Saudi Arabia, Iran katika meza ya mazungumzo

Saudi Arabia, Iran katika meza ya mazungumzo

Yussufhaji

Member
Joined
Sep 9, 2018
Posts
35
Reaction score
28
SAUDI ARABIA – IRAN KATIKA MEZA YA MAZUNGUMZO

Wagombanao ndio wapatanao, hivi karibuni kumekuwa na mbio za sakafuni zinazofanywa na Waziri mkuu wa Pakistan Imran Khan ambapo matarajio ya ukiongoni wa mbio hizo ni kuyaleta pamoja mataifa mawili ya mashariki ya kati yenye maingiliano makubwa ya kijamii,kiuchumi na kiimani Saudi Arabia na Iran katika kutatua na kusuluhisha mgogoro wa muda mrefu baina yao.

Historia inasemaje kuhusu uhusiano wa mataifa haya?

Historia ya uhusiano wa Saudi Arabia na Iran unaanzia katika dola ya utawala wa Ottoman na kuanzia miaka ya 1920s Saudi Arabia na Iran zimekuwa na migogoro mara kadhaa na kuitatua kwa njia ya mazungumzo, mwaka 1929 Saudi chini ya uongozi wa mfalme Abdoul Aziz na Iran chini ya uongozi wa Reza Shah waliekeana mkataba wa urafiki baina yao ulioweka misingi ya uhusiano kibiashara, siasa na diplomasia baina ya Tehran na Riyadh, ambapo mataifa haya yalishuhudia kuwa na uhusiano imara mpaka mwaka 1943 kuanza kusuasua baada ya kiongozi wa Iran Reza Khan kupinduliwa na mwanae Mohammed Reza Pahlavi.

Baadae tena mwaka 1965 Saudi Arabia na Iran waliekeana mkataba wa kumaliza mizozo baina yao baada ya mazungumzo ya muda mrefu, ambapo matokeo yake ni kuibika kwa uhusiano mzuri na mashirikiano mazuri zaidi baina yao, huku kiongozi wa Iran, Shah akinukuliwa:-

“Nimekuwa nikisafiri mara kadhaa kwenda Saudi Arabia, nchi ambayo uadilifu na uhuru ni takatifu kwa Waislamu wote. Kama Mwislamu mwaminifu na Mtetezi wa Imani, natumai kwamba Saudi Arabia itabaki kuwa mlezi wa maeneo haya matakatifu, Makka na Madina”

Nini kiini cha mzozo uliopo na mada zinazo tarajiwa katika mazungumzo hayo?

Chimbuko kuu la mgogoro uliopo sasa baina ya mataifa mawili haya ya ghuba ni mapinduzi ya Iran ya mwaka 1979 ambayo yalimuondoa madarakani Pahlavi ambae alipendelea kuiona Iran inayofanan na mataifa ya Magharibi, Mpainduzi hayo yaliochochewa na Ayatollah Khamenei huku hoja kuu ikiwa ni kuundwa kwa dola la kiislam lenye kufuata sharia na kanuni za kishia, kuondokana na kile kilichoitwa ukoloni wa kiutamaduni na kufeli kwa sera za kiuchumi za Pahlavi kutibu machungu ya kiuchumi yaliokuwepo.

Mapinduzi haya yaligeuka na kuwa tishio kwa Saudi Arabia na kuzidisha vita baridi ya ufahari wa mashariki ya kati, kwa kadri Serikali ya Kisslamu ya Iran ilivyokuwa ikibadilisha sharia na sera zake mbali mbali, tishio zaidi kwa Saudi Arabia. Adhma ya Khamenei ya kueneza ushia na kutanua mapinduzi ya 1979 na ushawishi wa Iran Mashariki ya kati pia ni miongoni mwa chagizo za mgogoro uliopo, kwa kumnukuu Tali Rachel Grumet wa chuo kikuu cha Denver, katika makala yake alioipa kichwa cha habari “VITA MPYA BARIDI YA MASHARIKI YA KATI; UHASAMA WA SAUDIA NA IRAN” anaandika kuhusu Iran baada ya Mapinduzi ya 1979 kuwa:-

“Ingawa ilihubiri umoja wa Waislam, Iran "iliunga mkono vikundi vya Afghanistan, Bahrain, Iraq, Lebanon, Pakistan,ambavyo vilikuwa na ajenda maalum za Shia.”

