Scolari Ambwagia Manyanga Ronaldinho

Scolari Ambwagia Manyanga Ronaldinho

Companero

Platinum Member
Joined
Jul 12, 2008
Posts
5,609
Reaction score
1,734
Baada ya kumpa Ronaldinho Gaucho nafasi nyingine ya kuuonyesha Ulimwengu kile alichokionyesha kwenye medhi dhidi ya Uingereza kwenye Kombe la Dunia la 2002, Kocha Philipe Scolari almaarufu kama Big Phil, amebwaga manyanga.

Kocha huyu ambaye anampenda Ronaldinho kuliko hata Gang Chomba anavyompenda mkongwe huyo ameamua kumwaga mchezaji huyo kwenye timu ya taifa baada ya kuonyesha kiwango cha chini kabisa dhidi ya Uingereza katika mchezo uliochezwa hivi karibuni.

Kama hadi Scolari wa Selecao uvumilivu umemshinda basi hakika huu ndio wakati wa mchezaji huyo aliyekwisha kutundika daluga kwa heshima na taadhima na kushuhudia Kombe la Dunia 2014 kwenye runinga au jukwaa la uwanja wa Maracana!

Rejea: Kaka back in Brazil squad but Ronaldinho left out - ESPN FC
 
Companero huo mwaka wa kombe la dunia umesema 2012 au 2002?!
 
Last edited by a moderator:
Ni ukweli unaoumiza kwa Gaucho,natamani angesoma ulichoandika.
 
Kombe la dunia ni kesho kwani wewe?.... mpaka mwakani anaweza kujitenegeneza na akaitwa tena kama ambavyo kaka amekuwa anaachwa then anarudi tena...
 
"Mwili wangu unashindwa kufanya vile akili yangu inavyonituma kufanya" by Ronaldo Dilima.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Gang Chomba hoi kashindwa kuendeleza porojo zake za kumsifia Ronaldinho,sijui safari hii malaika wameasi au wameamua kujiandaa kumuangalia lionel Messi next week akiwafurumusha AC Milano!!
 
Gang Chomba hoi kashindwa kuendeleza porojo zake za kumsifia Ronaldinho,sijui safari hii malaika wameasi au wameamua kujiandaa kumuangalia lionel Messi next week akiwafurumusha AC Milano!!

Dinho Magic...
Waja wa mola povu linawatoka kwa kumkashifu mbarikiwa...
 
"Mwili wangu unashindwa kufanya vile akili yangu inavyonituma kufanya" by Ronaldo Dilima.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

Kwani huyo ndiyo Ronaldhino! bado anayo nafasi
 
Back
Top Bottom