Scotland: 'No vote' haina maana 'No change'


Mchambuzi nakushukuru sana kwa kutudondolea hizi takwimu. Member mwenzetu Kobello ambaye anaona tunaotilia viulizo muundo wa Muungano wa sasa tuna matatizo fulani, labda anaweza kutueleza hapa takwimu hizi zinaeleza nini.

Wakuu labda tukubali kuwa hatujui sababu ya muungano, tukubaliane tu kuwa tujaribu kutafuta sababu za CCM kung'ang'ania muungano wa namna hii, na muungano una manufaa gani. Kimahesabu naweza kusema kwa kili yangu fupi naona ni hasara kwa bara, au ni unyinyaji wa wazi. Lakini najua kabisa watu wenye akili timamu wanajua kabisa this is monkey business. But the question is, wanajua kuwa ni ujinga na wakati huo huo wanafanya kitu ambachi wanajua ni ujinga na sisi tunajua ni ujinga, labda kuna kikubwa zaidi ambacho hatukijui ambacho kinawafanya wafikie maamuzi ambayo simple logic na common sense inasema haifai.

Kama Nyerere alivyowahi kusema "mimi sio kuku, sitagi mayai lakini mayai mabovu nayajua".

Sisi si wanahisabati lakini hesabu mbovu tunaweza kuzijua. Nadhani kama make up ya wazanzibar kwenye muungani ni asilimia 3 mgao wa nafasi za ajira kwenye mambo ya muungano uwe asilimia 3 kwa 97? Kama hii haifai basi nufaika ya Zanzibar ilingane na asilimia ya mchango wake kwenye muungano. Zaidi ya hapo ni usanii tu.
 


Mkuu Nguruvi haya maswali naona tuna haja ya kuulizana wenyewe huku bara. Nani alifikia uamuzi wa kutuingiza mkenge kiasi hicho na alitumia kigezo gani. Tunatakiwa kuwajibishana wenyewe kwenye ujinga huu. Wabara tunaumia kwa kulipia political fantancy ya baadhi ya wanasiasa.
 
Watanganyika mnayaona haya?
Sisi tukiuliza tunaambiwa tunachuki. Je, hapa ambapo namba zimezungumza mtasemaje?

Nikisoma ufafanuzi wa Mchambuzi, Napata picha moja kubwa.
Kwamba mzanzibar mwenye sifa hatakosa kazi labda atake.


92,000 kwa population ya 1.2M wakiwemo watoto ni sehemukubwa sana.
Tena wana raha nyingine ya kuchukua zile za 79% za Watanganyika.

Kwamba, mznz aliyekosa 21% bado ana nafasi katika 79% ya Watanganyika kwa jinala Watanzania.


Yote haya hayakujulikana kwasababu wznz walikuwa wazuri sanawa kuzusha uongo na umbea kuwa wanaonewa. Hivi katika hali hii kuonewa kupowapi? Nani anayeonewa, Mtanganyika au mzanzibar?
Na kila tunavyosonga mbele maswali yanazidi kuongezeka.

Hilini swali la tatu. Naomba mtu aje hapa atupe justifications kwanini wazanzibarwanaosoma elimu ya juu wanasoma bure na kwanini Watanganyika walipe mikopo?


b) Kwanini wazanzibar wanaodhaminiwa na SMZ wanarudishamikopo, lakini wale wanaodhaminiwa na JMT hawarudishi mikopo?
Niweke sawa

  1. Kuna uhalali gani wa znz kupewa 4.5% ikiwa mudaulikuwa miaka 5 tu.
    (b) Kuna hesabu gani zilizotumika kufikia 4.5 ya pato laTanganyika?
  2. Asilimia 21 ya ajira zisizo za muungano, formulagani imetumika.
    (b) Kwanini mzanzibar apewe nafasi halmashauri ya mji, jiji aumanispaa.

    Kwanini aajiriwe wizara ya kilimo, Afya, miundo mbinu, bandari, TBSna eneo linguine lisilo la muungano tena akipewa 21% halafu ubwete wa 79%

  3. Kwanini wznz wanaodhaminiwa na JMT hawarudishimikopo kama wenzao wa Tanganyika.
    (b) Kwanini wznz wanaodhaminiwa na SMZwarudishe mikopo na si kwa JMT


    Hapa Watanganyika wafunguke macho.Tutakapo waambia kuwa wizara ya ulinzi inayokula trilioni moja, wizara ya mambo yandani trilioni moja na wizara ya mambo ya nje nusu trilioni ni mzigo waowenyewe, sijui tutaambiwa tunachuki au vipi.


