Sauti ya waliosahaulika Tanzania

Sauti ya waliosahaulika Tanzania

fakhbros

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2013
Posts
388
Reaction score
666
NO REFORM, NO ELECTION: SAUTI YA WALIOSAHAULIKA TANZANIA

Na Kamgisha Abeid:

Wakati taifa linaelekea kwenye uchaguzi mkuu mwingine, sauti ya wanyonge inazidi kufunikwa na makelele ya wanasiasa. Lakini sasa, kutoka kwenye vijiwe vya kahawa, masoko ya wakulima, shule za kata, viwanda vya mishahara duni na vichochoro vya miji maskini, ujumbe mmoja unaenea kama moto wa nyika:
"No Reform, No Election."

Kauli hii siyo ya uvunjifu wa sheria, bali ni kilio cha mamilioni ya Watanzania wanaohisi kusahaulika na kunyonywa ndani ya mfumo ambao hauwajali. Bila mabadiliko ya kweli katika mfumo wa kisiasa, kiuchumi, na kijamii kura zao ni sawa na kutia sahihi kwenye mateso yao wenyewe.

Wakulima:

Mashujaa Wasio na Sauti
Wakulima wa Tanzania ndio uti wa mgongo wa taifa hili, lakini wanavunwa zaidi kuliko wanavyovuna. Bei ya mazao inapangwa na madalali, pembejeo ni ghali mkulima anakopeshwa mbolea badala yakugawiwa bure, barabara nyingi vijijini ni mbovu, na soko la mazao yao lenyeuhakika halipo. Kura zao kila chaguzi hazijabadilisha maisha yao.hivyo wakulima wanasema sasa,
"Tuna haki ya kusema, kama hatuoni mageuzi ya kweli, hatuna sababu ya kupiga kura."

Wafanyakazi:
Nguzo ya Uchumi Isiyolindwa
Katika viwanda na ofisi, wafanyakazi wanapambana kila siku kwa mishahara duni isiyotosha hata chakula cha mwezi. Hakuna bima ya afya, usalama kazini ni ndoto, na mikataba ya ajira imejaa mashimo ya manyanyaso. Bila mabadiliko katika sheria za kazi, haki ya wafanyakazi ni porojo tu. Kwao,
"No Reform, No Election" ni mwito wa heshima na utu kazini..

Wafugaji:
Wanalindwa na Mifugo:
Wafugaji wamekuwa wakihamishwa kutoka ardhi yao kwa nguvu, bila fidia wala maelezo. Migogoro ya ardhi imegeuka kuwa janga la taifa. Serikali inabaki kimya huku wafugaji wakihangaika kuhifadhi maisha yao na mifugo yao. Wao pia wanauliza, “Je, tuna nafasi katika mfumo huu wa uchaguzi usioleta amani wala usawa?” Jibu wanasema No Reform no Election"

Wanafunzi:
Wasomi Wanaokua kwenye Ukosefu
Wanafunzi wengi wanakaa kwenye madarasa ambayo yalijengwa nyakati za kupambania Uhuru wa Africa' Wasomi wa Secondary hawana ujira katika Elimu yao wanatoka majumbani wakiwa na njaa na wanakuja Mashuleni kukutana na walimu walio dhurumiwa mishahara yao kwa njia ya mikopo ya kilaghai kupitia mabank wakala, Mikopo ya Elimu ya Juu, Mikopo ya kuanzia maisha baada ya ajira, Michango ya mifuko ya hifadhi ya jamii, Michango hewa ya CWT, vyote hivi walimu wanasema kimoyoni No reform No Election.. Wanafunzi wa vyuo vikuu kukosa mikopo stahiki, pesa za kujikimu kutolewa kwa utashi wa wasimamizi bila kujali hali halisi ya uhitaji wa pesa hizo kwa wakati nao wanasema No Reform No Election,

MADEREVA BAJAJI NA BODABODA:
Unyanyasaji wa vyombo vya ulinzi na usalama ikiwa ni pamoja nakuporwa vyombo vyao kwa nguvu nakuliona jeshi la polisi kama Jeshi la Unyanganyi nao wanasema no Reform no Election"

WAHUDUMU WA BAR NA MAMA NTILIE"
Haya ni makundi ambayo Serikali imekuwa haiyathamini ni makundi ambayo huonekana ni dharili ila katika makundi haya ndiko ambako hutokea watawala na huko ndiko ambako kuna pesa nyingi za kodi ambazo huwalipa watawala lakini Serikali haiwapi kipaumbele kama inavyoweza kuwapa wabunge na wateule wengine katika huduma za msingi kama Bima za Afya nao wanaona kwakuwa miaka yote wamekuwa wakishiriki kuchagua na uchaguzi kuwaletea wateule wa Ikulu basi wanasema No reform no Election ni njia sahihi kuwaondoa watawala wasio tokana na wao'

WAVUVI:
Kundi la wavuvi ni kundi dogo lakini nalo ni kama makundi mengine wanasema bila uchaguzi ulio huru na haki basi thamani yao ndani ya hili Taifa haitakuwepo wanajaribu kuangalia namna Serikali inavyo ruhusu samaki kutoka mataifa ya mbali nakuja kuharibu soko la Samaki nchini basi wanaona bora waunge mkono No reform no Election

MTAZAMO WA KISIASA:
CCM ni chama ambacho waasisi wake wengi 1977 walikuwa ni wale ambao walishiriki katika harakati za kulikomboa Taifa maono yao ilikuwa ni Kujenga Taifa moja na wakawa na kauli mbiu yakwamba Uhuru na Umoja"
Uhuru ulio udhamiliwa ni Uhuru wa kujitawala' Kujiratibu' Kujikomboa' Kujieleza' Kijilinda' na kuweza kwenda popote pasina kubughudhiwa sababu wewe ni mwana wa nchi ilio Huru' CCM baada ya Miaka 48 imepoteza vyote vilivyo anzishwa na waasosi wake- hatimae kimekuwa ni chama cha Unyonyaji, Ubepari, Utekaji, Ufisadi, Ukiritimba, na hata kuwa chama cha Mauaji kwa wanao kosoa mienendo ya viongozi ndani ya Taifa'

NO REFORM NO ELECTION:
Hii ni kauli mbiu ilio asisiwa na viongozi ndani ya Chadema kauli hii inaleta maana kwa wananchi kutokana na matukio mbalimbali juu ya Chaguzi nyingi zilizofanyika nchini' Chaguzi zimekuwa zikinajisiwa na viongozi wa tume' hivyo No reform no Election inaweza kuwa njia bora itakayo leta usawa kati ya watu wanao omba ajira ya Uongozi kupitia Sanduku la Kura"
 
Attachments

  • Beige And Brown Motivational Book Cover_20250608_075751_0000.png
    Beige And Brown Motivational Book Cover_20250608_075751_0000.png
    1.2 MB · Views: 13

gazeti refu sana, umekula?
 
Asante kwa Uzalendo tupia kwenye tone tone
 
Back
Top Bottom