Scorpion anayetoboa watu Macho Buguruni, akamatwa

Nice work sa huyo bwege serikali si Ingemnyoosha tu
 
Wanajamvi tuache sheria ichukue mkondo wake na kuhamasisha wananchi wakatoe ushahidi ili apatikane na hatia huyo asiye na tofauti na gaidi
 

Acheni kumuogopa na kumpamba huyu sijui SCORPION wenu huko Buguruni na kusema kuwa hakamatiki. Sidhani kama huyo SCORPION wenu anafikia ' UKATILI ' wa Mtu mmoja ' TISHIO ' na ' HATARI ' anaitwa MBUZI YAKE KAMBA aliyekuwa akitikisa Kawe nzima na vitongoji vyake na kuna wakati kwa Uwoga tu Watu walikuwa wakipishana nae barabarani wanamsalimu na kumwambia tafadhali MBUZI YAKE KAMBA leo nina Simu nzuri na HELA mfukoni chukua tu. Kwa wale waishio KAWE nadhani watakuwa wanaelewa ninachokisema kwani huyu Jamaa hata Police tu wa Kawe walikuwa wanamwogopa ila tunashukuru kwa ujio wa Kamanda mpya SIRO na Mkuu mpya wa Kituo cha Kawe kwa kushirikiana na Wananchi kadhaa waliojitoa mhanga walishirikiana hadi wakafanikiwa kumkamata huyo MBUZI YAKE KAMBA na sasa yupo SEGADANSI nadhani Ukonga au Keko.

Hakuna MAASI ambayo huyu Jamaa MBUZI YAKE KAMBA wa Kawe hajayafanya na nakumbuka hata siku ile alipokamatwa tu sehemu mbalimbali za Kawe Wakazi walikuwa wakifanya Sherehe na kuna hata baadhi ya Police walisikika wakisema kuwa sasa WATAPUMUA. Nimeshamfuatilia huyo SCORPION wenu ila kwa aliyokuwa anawafanyia wana Buguruni miaka hii ya karibuni mwenzake MBUZI YAKE KAMBA wa huku Kawe aliyafanya miaka kumi ( 10 ) iliyopita.

Huyo SCORPION wala hashindikani kukamatika au kuchukuliwa hatua ila inaonyesha dhahiri kuwa nyie Wakazi wa Buguruni hamna Ushirikiano halafu yawezekana pia kuna Mtu au Mamlaka fulani inamlinda kwa minajili kuwa labda wanakula nae pale anapofanikisha ' tukio ' fulani lenye ' mtonyo ' wa maana. Nijuavyo Buguruni ndiko kumejaa ' Masela ' wa maana sasa inakuwaje mnlishindwa au mnashindwa kumdhibiti huyo SCORPION wenu?
 
Utadhani yeye hajui kwamba naye atakufa siku moja tu
 
Kwahiyo jamaa kawa kipofu kabisa? kama ndivyo kwanini na huyu anayejifanya mbabe asimwagiwe tu tindikali usoni then wakamuacha ili aone mateso yake.
 
Kisheria when attacked or provoked hutakiwi kuretaliate iyo ni kazi ya vyombo vya dola. Nadhan ndio maana watu wabugurun walisita kumchukulia hatua.

Pia kisheria ni polisi pekee yake mwenye uniform ndie anahusika kumtia nguvun mtuhumiwa.
 
Vituko kweli wanaumeeee....... eee
Mapanga...
 
Yapaswa tuangazie sheria za kunyonga huu ni ujinga mashtaka ya nini mjinga kama huyo ni wa Kunyonga au kuuawa Kwa namna yoyote .
Inauma sana .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…