    Katika muundo wa S2, Watanganyika mtaendeleakulipa kodi kwa ajili ya nchi jirani ya znz.
    Na wznz wataendelea kuleta madaiyao kila uchao kwasababu ninyi Watanganyika mumekubali kuwa shamba la bibi.

    Mnawekeza mahali msipotarajia kupata dividend hata siku moja.
    Si walisikia kunamadebe 57 ya mafuta wakakimbia kuondoa!


    Njia wanayotumia ni rahisi sana. Wznwanakuja na invoice hazina wakiwa na jina la Tanzania. Wakishapata chequewanarudi znz kwa jina la Uzanzibar na si Tanzania.
    Hiyo Tanzania ni yenuWtanganyika na bill zenu
    Mwigulu Nchemba Nape Nnauye Mkandara Happy Feet EMT Bongonder Alinda gfsonwin Ritz zumbemkuu Ngongo
 
Mkuu , ni kweli kabisa.
Ukiangalia wazanzibar wanatumia udhaifu wa viongozi wetu vema sana.
Kwanza walijenga mazingira ya znz kuonekana ni sehemu muhimu sana na hivyo kila walipodai walipewa.

Pili, wakajenga mazingira kuwa wanaonewa, kila wakidai wanapewa.
Yote hayo yamedhihirika pasi na shaka kuwa znz si muhimu, haionewi na ni mzigo mkubwa tu

Viongozi wetu hata sijui wanafikiri nini.
Mfano, aliyetoa 21% waliojipangia wznz ni Kikwete.Aliyetoa 4.5% kwa miaka 5 ni Mkapa.
Yote wazanzibar wameyageuza kama haki yao.

Mfano, mznz anafungu maalumu katika kupata pesa za bure za elimu ya juu.
Hawagombei kama Watanganyika, hivyo mznz mwenye division 4 ya znz anapata pesa za elimu ya juu ili kujaza nafasi walizotengewa.Huku Tanganyika, watoto wa walipa kodi wenye divi 2 au 3 wanakosa mikopo.Imagnie mikopo.

SMZ inadhamini wanafunzi 800 ambao lazima warudhishe mikopo kabla ya kwenda kusoma zaidi.

JMT ambayo ni Tanganyika, wanadhamini wazanzibar 1,700 wanaopewa pesa za buree za Mtanganyika.

Huko kwao SMZ inaona uchungu lazima hao 800 warudishe mikopo.
Wakivuka bahari ni ubwete tu , ndio maana miongoni mwa hao 1,700 wanakuja hata div dah! kwasababu wznbz hawana hasara. Wanaleta tu

Anayeidhinisha pesa hizo za buree kwa wznz na mikopo kwa walipa kodi wa Tanganyika ni hawa akina Mwigulu Nchemba wanaodai ni watoto wa wafugaji, wana uchungu.
Uchungu upi ikiwa mnaandika cheque za bure kwenda nchi jirani ya Zanzibar.
Uchungu gani ikiwa hamuoni uchungu na pesa zinazotiririka kwenda znz bila formula.

Hivyo tatizo ni viongozi wa bara ambao wameridhika kuwa znz wapate wanachotaka tena kama haki yao.

Leo ajira 21% wamegeuza ni haki yao. 4.5% wamegeuza ni haki yao.
Elimu ya juu nafasi 1,700 zizsizo na gharama wamegeuza ni haki yao.

Haki wasiotaka kuisikia masikioni ni kuchangia muungano au kuwajibika katika muungano. Hiyo wazanzibar hawataki.

Wa kulaumiwa hapa si wznz , ni watanganyika waliokubali kulipa kodi kwa ajili ya nchi jirani ya znz.

Tukindelea na mfumo wa S2. wao watatumia jina kuja kupora kila siku.
Ni lazima Watanganyika waamke, waone haya! si madogo.

Yaani pesa zinazokwenda znz peke yake zinatosha kabisa kuhudumia wizara ya ulinzi ya Tanganyika kwa mwaka 1 bila msaada au mkopo. Hizo zinatiririka kwenda nchi jirani ya znz wakitoa misamaha ya kodi, wakilala bila kukusanya kodi. Mjomba Tanganyika atalipa bill.

Nakubaliana nawe, Watanganyika lazima waone haya! Hatuwezi kuendelea kuwa na kataifa ndani ya taifa kenye kuchukua rasilimali bila kuwajibika. Hatuwezi kuwekeza mahali pasipo na manufaa hata siku moja.

