[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading, width: 100%"]Dk Mafunda: Ugunduzi wa kisayansi utainua maendeleo ya jamii [/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"]
Send to a friend [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"] Tuesday, 26 June 2012 09:40 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] 0digg
Ibrahim Yamola
UGUNDUZI wa kisayansi na kiteknolojia ni muhimu katika dunia ya sasa ambapo utandawazi unaelezwa kuchukua nafasi kubwa katika maendeleo ya nchi mbalimbali duniani.
Kwa nchi kama Tanzania ambayo bado imo katika kundi la nchi zinazoitwa za dunia ya tatu, haina jinsi ya kuepuka kujihusisha zaidi na michakato ya ugunduzi wa kisayansi na hata matumizi yake kama inataka kupiga hatua zaidi kimaendeleo.
Hata hivyo, inasikitisha kuona kuwa bado kumekuwapo na kasi ndogo ya Watanzania kujihusisha na masuala ya ugunduzi na ubunifu hasa katika nyanja za sayansi na teknolojia ambazo kwa sasa zimeshika kani duniani kote.
Lakini hali hii haijawazuia wadau wa sayansi na teknolojia nchini, ikiwamo Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), kuendelea na mipango na mikakati ya kuimarisha maendeleo ya sayansi.
Kwa mfano, Kaimu Mkurungezi wa Kituo cha Kuendeleza na Kuhawilisha Teknolojia (CDTT) katika tume hiyo, Dk Dugushilu Mafunda anasema kwa kutambua umuhimu wa teknolojia, tume imekuwa na utaratibu wa kuwatunuku wagunduzi katika kada mbalimbali za sayansi na teknolojia.
Kwa mujibu wa Dk Mafunda, utaratibu huo ulioanza mwaka 1981ikiwa ni sehemu ya kuwatambua na kuwatunuku wagunduzi na wabunifu hasa wale wadogo, unalenga kutambua mchango wa wagunduzi hao katika jamii zao na Taifa kwa jumla.
"Kufanya hivyo ilikuwa ni njia stahiki kwa wagunduzi kuamsha morali na watu wengi kujiingiza katika ugunduzi kwa manufaa ya jamii inayowazunguka" anasema na kuongeza:
"Ni wajibu wetu kuhakikisha tunatambua mchango wa wananchi wanaogundua vitu mbalimbali, hususani vifaa vya kisayansi kwa kuwatunuku na kuwaendeleza kwa manufaa ya Taifa letu.''
Anaeleza kuwa kwa sasa tume imekuwa ikitoa tuzo kadhaa ikiwamo Tuzo ya Sayansi Shuleni (SSA) inayolenga kujenga misingi ya sayansi, teknolojia na ubunifu katika ngazi ya shule za sekondari na vyuo.
"Tuzo hii hutolewa kwa shule itakayokuwa imeonyesha juhudi katika matumizi ya sayansi, teknolojia na ubunifu hasa katika kufundishia, kutengeneza zana za kufundishia au katika majaribio ya kisayansi,''anabainisha.
Tuzo nyingine ni ile ya Utafiti wa Hifadhi na Uendelezaji wa Mazingira (NAEM) ambayo hutolewa kwa wanasayansi na wanateknolojia wanaotoa mchango katika kubuni teknolojia zinazopunguza uharibifu wa mazingira kama vile uchafuzi wa hewa, taka za sumu, uharibifu wa maliasili na wanyama pori.
Nyingine ni tuzo ya Taifa ya Mafanikio katika Sayansi na Teknolojia (TASTA). Hii hutolewa kwa Watanzania waliofanya ugunduzi ambao unaweza kuleta manufaa katika kuboresha maisha na uchumi nchini au kuendeleza elimu na taaluma za fani mbalimbali za sayansi, teknolojia na ubunifu.
Akieleza sifa ambazo mgunduzi hutakiwa kuwa nazo ili aweze kutunukiwa tuzo, Dk Mafunda anataja kuwa ni pamoja na mgunduzi kuonyesha uasili wa alichokigundua, kuwapo kwa tathimini ya kitaalamu, uwezo wa manufaa ya ubunifu wake kwa jamii na Taifa, upya wa ugunduzi wake, matumizi ya malighafi zinazopatikana nchini na uendelevu wa ugunduzi.
"Mara baada ya mtu kufanya ugunduzi anatakiwa atume maombi kwetu, na sisi tutawashirikisha wataalamu wetu kuupitia ugunduzi huo na kuona kama kweli unakidhi haja na hatimaye tunaanza kumtambua," anaeleza.
Anaongeza: "Baada ya kuona watu wengi wanagundua vitu mbalimbali bila ya kuviendeleza, COSTECH ilianza utaratibu wa kuwatunuku vifaa vinavyoendana na ugunduzi wao ili waweze kujiendeleza kwa manufaa ya jamii zao.''
Akitoa mfano wa matatizo yaliyoko katika sekta ndogo ya nishati umeme, anasema wamekuwa wakipokea gunduzi za wananchi wanaozalisha umeme hasa katika maeneo ya vijjini ambayo hayafikiwi na umeme wa gridi ya Taifa.
"Endapo tutawapa vitendea kazi hawa wagunduzi, nina uhakika watasaidia kuondokana na utegemezi wa umeme wa gridi ya Taifa kwa baadhi ya maeneo.
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Najiuliza, tuzo tu zinahitajika? Ni vipi tunaweza kuitumia hii sayansi na teknolojia kutatua matatizo yanayotukabili? Naona hapo hamna popote yalipoorodheshwa mambo ambayo yanaweza kutatuliwa.