Kwame Nkrumah:
Maana ya Visionary ni: A person with unusual powers of foresight; Je unaweza kumjadili Lowassa katika muktadha husika kwa kutumia maana ya dhana hii?
What is so unusual kuhusu alichozungumza Lowassa? Nadhani hata Lowassa mwenyewe sana sana atakubali kuchukua credit kwa kulizungumzia akiwa kiongozi wa CCM, lakini atakwepa kwa kila njia kuitwa A Visionary kwa suala ambalo hata yeye anajua fika kwamba ameligundua kupitia tafiti na ripoti mbalimbali;
Suala hili limekuwa likizungumzwa kwa miaka mingi sana, kwa mfano rejea tafiti za REPOA, ESRF, na pia kutoka taasisi nyingine nyingi za nje ya nchi zinazojishughulisha na masuala ya Sera za Kutokomeza Umaskini Afrika; Suala hili limejadiliwa kwa kina sana pamoja na athari zake kwa miaka mingi, kabla hata Kikwete hajawa Rais wa Tanzania;
Kwame Nkrumah, kama tunampenda Lowassa kwa uongozi wake,jambo ambalo ni sahihi kabisa, tujaribu kumuunga mkono kwa hoja nzito, sio hizi nyepesi nyepesi; Lowassa anastahili sifa kubwa kwa kuwa Kiongozi wa CCM kulisemea hilo wakati wengine wakiwa wamelala, lakini tusinogewe na kuanza utamaduni wa kumjengea sifa zinazombatiza mambo mengine ambayo hata yeye anajua bado hastahili; Itafikia wakati tutasema Lowassa ni Visionary, lakini wakati huo sio sasa;