Sasa Majaji kuomba kazi Tume ya Utumishi wa Mahakama

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
36,982
45,900
Uwazi wa Teuzi za Nafasi ya Majaji katika mahakama zetu umeendelea kua mzuri baada ya tume kuamua kuachana na utaratibu wa zamani wa kupendekeza majina wenyewe kwa rais, kwa kuwakaribisha wenye sifa kupeleka maombi ili wafikiriwe katika kupendekezwa.

Hii ni hatua kubwa ya kwanza katika kuelekea mahakama zenye weledi na kutoa haki kwa wakati.

Hongera Magufuli na Hongera Jaji Mkuu.

Naambatanisha tangazo la tume ya utumishi wa mahakama.
IMG-20160718-WA0010.jpg
 
Hatua hii ni kiashiria kwamba sasa tunaelekea kuzuri.

Mahakama huru, zenye kutoa haki kwa wakati na weledi.

Hongera kwa Magufuli na Jaji mkuu.
 
Ni utaratibu mzuri unaoonesha kuwa wana nia nzuri ila angalizo tu kwa tume na muheshimiwa raisi kuwa still special vetting ya vyombo vya ulinzi na usalama inahitajika sana kwa kuwa ujaji sio kuwa umeenda shule tu bali ujaji ni weredi katika busara na maadili kwa kuwa naamini wapo wajuzi wa sheria wengi tu ambao wanaweza kuongoza katika iyo interview ya tume lakini still kwenye maadili wakawa zero.

Mifano ipo na inajulikana. Jaji ni moja ya nafasi nyeti kabisa katika nchi yeyote ile duniani.

Juzi Ruto kajuta kuwa anashindwa ku7mshawishi mwanae asome sheria kwea kuwa Jaji Mkuu wa Kenya anavaa hereni so umakini unahitajika sana kwenye hili.
 
Kwa moyo mkunjufu kabisa. Hii ni hatua nzuri sana kwa ustawi wa jamii na taifa letu. Sasa haya mambo ya kupata "vilaza" na watu kufanya kazi kwa uoga uoga vitapungua kama si kuisha kabisa.

Hongera sana Mh. Magufuli. Transparency is key. Na naamini kabisa hata watoto wa wakulima na wale wasiojulikana Lumumba wataanza kupewa fursa za kulitumikia taifa kwenye nafasi mbali mbali nyeti za taifa letu. Tupunguze siasa kwenye mambo ya msingi kulijenga taifa letu.
 
Tumechelewa sana. Bado nafasi nyingi za juu zinafanyiwa uteuzi usio na sifa kinachoangaliwa mtu katoka kanda ipi .
 
Kama utaratibu huo ungekwenda mbali zaidi hadi kwa wakurugenzi, makatibu wakuu na mawaziri huenda productivity/efficiency ingekuwa juu zaidi kwani tunahitaji professionalism kwenye utendaji ili kusonga mbele
 
Magufuli anahusika vipi na habari hii? Hii wewe una akili hata za kuvukia barabara?
ha ha ha ha..... punguza husda ndugu Matola, matusi ya nini? likifanyika baya anatukwanwa magufuli, likitendeka zuri asitajwe yeye! utajakufa bure na kijiba cha roho.. relax bro.
 
Ni hatua nzuri sana japokuwa uteuzi uko palepale, ukisoma vyema tangazo la ajira linasema ''Waombe ili kufikiriwa kuteuliwa kuwa majaji wa mahakama kuu". Kimsingi bado hatujafika pale tunapotaka kama wenzetu wakenya ambao majaji wanapatikana kwa kufanya usahili. Hapa wanaomba ili wafikiriwe kuteuliwa.
 
ha ha ha ha..... punguza husda ndugu Matola, matusi ya nini? likifanyika baya anatukwanwa magufuli, likitendeka zuri asitajwe yeye! utajakufa bure na kijiba cha roho.. relax bro.
Haha achana nae huyo mkuu,..
 
Magufuli anahusika vipi na habari hii? Hii wewe una akili hata za kuvukia barabara?

Mkuu kuna watu humu hata mvua za masika zikiwahi kunyesha wata sema hongera magufuli kwa kusababisha mvua kunyesha. Tangazo hilo lina faida gani ya msingi hasa ukiangalia? Kwamba unaomba kisha unasubiri kufikiriwa uteuzi?
Kuna tofauti gani na awali alivyokuwa anateua tuu?
Akitaka kumteua Matola na kama hajaomba sii anamwambia omba basi nataka nikuteue! Tuangalie wenzetu hata hapo Kenya tuu, kama ziko nafasi 10 za majaji wapya watu mnaomba hata 100 na kuitwa kufanyiwa usaili kisha wanaopita kumi wanaajiriwa. Hapo Rais hahusiki na uteuzi wala nini.
Watu waache kumsifia huyu mtu kwa kila jambo kama mazuzu, kwanza sasa imekuwa kama kumzihaki.
 
Ni hatua nzuri sana japokuwa uteuzi uko palepale, ukisoma vyema tangazo la ajira linasema ''Waombe ili kufikiriwa kuteuliwa kuwa majaji wa mahakama kuu". Kimsingi bado hatujafika pale tunapotaka kama wenzetu wakenya ambao majaji wanapatikana kwa kufanya usahili. Hapa wanaomba ili wafikiriwe kuteuliwa.
Angalau ni hatua mkuu, ila tunasogea tunapotaka, angalau ile mindset kua wanaoteuliwa ni kina fulani itakua imepungua, tunaelekea mahali, juhudi hii iendelee kwa kuirekebisha katiba yenyewe ili sasa tufikie kule tunakotaka, but..juhudi inaonesha mwanga kidogo, wadau wa sekta ya sheria wanalifahamu hili..
 
Kwa mujibu wa katiba yetu jaji anateuliwa na raisi. kwa hiyo huko wanatafutwa viherehere tu, ndio maana watumishi wa mahakama hawaruhusiwi kuomba hizi kazi
 
Mkuu,ondoa haraka na uandike vitu vya maana. Hata usipoandika humu kwa siku,malipo yako palepale.Rais Magufu ndiye nani? Chunga mkuu!

Mzee Tupatupa

BAVICHA pole sana, hapa ni kazi tu na mabadiliko ya kweli yanaonekana sasa. Siasa zenu za kitapeli tulizikataa 2015.
 
Back
Top Bottom