ray57,
Scripting language ni subset ya programming languages. Hivyo scripting languages pia zinaitwa programming languages.
Tofauti ya matumizi ya maneno scripting na programming ni wether zinakuwa
interpreted au
compiled kabla ya kufanya kazi. Inabidi kwanza uanze na maana ya terminologies hizi mbili, katika hili naungana na mdau aliyekushauri uwe rafiki wa Google.
Lakini kwa mfano rahisi. javascript kwa kiasi kikubwa (tutarudi hapa) ni interpreted language, ukishaprogram ina-run hapo hapo kwenye browser bila ugumu wowote, labda tu itabidi u-refresh page. Upande wa pili, C ni compiled language, ili i-run, inabidi upitie hatua ya compilation ndio ita-run.
tofauti nyingine rahisi ni kuwa code ya scripting language inaonekana kirahisi kwa kuangalia tu HTML file, lakini programming language kama java au C huwezi kufanya hivyo, kwa sababu code imefichwa.
Tukirudi pale juu, nikutahadharishe tu vile vile kuwa kutokana na maendeleo ya teknolojia, siku hizi languages nyingi ambazo traditionally zilikuwa zinaangukia kwenye kundi mojawapo (scripting au programming) sasa hivi zina uwezo wa kucheza pande zote. Hivyo suala la kama language ni scripting language au programming language linakuwa suala la matumizi yake na si aina kihivyo.
Mfano: traditionally Javascript ilikuwa ni scripting language lakini kwa sasa inaweza kutumika kama programming language kupitia mavitu kama v8 engine, node.js n.k, vile vile languages kama C ambazo ni compiled ones, wako mageeks wanatengeza interpreter na inaweza ku-run kama interpreted language.