Salahan
JF-Expert Member
- Sep 10, 2014
- 2,963
- 3,680
13 Reasons Why (imepewa ubunifu wa jina Th1rteen R3asons Why katika video)ni tamthilia ya ki amerika iliyotolewa(kuuzwa) katika mtandao na televisheni.Imetokana na kitabu cha tamthilia kilichoitwa THIRTEEN REASONS WHY cha mwaka 2007 kilicho tungwa na mtunzi Jay Asher.Kikakubalika na Brian Yorkey kwa Ajili ya kuonyeshwa NETFLIX. Tamthilia imewahusisha wanafunzi wa elimu ya juu,Clay Jansen na rafiki yake Hannah Baker,ambaye alijiuwa baada ya kuzongwa na kila la kumtia huzuni,ambayo yametokana na kila aliyemtaja mmoja baada ya mwingine hapo shuleni.Boxi la kanda zilizo rekodiwa na Hannah kabla ya kujiuwa zinafafanua sababu kumi na tatu kwa nini ameyasitisha maisha yake.
Msimu wa kwanza (season 1) ina jumla ya sehemu(episodes) 13.Tamthilia imeanza kurekodiwa chini ya televisheni ya NETFLIX mwishoni mwa 2015 chini ya usimamizi wa projuza Gomez.Msimu wa kwanza ulianza kuonyeshwa duniani kote kupitia televisheni ya NETFLIX tarehe 31/03/2017 kwa jina "13 REASONS WHY".
Tamthilia imekubalika na kupata muitikio chanya toka kwa watazamaji na kupewa nyota za juu kwa wingi(star rate) na ina mapitio mazuri na kushika nafasi za juu za Mapitio/maarufu( trending)
Imegusia masuala ya kisheria kama ubakaji na kujiuwa.Mwezi wa 5 2017 imetolewa taarifa ya kutolewa kwa mwendelezo wa msimu wa pili (Second season) inayotazamiwa kufika 2018.
MDOKEZO
Kijana Clay Jensen anarudi nyumbani toka shuleni na kukuta boxi lisilo na anuani ya mtumaji likiwa baraza ya nyumba yao.Ndani ya box anakuta kanda (cassette) saba zilizorekodiwa pande zote mbili na Hannah Baker,binti ambaye anasoma nae darasa moja na walio na mahusiano ya kimapenzi yasiyo wazi(unrequited love),ambaye alijiuwa wiki mbili zilizopita.Katika kanda,Hannah anasimulia hisia zake juu ya yale aliyopitia,anaelezea sababu 13 kwa nini amechagua kuyasitisha maisha yake.
Utangulizi wake upo wazi:anaanzabkwa kusema;kila mtu aliyepata kanda ni miongoni mwa sababu za yeye kujiuwa,na kila mmoja baada ya kumaliza kusikiliza kanda ni lazima ampe mtu mwingine anayefuata.Kama mtu yeyote atakaye taka kusitisha kufanya ivyo(kujitoa katika mtiririko) basi kanda inayo mhusu mtu huyo itatolewa kwa watu wote wengine (public) wakajua.Kila kanda imemlenga mtu katika iyo shule na kuelezea vipi anahusika na kifo kilicho mbidi kukikabili (inevitable suicide)".
Season one inashika ikiwaacha watazamaji na kiu kutaka kujua nini kinafuata na ninank hasa kahusika na kujiuwa kwa Hannah.Je ni uongozi wa shule...Je ni hao alio wataja tu aliowataja katika kanda....nk.