Sehemu ya mabaki ya Titan baada ya kuopolewa

Sehemu ya mabaki ya Titan baada ya kuopolewa

Billy the Goat

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2013
Posts
566
Reaction score
353
Baadhi ya Mabaki ya Chombo cha Titan mali ya kampuni ya utalii wa bahari iitwayo Oceans Gate, kilichopata hitilafu na kupasuka Kwenye kina kirefu cha bahari na kusababisha vifo vya watu watano waliokua wakienda kuangalia mabaki ya Meli ya Titanic, yameanza kuopolewa kutoka chini ya bahari Kwa jitihada za jeshi la wanamaji la Marekani wakishirikiana na makampuni binafsi. Taarifa zinasema utafutaji na uopoaji wa mabaki hayo ambao wataalamu wanasema utagharimu mamilioni ya dola, utafanyika ili kuopoa kila kitakachoweza kupatikana ili uchunguzi rasmi ufanyike kujua sababu hasa za ajali hiyo ili pia hatua za kisheria zichukuliwe ikiwa ni pamoja na marekebisho katika Sheria zinazosimamia safari na vyombo vya Aina Hiyo ili kuzuia kutokea Kwa ajali kama hizo.

UPDATE

Taarifa kutoka Kikosi cha Coast Guard cha Marekani zinasema mpaka sasa wameopoa Baadhi ya mabaki ya mwili yanayosadikika kuwa ni ya binadamu, na yamepelekwa Marekani kutokea pwani ya St. John's Newfoundland Kwa uchunguzi zaidi

Mkuu wa Kikosi cha U.S Coast Guard Kapteni Jason Neubauer amesema "Ninashukuru kwa usaidizi ulioratibiwa kimataifa na mashirika ya kimataifa ili kurejesha na kuhifadhi ushahidi huu muhimu kutoka Kwenye kina kirefu cha bahari. Ushahidi huo utawapa wachunguzi kutoka mamlaka kadhaa za kimataifa ufahamu wa kina kuhusu chanzo cha janga hili. Bado kuna kazi kubwa ya kufanywa kuelewa mambo yaliyosababisha janga hili kubwa la TITAN, kazi ambayo itasaidia kuhakikisha janga kama hilo. haitatokea tena."

20230629_101126.jpg
20230629_101128.jpg
 
Back
Top Bottom