Watanganyika mnayaona haya?
 

Nafikiri nimekukata kiu ya manung'uniko yako kwa ku RED majibu yangu.

Je una ziada? basi Bismillah

 

Kuhusu hili la JFC nilitaka kukusaidia sana kama ungebahatika kujibidiisha kidogo tu na kutafuta ripoti yao waliompa Rais kikwete kwa utekelezaji wa majukumu yao ambayo inapage zaidi ya 120 imesasambua mengi sana kwa wataalamu hao waliangalia nyanja zote za uchumi wa nchi hizo mbili mapato yake na matumizi yake lakin walikuja mpaka kuangalia stuffing nzima na uwiano wake na kuja na ripoti mahili sana AMBAYO SERIKALI YA JMTZ MPAKA LEO IMESHINDWA KUTEKELEZA IKIWAMO KUWAPA MAJUKUMU YAO KAMA WALIVYOPENDEKEZA.

Huu ni uwanja mfupi sana lakin ni vizuri tafuta hiyo ripoti uipitia utajifunza mengi na nadhani itakata kabisa manung'uniko yako
 

Nafikiri unajua mengi kidogo kuhusu hii formula lakin unapenda tu na kutaka kuuficha ukweli.

Mimi nilitaka nikusaidie. Ukitaka kujua kwa kina zaidi hii 4.5% ilitokea wapi unatakiwa urudi nyuma sana na kuanza kuangalia kuanzishwa kwa BOT ma mchang wa kila nchi kwa maana ya share za kila nchi katika uanzishwaji wake.

Lakin pia kufa kwa Bank ya sarafu ya afrika mashariki na mgao wa share zake kwa nchi wanachama ambapo Znz alikuwa mwanachama na Tgk alikuwa mwanachama lakin share zote zikatumbukizwa katika BOT.

Wataalamu wa JFC hawakudandia hiyo formula kwani nao waliangalia kwa kina sana hizo share za kila nchi na nyanja nyingine za uchumi wa nchi hizo mbili na kubariki formula hiyo.

suala mbalo kila wakti unalikwepa.
KWANINI BUNGE LA JMTz LILIPITISHA SHARIA YA KUUNDWA KWA JFC na rais akaikubali itumike LAKIN MPAKA LEO SERIKALI YA JMTZ INASUASUA KUTEKELEZA SHARIA HIYO?

 
Basically umekubaliana na hoja za Mchambuzi kuhusu kuanzishwa kwa BoT na JFC na majaukumu yao.
Hujajibu hoja bali kuleta hadithi.

Ahsante tumekusoma
 
Tunaendelea kuwaeleza Watanganyika wasichojua na ambacho sasa wanakijua vema sana.

Barubaru mapato ya znz ni bilioni 400 kwa mwaka. Ukifahamu hilo utakuwa umepata majibu mengi.
Huna hoja za formula afadhali Mkandara kajikaliia kimya.

Kwa taarifa yako, Watanganyika hawahitaji ku-vote kwasababu muungano uwepo usiwepo hawapotezi lolote.
Wanachopoteza sasa ni matumizi ya jina Tanzania kuhalalisha wizi. Hili ndilo wanatakiwa kulipiga vita kali sana.

Nimekuuliza swali rahisi sana la tatu
Kuna uhalali gani wznz wasome bure ndani ya JMT wakati walipa kodi wa Tanganyika wenye pesa zao wakisoma kwa mkopo.

Kuna uhalali gani wa SMZ kukusanya madeni ya mikopo kwa wanafunzi 800 inaowadhamini, huku wale 1,700 wakisoma bure ndani ya Tanganyika. Hili ni rahisi kwako

Kuhusu 21% na 4.5% hilo usijibu tena huba majibu. Period.
 

Mkuu wangu umetumia lugha ya kidiplomasia lakini ukweli ni kwamba ukiangalia ukubwa wa Zanzibar na Idadi ya Wakaazi wa Zanzibar na hiyo 4.5% inayo daiwa pewa Zanzibar na ukalinganisha hali ya maendeleo ya Zanzibar,moja kwa moja unagundua Ufisadi wa kutisha kupitia ktk mradi huu wa CCM unaoitwa Muungano!
 
nguruvi 3 na Mchambuzi asanteni sana kwa darasa na naomba radhi kwa kutokuwepo kwa muda kidogo kazi zilibana kimtindo.

