari zaidi katika picha, tembelea; http://mjengwa.blogspot.com
Lissu sijui analijua hili
 
Back
Top Bottom