Sasa Machinga wametushika pabaya

Nilikwenda karume hatari tupu, vibanda vya biashara mpaka sehemu ya stand, hakuna pakusimama abiria kusubiria gari.
 
Ajira hizo Mkuuu
Machinga....
Bodaboda....
Betting.....
Teheteheeeeee
Betting inafanyika kote duniani, tena na mataifa yaliyoendelea. Ondoa betting katika orodha yako.

Mzee baba anazingua sana, hakuna ustaarabu kabisa mitaani Kwa sasa, kila kona kuna kijibanda, hadi barabarani. Lile lorry pale Milimani city ni matokeo ya watu kujipanga pembeni mwa barabara na kujifanyia biashara.
 
Nini kifanyike mkuu!! wenye exposure ya mataifa ya wenzetu hasa Waafrika wenzetu kwani wao wanafanyaje swala la wamachinga!! Ukweli hili swala limekuwa changamoto, Pale round about ya Mwanza jengo la Nyerere wamama wamepanga bidhaa barabaran muda wa jioni umakini unaotajika kwa wenye Magari..
 
Mkuuu tukumbukeni mwamba siyo kila mtu awe machinga. Hivyo yaandaliwe maeneo rasmi ili biashara yao isiwe bugudha kwa wengine"
 
Rais wa wanyonge na masikini. Anasema hao ndio wapiga kura wake waliompa ushindi wa kishindo.
 
Kuwe na maduka 24hrs. Kariakoo, tandika, mwananyamala na ferry.
Mtaa uwe na urefu wa kilometa moja na nusu au mile moja.
Mtaa uwe na taa za kutosha, barabara pana na defender mwanzo, na mwisho. Askari wa miguu katikati.
Kama pattaya Thailand au one moe Manila. Au walau kama forodhani gardens lakini pia kuwe na biashara za vitu vingine siyo chakula tu.
Kariakoo patapungua sana.
 
Yaani Siku hizi Majiko ya kupikia, Nyama/mishikaki Choma, mahindi Choma, wapika Supu, wakaanza mihogo. Ndizi na Chips na Biis Sufuria na Majiko ya Moto ni Barabarani na vituo vya Mabasi vya kuzibiti Abiria. Kuna Siku nilinusurika kuchomwa na mafuta ya Moto ya kwenye Karai njiani. Yaani Biashara ya Chakula ni Holela Pita Mwenge, Posta Mpya, Pamba Road mjini, Ubungo utajionea Usumbufu huu. Hotel zimefungwa Majiko yamehamishiwa Side Walk(Pedestrians ways).
 
Unasema wameshaanza kukupapasa sehemu gani???? Rekebisha sentensi please
 
Unasema wameshaanza kukupapasa sehemu gani???? Rekebisha sentensi please
Mkuuu hao watu wanachungulia kaburini...
Si umeskia wameanza kuparamiwa na malori huko barabarani. Kule Moro waliuliwa, Moshi pia, Majuzi tena Mlimani City tusipochukua hatua yatakuja maaffa makubwa halafu tuseme ni Mipango ya Mungu.
 
Mkuuu hao watu wanachungulia kaburini...
Si umeskia wameanza kuparamiwa na malori huko barabarani. Kule Moro waliuliwa, Moshi pia, Majuzi tena Mlimani City tusipochukua hatua yatakuja maaffa makubwa halafu tuseme ni Mipango ya Mungu.
Kwa awamu hii itakuwa sawa na kumpigia mbuzi gitaa,labda awamu ya 6
 
Picha
 
Mambo mengine yanafanywa kwa ajili ya siasa haijalishi nini kietokea,hata tukio tulilolishuhudia hivi juzi la kutoa wafungwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…