Binafsi mie niliwah kumwambia mtu JFC iliundwa kama njia ya kuwalamba wanzibar miguu, na ni ukweli usiopingika kwamba wakati wanaunda hili walihofia wazaznibar kujitoa kwenye muungano kwa kile wanachodai kwamba wanaonewa, lkn laabda turudi kule zaznnibar kwenyewe mbona jamani kati ya Unguja na Pemba kuna tofauti kubwa sana ya kiuchumi??

mmoja ni tajiri zaid kuliko mwingine kitu ambacho kimenifanya mie nione kama wanabaguana wenyewe tu wala sio siuo sisi watanganyika tunao wabagua.

sasa kwanza toka JFC iundwe haijawaha kufanyiwa marekebisho yenye tija na rais bado anahofia wazaznibar kana kwamba wao ndio watanzania pekee wenye nguvu hapa nchini.

ukija UDSM utajionea mwenyewe bodi ya mikopo inadai haiwez kukopesha wanafunzi wa uzamili na uzamivu lkn hapa udsm wapo wanaotokea zaznibar eti wanalipiwa na bodi af tena hawarudish sasa mtanganyika yeye hapewi kabisa hawa wazanzibar wanapewa na tunajua hayo, mbaya zaid huyu mtanganyika anatakiwa ajilipie ada ya uzamili/uzamivu huku bodi bado ina mfyeka alizokopeshwa. too sad kwakweli.

mie majuzi nilikuwa najadiliana na mtu, nilipata hasira kwa mambo niliyoyajua kuhusu zanzibar.
 
Last edited by a moderator:

Nguruvi3,

naona wewe ni mtaalamu wa kulalamika na kuuliza masuala lakin ukiulizwa wewe unaruka maili mia.

KWANINI SERIKALI YA JMTZ MPAKA LEO IMESHINDWA KUTEKELEZA SHARIA YA KUANZISHWA JFC IKIWAMO KUWAPA MAJUKUMU YAO KAMA WALIVYOPENDEKEZA KWA ZAIDI YA MIAKA KUMI? JE KUNA SIIRI GANI YA UTEKELEZAJI WA SHARIA HIYO?
 
Basically umekubaliana na hoja za Mchambuzi kuhusu kuanzishwa kwa BoT na JFC na majaukumu yao.
Hujajibu hoja bali kuleta hadithi.

Ahsante tumekusoma

Tatizo umezowea kutafuniwa wewe unameza tu.

Hapo unahitajika kuchimba sana ujue hiyo 4.5% imetoka wapi. unatakiwa kujua hisa kila mmoja (Znz na Tgk) katika kuanzishwa BOT nl vile vile hisa za kila mmoja katika bodi ya sarafu ya east Africa ambazo nazo baada ya kufa bodi hiyo share za nchi hizi mbili zilipelekwa BOT.

Sasa jifungie usome kwa nia ya kujua na sio kunung'unika.




 
Nimeamini tatizo la wazanzibari ni mzanzibari mwenyewe. Wa znz ni wanafiki sana. How hard is it for then to unite as one? Kudai self determination au referendum? Hawatofika kokote kama wenyewe kwa wenyewe wako hivi. ------------ kwa dola 200 na wakirudi Znz watapokelewa kwa vofijo na nderemo bafala ya disgust na itikafu. Wazanzibari ni wanafiki sana na njaa ya dola 200 ndio imezidi kuchangia
 

Mimi nilitaka kukujuza jambo moja kiduchu ambalo nadhani ulifahamu.

DENI LA NJE LA TZ KUFAIIKIA 30th APRIL 2014 LILIKUWA ZAIDI YA 38.6 TRIL (Yaani mara mbili ya makadirio ya bajeti ya
mwaka.

68.4% ya deni hilo limekopwa kwa ajili ya wizara zisizo za muungano yaani wizara miundombinu, uchukuzi, kilimo na afya.

Na deni hili limekopwa kwa jina la TZ na sio TGK.

Sasa kwa mtindo huu JFC inaweza fanya kazi hapo?

Pole sana



 
Shut up! tupo hapa kwa mjadala si kupeana website. Hizo website wangapi wana access na wana uwezo wa kuelewa. Kama huwezi kudadavua kaa kimya. Mchambuzi kakupa darsa la kutosha, kaonyesha usivyojua BoT wala JFC zinavyofanya kazi. Halafu ulikuwa mchumi wa nchi hii, no wonder sisi nbi masikini.
Hiuna hoja stay out of the debate, kazi yako kila siku ni kuchafua mijadala ya watu kwa trivial and stupid arguement.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…