huu ni ujumbe tosha kwa wote wenye biashara. habari ya kufungua biashara unawaachia wafanyakazi bila kuwafuatilia kwa siri kujua wanadili vipi na wateja wako huchelewi kufunga biashara kwani wafanyakazi wengi hawajui uwepo wa wateja ndio unasababisha wao wapate mshahara yaani hawajui kabisa kama mteja ni mfalme. kwa habari hii tu kufika hapa jf mwenye famasi kashakosa wateja wengi sana kwani kupata mteja 1 ni kazi ngumu sana lakini kupoteza wateja 100 ni sekunde tu. hao wakina dada hawajui ni kiasi gani wameharibu biashara ya mmiliki wa hiyo famasi. ningekuwa mimi ndio mmiliki ningefanya uchunguzi wa haraka haraka nikibaini kuwa kuna chembe ya ukweli basi ningesitisha mikataba yao ya kazi na kuajiri wafanyakazi wengine ili kurudisha imani ya wateja.