Sera ya majimbo pamoja na uzuri wake inatakiwa uwepo mfumo wa kuihimili ambayo kwa Tanzania bado hatjafikia kwani wal si rasilimali tu bali uchumi na mfumo mzima wa uendeshaji. Kuna nchi zinazoendesha mfumo huu, japo zimeendelea, manung'uniko kutoka kwa majimbo yenye uchumi mzuri kubeba dhaifu k.m Ujeumani na Ubelgiji, nakiri sijui Marekani wanaendeshaje kwani naowana mfumo huu. Hivyo kabla ya kuushabikia tuone wengine wanaendeshaje pengine tunaweza kuibua wa kwetu pia.
Swala la gesi ni la kisiasa zaidi, na wa kulaumiwa ni CCM wenyewe kwa ahadi zao wakati wa uchaguzi. Pengine hilo ni onyo kwa uchaguzi jao na Rais ajaye asiahidi mno mambo yasiyotekelezeka kwa kuwaaminisha wananchi kuwa inawezekana. Kinachogomba hapa, kwa maoni yangu ni swala la kuangalia faida kiuchumi zaidi kuliko maendeleo endelevu kwa sehemu husika. Kwa wawekezaji wanataka faida mapema zaidi iwezekanavyo jambo ambalo halitakiwi kukaziwa na serikali. serikali itazame faida kwa siku za mbele yaani kuwa na economic center moja au kuzitawanya sehemu mbalimbali! Kama serikali la pili ndio sehemu yake japo itahusisha uwekezaji kwenye miundo mbinu mikubwa zaidi kuliko sasa. Yaani kujenga mitambo ya ufuaji umeme Mtwara itabidi serikali ijenge pia mfumo wa umeme mkubwa, 'gridi' ambao wanaukwepa!! kuna mradi wa Mtwara corridor wa kuendeleza bandari ya Mtwara mafanikio yake kwa kiasi kikubwa yataokana na kuongezeka kwa shughuli za kiuchumi ya eneo hilo. Je serikali yetu itaendelea mpaka lini kfikiria kama cash bugdeting badala ya strategic development.
Serikali inaweza kujitoa katika kuendesh biashara lakini si kuendesha na kuongoza uchumi!! tukiachia seekta binafsi iendeshe uchumi, kama inavyotaka kuwa sasa, usalama wa Tanzania kama taifa hauwezi kuwa guaranteed. Sera za vyama vya siasa iwe maendeleo kwa wananchi tubishane jinsi ya kuyafikisha bila kubomoa mfumo, labda uwe umeoza. Kwa maoni yangu gesi kusambazwa sehemu nyingine hakuepukiki kwani matumizi eneo la kusini tu hayakidhi uwekezaji lakini umeme ufuliwe Mtwara. Na hakika watu wa Mtwara wanajua kilichotokea Kidatu ambapo umeme ulisafirishwa Dar na sehemu nyingine. Asante mzee wa kazi Sokoine aliposimamia kwa miezi mitatu tu, jambo amablo kwa miaka kumi 'halikuwezekana', umeme ukafika Mang'ula na sehemu nyingine. Wat wanakumbukumbu kuliko sirikali!!