Anaendelea kuandika:-

"Khominei aliona utawala wa Saudi kama ugani wa uingizaji wa Marekani na alilenga kupindua kile alichokiangalia kuwa udikteta mbaya na ulio na udanganyifu, kwa kutumia njia sawa ambazo alitumia kwa ufanisi kuipindua tawala ya Shah ya Iran"

Hivyo tangia kutokea kwa mapinduzi ya Iran uhusiano baina ya mafahari hawa wawili wa mashriki ya kati umekuwa wa mashaka na wa kutoa aminiana, huku mara kwa mara kila mmoja akimtupia mzigo wa lawama wa kumdhoofisha mwenziwe, na huku Usunni na Ushia ukitumika kuwa propaganda kuu ya kujipatia wafuasi.

Mada mbali mbali zitategemewa katika meza ya mazungumzo biana ya Riyadh na Tehran kama masuala ya Siasa, Nyukilia, Biashara na Jamii ikiwemo suala la Hijja pia migogoro ya Palestina , Syria, Iraq, Yemen na kuondoa tofauti zao mbali mbali.

Sasa ni wakati muafaka kwa mazungumzo baina ya mataifa haya?

Mataifa yote mawili, Saudi Arabia na Iran yameonesha utayari wake wa kukaa katika meza ya majadiliano, huku Waziri Mkuu wa Pakistan akinukuliwa kuwa Mwanamfalme Mohammad bin Salman alimuambia kuwa Saudi Arabia ipo tayari kwa mazungumzo, Mwezi Oktoba mwaka huu Waziri wa mambo ya nje wa Iran nae amesema Iran ipo tayari kwa mazungumzo aidha kuwepo kwa mpatanishi au bila ya uwepo wa mpatanishi.

Kujitolea kwa Pakistan kuwa mpatanishi wa mzozo huo panajenga hoja kuwa sasa ni wakati muafaka wa mazungumzo, ukimurika uhusiano mzuri ilio nao Pakistani kwa mataifa yote mawili na pia umiliki wake wa Silaha za Nyuklia kunaipa Pakistani heshima ya kipekee kusuluhisha mgogoro huu kwa wakati huu.

Kukua kiuchumi, kiteknolojia na kijeshi kwa Iran, kutengwa kwa Iran na mataifa kadhaa ya ghuba, kuengezeka kwa ushawishi wa mataifa kadhaa ya nje kama Urusi na Marekani ya mashariki ya kati katika masuala mbali mbali ya mashariki ya kati, kudorora kwa uchumi wa dunia, kulinda amani na usalama wa mashariki ya kati na mapambano dhidi ya makundi mbali mbali ya ugaidi mashariki ya kati na ulimwengu kunaibua hoja muhimu ya upekee wa kufanyika kwa mazungumzo wakati huu baina ya mataifa haya hasimu.

Nani mnufaika iwapo mazungumzo hayo yatafanyika na kufanikiwa?

Bila ya shaka wanufaika nambari moja ni raia wa Saudi Arabia na Iran ukizingatia matokeo ya mazungumzo hayo yatawapa fursa raia wa mataifa hayo kujongeana zaidi kijamii, kiuchumi na kisiasa pamoja na raia wa mashariki ya kati na ulimwengu, haswa ulimwengu wa kiislamu kwani nguvu za pamoja zitaengezeka na kuzipa nguvu taasisi kadhaa za kimataifa kama Umoja wa nchi za kiislamu OIC na Umoja wa nchi za Ghuba GCC.

Biashara itaengezeka na kukua baina ya mataifa hayo, kuengezeka kwa mahujaji wa Iran Saudi Arabia na nchini Iran katika mji wa Karbala.

Vile vile mazungumzo haya yatanufaisha na kufungua ukurasa mpya wa uhusiano baina ya mataifa ya magharibi kama Uengereza, Ufaransa na Ujerumani zikiongozwa na Marekani na taifa la Iran.

Bila ya kusahau mazungumzo ya mafahari hawa wawili wa Mashariki ya Kati yanaweza kufungua mazungumzo mengine ndani ya mashariki ya kati kama mazungumzo baina ya Qatar na nchi za Ghuba na Iran nan chi za Ghuba.

