Kuna tofauti kubwa kati ya Dr. feck na Dr. wa ukweli. Dr. feck anahangaika kuwagandamiza watanzania kwa kutumia polisi ili kuwatisha wamwachie nafasi. Dr. wa ukweli anatumia elimu yake Mungu aliyompa kuwasaidia watanzania waelewe haki zao na namna ya kuzitetea kwa hali na mali. Dr. feck atakuuwa kama alivyofanya kwa Dr. Ulimboka kuwanyamazisha madakari kwani alijua mambo yakiendelea vile hatimae watanzania wote wataamka na kuwafuata madakari nyuma hatimae atabaki na kanga za kijani, tishert za njano, na kofia za kijani bila wa kumgawia. Ninaiomba serikali ya CCM itambue kuwa pamoja na nguvu kubwa sana inayotumia na gharama ya walipa kodi kutugandamiza kwa sasa vinaishia kushindwa. Huwezi kuchanganya maji na mafuta. Wajinga hata watoto wadogo wanaweza kutenganisha. Huwezi kuchanganya ukweli na uwongo. Wapumbavu na hata wasio na elimu watajua tofauti. Huwezi kuchanganya usiku na mchana. Mbuzi, ng'ombe, na kuku watakuambia sasa ni jioni na tunaenda kulala. Ikifika asubuhi wataamka na kuendelea na shughuli zao za kujipatia ziriki. Kwa maana hiyo basi niseme CCM mnajitesa bure. Dr. wenu ni fack na anafanya mambo feck kwa kuwachekea na kuwapumbaza na mnamkubali. Mimi sii mwana CDM wala sitakaa niwe mwana CDM wala mwanachama wa chama chochote kile. CDM wanasema walianza na Mungu na watamaliza na Mungu. Hu ni msemo mkubwa sana kwangu na wengine wote wenye akili timamu. CCM watanzania wanapata mwanga japo taratibu. Nionavyo mimi siku moja wataamka. Kubalini msikubali wanaamka, wengine wameshaamka, wachache wanaendelea kuamka na siku moja wote watamka na hamtakuwa na pa kupita kugawa wala kanga, wala vitenge, wala tishert, kofia, sijui shilingi elfu kumi, elfu mbili nk. Najua mtanipuuza, lakini ifikapo siku hiyo naomba mnikumbuke!