Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
MTANGAZAJI: Wewe ni mtumiaji mzuri sana wa mitandao ya kijamii, na tumeshuhudia siku za karibuni watuamiaji wenzio wa mitandao wakikamatwa na kufikishwa mahakamani. Kwanini wewe hukamatwi?
MALISA: Kwanini nikamatwe?
MTANGAZAJI: Kwa sababu umekuwa ukiikosoa serikali mara kwa mara.
MALISA: #Mosi; Ni kweli kuwa nimekua nikiikosoa serikali mara kwa mara lakini hii haimaanishi kwamba huwa siipongezi. Serikali inapofanya vibaya huwa nakosoa na inapofanya vizuri huwa napongeza.
Mimi ni miongoni mwa watu waliompongeza Rais Magufuli kwa kufuta sherehe za siku ya uhuru na kulekeza fedha zile zitumike kujenga barabara ya Mwenge hadi Morocco. Lakini ni mimi huyohuyo niliyemkosoa Rais Magufuli aliporuhusu mbio za Mwenge wakati "essence" ya kufuta sherehe za Uhuru ni ileile ya mbio za Mwenge (kubana matumizi).
Tena Mwenge ni gharama kubwa zaidi kuliko gharama za sherehe za uhuru. Nilimkosoa Rais kuruhusu mbio hizi na niliweka "Economic analysis" inayoonesha athari za mbio za Mwenge kiuchumi.
#Pili; nipende kusema kwamba kukosoa si dhambi na haijawahi kuwa dhambi. Kwahiyo sioni sababu ya kukamatwa kwa kukosoa. Jambo la msingi ni kukosoa kwa staha, bila matusi, lugha za kuudhi wala kuvunja sheria za nchi. Unapokosoa zingatia maadili ya jamii, na sheria za nchi. Hata kama sheria zilizopo ni mbaya lakini tukosoe kwa kuziheshimu huku tukipiga kelele zirekebishwe.
#Tatu; unapokosoa lazima ujue "motive" yako. Kwanini unakosoa.? Ili iweje? Umetumwa na dhamiri yako au umetumwa na watu/taasisi fulani? Lengo lako ni nini? Unataka nini kitokee baada ya kukosoa? Unakosoa kwa maslahi ya nchi au kwa maslahi binafsi?
Kuna watu wanakosoa ili kuchochea fujo (Provoking critics), kuna watu wanakosoa kwa kushambulia (attacking critics), kuna watu wanakosoa ili kupendelea upande wanaofanana nao mawazo (judgemental critics), na kuna watu wanakosoa kwa nia njema ya kusaidia nchi (critisism with good faith).
Kwa hiyo hoja si kukosoa, hoja ni kwanini unakosoa.
Mimi naamini kwamba huwa nakosoa "in good faith", na kwa maslahi ya nchi. Nina uhakika kama Rais Magufuli huwa anasona maandiko yangu au kama watu wa karibu yake wanaonisoma wanajua wazi kwamba sijawahi kukosoa kwa nia mbaya (critisism with malice aforethoughts). Lengo langu ni kuona Tanzania ikisonga mbele. Kwangu mimi Tanzania ni muhimu zaidi kuliko vyama vya siasa.
Kwa hiyo serikali haipaswi kukasirika kwa sababu nakosoa, badala yake inatakiwa kufurahi kwa kuwa naisaidia kuipa changamoto mpya za kuiwezesha Tanzania yetu kupiga hatua. Kwahiyo sioni sababu kwanini nikamatwe?
Watu wanaokosoa "in good faith" hawatakiwi kukamatwa. Hawa ni "think tank" ya taifa, wanatakiwa kuwezeshwa ili kuisaidia nchi, maana wanaona mahali ambapo wengi wetu hawawezi kuona. Huku kwetu tunaweza kuwakamata na kuwatesa, lakini nchi zilizoendelea wanawatumia kwa maslahi ya taifa.!
Malisa G.J