Iwapo mazungumzo hayo yatafanyika na kufanikiwa kufikia mkataba utakao ridhiwa na kutekelezwa na pande zote mbili itakuwa ni furaha kwa dunia na ni jambo la kupigiwa mfano na kuigwa huku wanufaika wakuu wakiwa ni raia wa nchi hizo.

Wakati nikiwatakia kheri mataifa haya mawili kufanikiwa katika mazungumzo yao, nami naweka chini kalamu yangu kuhusu mazungumzo hayo huku nikichukua jembe kwenda kulima, huku nikifuata msemo wa wahenga unao sema ndugu wakigombana chukua jembe ukalime!

Imeandaliwa na;
Yussuf Haji Khatib,
Email:hajjyussuf2@gmail.com
Simu:+255777158131
 
Tatizo lipo kwenye ushawishi ndani ya mashariki ya kati, Nani atakubali ushawishi wa mwenzake ushamiri katika himaya Yake au Kwa wafuasi wake!!

Je saud Arabia atakubali ushia upenyezwe kwenye himaya zake au Iran atakubali usuni ushamiri katika himaya na ngome zake nje na ndani ya Iran??

Hapo ndipo kasheshe ilipo kama watapatana na kufuta tofauti zao.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo lipo kwenye ushawishi ndani ya mashariki ya kati, Nani atakubali ushawishi wa mwenzake ushamiri katika himaya Yake au Kwa wafuasi wake!!

Je saud Arabia atakubali ushia upenyezwe kwenye himaya zake au Iran atakubali usuni ushamiri katika himaya na ngome zake nje na ndani ya Iran??

Hapo ndipo kasheshe ilipo kama watapatana na kufuta tofauti zao.



Sent using Jamii Forums mobile app
Kama wameruhusu dini nyenginezo kuwepo katka nchi zao. Hilo pia linawezekana. Mazungumzo ni win win situation au lose win situation. Kama USSR na USA iliwezekana. Hata hao itawezekana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwenye kufahamu,


kwanini Pakistan akumbani na vizingiti vya kumiliki nyuklia ???

Tukiangalia Kwa Jirani Yake Iran au Korea ya kaskasini ni tofauti kidogo,

Mwenye kujua anijuze jaman wakuu!!!

Sent using Jamii Forums mobile app

Jibu Ni Rahisi Sana Mkuu

Tangu Mapinduzi ya IRAN Mwaka 1979, utawala wa Ayatollah uliapa Kuingamiza ISRAEL na USA, kwahiyo kukabiliana na Hilo suala imewabidi ISRAEL na USABwapambane kuhakikisha IRAN hamiliki silaha za maangamizi kama Nuclear, Ndo maana Utaona ISRAEL ameendesha Misheni za Kuua wana sayansi wa iran wanaojihusisha na Nuclear na Pia Israel waliiba documents zinazohusu masuala ya Nuclear hapo Iran

Kwa Upande Wa Pakistan Israel na Marekani hawana Inshu nae maana Pakistan hajatishia kuingamiza ISRAEL wala USA, yeye Pakistan Adui Yake ni INDIA.
 
Ukristo,budhism zote zipo practiced ktk hizo nchi. Kama unaamini hizo dini hazipo practiced ni propaganda

Sent using Jamii Forums mobile app
Una maana kuna kanisa kabisa mjengo ? Taja miji makanisa yapo acha story wao kukataza dini nyingine ni sahihi wameshajibainisha wanafuata sharia.

Hivyo kuruhusdu " makafir" itakuwa kujochanganya sana. Wako wazi kabisa ni nchi za kiislam.
 
Una maana kuna kanisa kabisa mjengo ? Taja miji makanisa yapo acha story wao kukataza dini nyingine ni sahihi wameshajibainisha wanafuata sharia.

Hivyo kuruhusdu " makafir" itakuwa kujochanganya sana. Wako wazi kabisa ni nchi za kiislam.
Ina maana furaha yko uone mjengo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo nyuma hizi nchi zilikuwa zikiptn vizuri tu. Pmj na kuwepo na ushia au usunni. Hivyo ushia na usunni sio hoja ya kukatiza mazungumzo. Hapo ni maslahi ya kisiasa na uchumi katika kanda tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom