TandaleOne
JF-Expert Member
- Sep 4, 2010
- 1,644
- 709
Siku zote huwezi kutoa SOLUTION bila kwa kuainisha TATIZO. Wapinzani wamesifia mazuri yaliyofanywa na ndio mana kila MTU amekuwa akimsifia na kusifia serekali iliyokuwa chini ya Mwl. NYERERE.Tufikiri upya na kwa makini zaidi.
Nadhani ni wakati mwafaka sasa tukae na kujiuliza kama mtu/chama kinaweza kuwa madarakani kwa miaka mingi na mtu ukasema hakijafanya chochote.Kujifunza nini hasa maana ya takwimu na kuna maana gani mtu anaposema uchumi umekua lakini hali ya maisha ikaonekana bado ngumu.Kujifunza tofauti ya kuongezeka kwa pato la taifa na maendeleo.
Ni wakati mwafaka sasa kufahamu kwamba kazi ya chama cha siasa si tu kuponda bali hata kusifia yale yaliyofanyika.Kama raisi wa nchi anasimama na kusema yeye ndo aliamu kuanzisha chuo kikuu kama sehemu ya ilani ya chama halafu mtu mwingine akaja akasema rais anaongopa inabidi huyu mtu atuambie rais anaongopa kivipi na kwa nini kama alijua ukweli siku zote hakuusema mpaka wakati huu.Kwani harakati zina likizo???(napata mashaka).!
Kama unaweza kukaa ndani ya nyumba kwa miaka lukuki huku ukiona ni nyumba mbovu yatupasa utushawishi uliwezaje kufanya hivyo.(mashaka makubwa)
Ni wakati wa kufikiri na kuamua.:violin:
Siku zote huwezi kutoa SOLUTION bila kwa kuainisha TATIZO. Wapinzani wamesifia mazuri yaliyofanywa na ndio mana kila MTU amekuwa akimsifia na kusifia serekali iliyokuwa chini ya Mwl. NYERERE.
Yanayosemwa sasa ni ubovu wa Serekali hasa hii ya AWAMU YA NNE. Wewe fikiria, very simple: Mwaka 2005 Sukari ilikuwa Sh.600, leo Sukari ni Sh. 2000. Mshahara wa kima cha chini umeongezeka kutoka Sh.60,000 Kufikia around Tzs.135,000. Kama unajua Hesabu embu piga Ongezeko la Kipato na Lile la gharama za maisha!
Sasa hapo wewe unataka mtu asifie NINI?????
Kwenye UPUUZI ni Lazima tuseme! Wewe ukipewe T-shirt ya CCM leo utasifia kuwa umepewa MAISHA BORA?
Hakuna MUDA WA KUFIKIRIA! HUU NI WAKATI WA KUFANYA MAAMUZI!
Tumeshafikiria kwa miaka Mingi sana!
Ummetoa jibu mwafaka kwa muda mwafaka kabisa.Hakuna MUDA WA KUFIKIRIA! HUU NI WAKATI WA KUFANYA MAAMUZI!
Tumeshafikiria kwa miaka Mingi sana!
Tuma ujumbe huu kwa watu 50 thanksKwinini😛osts zako zinaelezea mengi kuhusu uwezo wako wa kufikri na matumizi ya social media.:confused2:
Lakini serikali hii ina ubovu peke yake??????:confused2:
Usilolijua ni sawa na usiku wa giza wewe unadhani kuwa mtumwa na kukesha JF kuwatumikia makafiri ndiyo una akili nzuri, na thread zako zote zitakuwa zinajaa ujumbe huu pekee.Poor thinking capacity:confused2:
Yatakuwepo Mazuri. Lakini jambo kuu hapa ni maisha ya Watanzania 45m. Serekali inaonekana imefanya mazuri kwa wachache kama marafiki na wanafamilia wa viongozi wa juu wa CCM. Uongozi wa nchi umeshindwa kuleta maendeleo kwa wanachi wa kawaida. Ukiangalia Miaka 50 baada ya uhuru bado sisi ni masikini wa kutupwa wakati nchi imekuwa na utulivu ndio mana wanatokea wapinzani na kusema kuwa CCM imeshindwa nchi na iwaachie wengine.
Ni ukweli usiopingika kuwa Tanzania haitaweza kuona maendeleo yanayotakiwa kuondoa umasikini bila ya kuwa na mfumo mpya wa uendeshaji. Tunahitaji safu mpya za viongozi wenye chachu ya maendeleo ya kiuchumi na kuwaweka pembeni wale walio viongozi wa Kisiasa zaidi kama hawa CCM. Kama wanasema wamejenga shule za kata, kwa nini watoto wao hawasomi huko? kwa nini viongozi wanaenda nje ya nchi kwa matibabu?
Au labda wewe unajua mafanikio gani ambayo wapinzani inabidi wayasifu?
Usijiangalie wewe mwenyewe, waangalie watanzania wengine huko vijijini, bila shaka unao ndugu zako walio vijijini!
Ukijiangalia mwenyewe basi utaona CCM imekufanyia makubwa, hasa kama upo kwenye system.
Mimi sina shida kabisa, hata CCM wakiwa madarakani maisha yangu yako sawa na yataendelea kuwa mazuri...ila kwa manufaa ya nchi, CCM wameshindwa kazi!
Angalia nchi nyingi zimefanya mabadiliko, Australia, Sweden, Japan, UK ... hawa bado ni nchi zilizoendelea ila watu wamegundua hakuna mabadiliko bila ya kuweka sura na mawazo mapya!
Nani anayehangaika mimi au wewe kazi yangu ni ku-copy N' paste nimeseti automatic special kwa post zako tu chukua nyingine hiyo...Utahangaika sana mwaka huu.Na yule aliyeanguka bafuni?:confused2:
Serekali inaleta maendeleo.And let's face the facts brother,serikali inaleta maendeleo au inatengeneza miundombinu kuyaendea maendeleo?:confused2:
TandaleOne haathiriki na maisha ya kati kuelekea chini ya waliowengi.
TandaleOne yupo kwenye payroll ya waliomtuma hivyo haoni hatari kuongea chochote baada ya akaunti yake kutuna.
I dare to say kwamba for 5yrs hatukuwa na serikali bali watawala walioungana na wahujumu kuifilisi nchi
And for 5 years the so called POLITICIANS LET THAT HAPPEN????UNAFIKI HUU,MBONA POSHO ZA BUNGENI HWAKUZIGOMEA????CHAGUA CCM,HAPA USANII MWINGI.WALE WALE.:confused2:
Bora hao waliochukua Posho na kwenda kuwasaidia wananchi wao! Hakukuwa na sababu ya wao kuziachia Posho ambazo zingeliwa na wachache, lakini kuna udhibitisho kuwa walitumia kipato chao kutumikia Wananchi.
TUSUBIRI 31 October tuone!