Sasa tuanzishe 'sleeping allowance' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sasa tuanzishe 'sleeping allowance'

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by sulphadoxine, Jul 6, 2011.

 1. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #1
  Jul 6, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Wakati mkijilisha pepo na matanuzi wenzenu wanatanuliwa na dhiki.je mnawawakilisha wao au matumbo yenu?.Kwani tulipowachagua tuliwaambia mwende kusimama?Mbona wafanyakazi wengine tena wa haja,hawalipwi hiyo mishiko ya makalio?Mbona wakina steve Wahasira wanauchapa usingizi kwenye mjengo hamuwapi mshiko wa usingizi?.Kesho mtakuja na usanii mwingine wa kutaka posho za kulala au sleeping allowances.Na hapo bado posho za kupayuka au shouting allowances.
   
 2. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #2
  Jul 6, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Pia nashauri zilipwe posho za kumshangilia madam microphone na kuogopa kutoa hoja za mashiko au cheering and fearing allowances.
   
 3. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #3
  Jul 6, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Wenzetu pale kwa nyayo wanalipa kodi wakati nyinyi mnaendela kucheza makidamakinda! Wenzenu hawana vyanzo vya umeme lakini bado hawana mgawo wakati nyinyi mnavyo mmevikali na kukalia ujambazi mbuzi! Wenzenu wamepiga maarufu ushambenga wa kutumia mashangingi nyinyi mnazidi kujiongezea mishiko kwa kuwaacha walevi wanyongwe na umaskini! Iko siku iso jina hiyo mishiko itawatokea puani. Shauri yenu. Mwenye akili na atie akilini na mwenye
   
 4. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #4
  Jul 6, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  wakianza kutoa sleeping allowance basi wabunge wa ccm watazichota sana maana ndio wanaongoza kwa kuuchapa usingizi.
   
 5. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #5
  Jul 6, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Naunga mkono hoja,yaani watachukuwa zote wao tu.
   
 6. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #6
  Jul 6, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Juzi juzi wameamua kuingia mitaani na kupambana na shirika la kiza la nchi yao baada ya kuwaweka kizani kwa saa 48 tu. Nyie mmewekwa gizani sasa ni miaka kumi lakini bado hamuamki! Kumbaff nyote.
  Walimu, madaktari na wafanyakazi wengine wanakosa mishahara nyie mnazidi kujirundikia miposho ya uongo na ukweli! Ni ulafi na upogo kiasi gani? Hamuona jinsi mahospitali yalivyojaa magonjwa badala ya madawa? Ama kweli mchoyo hana rafiki na rafiki yake ni tumbo lake. Inatisha kuona huko madongo poromoka mtokako watoto wanakalia mimawe kama manyani wakati nyingi mnaongezeana posho za makalio. Lipeni basi posho za akili kwa walimu na madaktari badala ya makalio yenu.
   
 7. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #7
  Jul 6, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Msiseme nawatukana. Hasha, nawapa ukweli ambao wengi wameshindwa kuwapa. Mnapata wapi jeuri ya kujilipa posho za makalio wakati wale mnaodai kuwawakilisha wakifa kwa magonjwa ya senti kumi? Hamjui kiza kinafanya wakaliane na kulaliana na kuongeza utitiri watoto ambao hapo baadaye watateswa na uchoyo wenu pia akili zao zitajaa kiza kutokana na kukaa kizani tangu tumboni?
  Hapa lazima niwapongeze CHAKUDEMA kwa kuliona hili hata kama kwenye kambi yao kuna fisi kama lile fisi la kisukusi Joni Kibuda. Walevi hawawezi kuendelea kubeba wezi wanaojipa utukufu na uheshimiwa wakati ni wizi wa kawaida. Never, things must be changed. Why should they own everything and give us usufunctuary as the only rights for us? Thubutu yako! Patachimbika bila jembe na patakuwa hapatoshi.
  Mnajilipa posho ya makalio kwa utajiri gani iwapo hata kodi yenyewe hamlipi? Muulize kiranja wao kama analipa kodi. Muulize hata baba yao kama ametaja mali zake. Wanaogopa nini kama si kuumbuka walivyo majizi ya kutupwa yaliyojificha nyuma ya madaraka? Msiseme natukana. Situkani. Kama kusema ukweli ni matusi basi natukana. Nami napaswa kupewa posho ya Kunena ukweli au truthtelling allowance. Kama wao wanapeana posho za majungu, kwanini mie nisipewe ya kupasua jipu? Mimi ni daktari wao ni wagonjwa. Wao wanauhitaji ukweli wangu ila mimi siwahitaji kwa lolote.
   
 8. tz1

  tz1 JF-Expert Member

  #8
  Jul 6, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 2,118
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Pia 'mute allowance'Rostama atazikomba zote
   
Loading...