Scotland kuamua iwapo itajitenga na Uingereza

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Kiongozi mkuu wa Scotland, Nicola Sturgeon, amesema kwamba kufuatia kura ya kujiondoa kwa muungano wa EU, sasa ni bayana kuwa hatma ya baadaye ya watu wa nchi yake wanajiona kuwa sehemu ya EU.
Kuna uwezekano mkubwa wa Scotland kupiga kura upya ya kujitenga na Uingereza.

Kiongozi mkuu wa Scotland, Nicola Sturgeon, amesema kwamba kufuatia kura ya kujiondoa kwa muungano wa EU, sasa ni bayana kuwa hatma ya baadaye ya watu wa nchi yake wanajiona kuwa sehemu ya EU.

Matamshi ya Sturgeon yanafuatia matokeo yaliyodhihirisha kuwa kila eneo wakilishi la Scotland lilipiga kura kusalia kwenye muungano wa Ulaya EU wala sio kujiondoa.

160624060636_nigel_farage_976x549_stefanrousseaupa.jpg


Kiongozi mkuu wa chama chama UK Independence, Nigel Farage, amemuomba Bwana Cameron kujiuzulu.
Waandishi habari wanasema kuwa, uwezekano wa kuwepo kwa kura nyingine ya maoni ya iwapo Scotland isalie kuwa sehemu ya Uingereza au la umeongezeka mara dufu.

Mwenyekiti wa chama cha Irish Republican, Sinn Fein, maarufu kama (Declan Kearney), amesema kwamba kura ya Uingereza imechochea kesi ya kuitisha kura ya maoni kuhusiana na umoja wa Ireland.

150508030544_nicola_sturgeon_624x351_getty.jpg


Kiongozi wa Scotland Nicola Sturgeon
Mbunge wa chama pinzani cha Labour, Keith Vaz, ameitisha wito wa kufanyika kwa kongamano la dharura kwa mataifa ya EU; huku akisema matokeo ya kura hiyo ni jambo la kutisha kwa Uingereza.

Hata kabla matokeo hajakuwa bayana, wafuasi wa chama cha Conservative wa mrengo uliotaka Uingereza iondoke, wamertia saini taarifa ya gazeti moja inayomtaka waziri mkuu David Cameron kusalia ili kurekebisha kura hiyo ya maoni.

Naye kiongozi mkuu wa chama chama UK Independence, Nigel Farage, amemuomba Bwana Cameron kujiuzulu.

======================
Nicola Sturgeon says the option of a second referendum on Scotland's independence "must be on the table" because the country faces the prospect of being taken out of the EU against its will.

She says a "significant and material change in circumstances" had occured since Scotland voted to stay in the United Kingdom in 2014.

But since the UK had voted to leave the EU, the Scottish government "will begin to prepare the legislation required" for a second referendum to take place.

England, Wales and Northern Ireland would remain friends of Scotland, she says.

We said clearly we do not want to leave the EU. I will do all it takes to ensure these aspirations are realised... An independence referendum is highly likely."
 
Sasa scotland na ireland zikijitenga mbona itakuwa majanga kwa UK.


Kabla hawaitenga iraq naona wao ndo wameanza kujitenga automatically
 
Back
Top Bottom