Samsung Z, mwanzo wa Samsung kuachana na Android.

Samsung Z, mwanzo wa Samsung kuachana na Android.

Joined
Jun 3, 2014
Posts
28
Reaction score
16
[h=3][/h]
samsung Z. chanzo: samsung

Hapo jana kampuni ya Samsung imezindua simu ya kwanza duniani inayotumia mfumo wa uendeshaji wa Tizen badala ya Android kama ilivyozoeleka. Samsung Z yenye uwezo unaolingana na simu ya Galaxy S5, ikiwa na vitu kama fingerprint scanner na vinginevyo, inatarajiwa kuingia sokoni baadae mwaka huu.


Lakini wakati Samsung ndio mtengenezaji mkubwa wa simu zinazotumia mfumo wa Android duniani, kampuni ya Google ndiyo inayomiliki mfumo huo. Na hivyo inalazimu watengenezaji wa simu kama Samsung, HTC na wengineo kujumuisha apps kama vile Gmail, na Google+ kwenye simu zao kama moja ya masharti ya mkataba wa matumizi ya mfumo huu kutoka Google.


Kuhama huku kwa Samsung kunaweza kufanya mfumo wa Android kuwa matatani. Kwa sasa Samsung ndio kampuni inayoongoza kwa uuzaji wa simu za mkononi. Mauzo ya Samsung kwa mwanzo wa mwaka huu ni makubwa kuliko jumla ya mauzo ya simu ya washindani wake wanaofuatia; Apple, Huawei, Lenovo na LG. Hapo hapo Samsung inashikilia asilimia 65 ya simu zote zenye mfumo wa Android. Endapo Samsung itahama ghafla, na Tizen itakuwa na mafanikio sokoni, itasababisha Android kushuka thamani. Kampuni ya Google inayoendesha Android yenyewe haitengenezi simu, na hata kwa sasa Android haiingizi mapato makubwa kwa Google. Kuondoka kwa mtumiaji mkubwa wa Android kutafanya Android kuwa mradi wenye hasara zaidi kuliko sasa kwani Google itajikuta inamiliki mfumo ambao una soko dogo sana.


Vile vile kitu kingine kinachotishia uhai wa Android ni kuwa ingawa Tizen ni huru (open source) kama ilivyo Android, Tizen haina utata wa hataza zake (patents). Android inakabiliwa na mashtaka makubwa juu ya baadhi ya vipengele vyake kudaiwa kuingilia hataza za makampuni kama Apple na Oracle. Hivyo watengenezaji waliobakia kama HTC, Huawei na wengineo wanaotumia Android sasa, hawatasita kuhama kambi kwenda Tizen ambako hawatakuwa na wasiwasi wa kushitakiwa kama ilivyoshitakiwa Samsung hapo nyuma kuhusu matumizi ya Android.


Jambo lililo wazi ni kuwa Tizen itachukua muda kukubalika. Mtumiaji wa kawaida huhama mfumo baada ya kuridhika na uwapo wa uchaguzi mpana wa programu (apps). Mpaka pale soko la apps la Tizen (ambalo bado halijaanza) litakapokuwa na apps mbadala wa zile zinazopatikana soko la Google, Google Play, na soko la apps za iPhone, App Store, ndipo Tizen inatarajiwa kutoa ushindani mkubwa katika soko la mifumo ya simu.

source: bofyatz.com
 
Wajipange kwenye apps tu..
Sikuhizi os ni apps bhana..
Nna blackberry q5,trust me ina UI hatari sijawahi kuona,camera nzuri,battery life ni siku nzima with heavy usage,lakin apps za kijinga..
Hadi naichukia..
 
Bao la kisigino kwa android apps makers, hasa hawa uchwara wa kibongo, Ila isiwe rasmi, coz hata windows 8 imebuma sokoni ingawa ilipigwa promo ya hatari na developers wake
 
Nunua sasa hii simu hafu waku abandon peke yako.

Kama mnakumbuka Samsung walivyotoa simu zenye Bada OS, walivyoona mauzo fyongo, wakawaacha wateja wao hadi leo wanalia tu.

Jaribu vyote ila sio OS mpya. Bora ujaribu simu mpya ila OS ya zamani.

Samsung wanajaribu jaribu tu nowadays. Sijui wameishiwa au vipi? Nimeona tena wamerelease Smartphone with 7" screen. Dah, mi nikajua wataiita Tablet, ila wao wamekomaa it's smartphone. Maybe siku hizi wana target soko kwa watu flani flani.

Ila watu tuna mitazamo tofauti. Wadau wengine wameipokea +vely. Wengi wanasema wanahitaji a new non-American OS, kwa madai iOS, Android na Microsoft Windows zote za US zina ruhusu NSA wafanye yao. Ok, let's wait and see.

Hafu hapo mbele na ilo jina "Z" mbona kama Sony?

Cc: chief-mkwawa
 
Last edited by a moderator:
Hata Samsung wanajua android ndo heart yao kwenye soko la simu zao, hii tizen haiwezi kuwa tishio kwa sasa na hata baadae, na tutegemee flagship ya Samsung kuja na android miaka yote unless hiyo tizen iwe nyepesi kuliko android, lakini naamini programmers wa Google hawaiangalii tizen kwa kicheko hata kidogo ikitegemea wote wanatumia kernel aina moja, na sitashangaa kama yaliyowakuta meego na maemo yakamkuta tizen
Ni mtazamo wangu tu.
 
Hata Samsung wanajua android ndo heart yao kwenye soko la simu zao, hii tizen haiwezi kuwa tishio kwa sasa na hata baadae, na tutegemee flagship ya Samsung kuja na android miaka yote unless hiyo tizen iwe nyepesi kuliko android, lakini naamini programmers wa Google hawaiangalii tizen kwa kicheko hata kidogo ikitegemea wote wanatumia kernel aina moja, na sitashangaa kama yaliyowakuta meego na maemo yakamkuta tizen
Ni mtazamo wangu tu.

Well said boss. Ila still Samsung ndio wanaoongoza kwa mauzo ya simu, kwahiyo wanaweza change uelekeo wa OS muda wowote wakiamua aswaaa. Pia kuna uwezekano wasi base sana kwenye hii OS ila wakafanya kama walivyowahi kutoa product zenye Windows OS, au Nokia waivyotoa Android. Ila tumezoea wanatoa low end smarts, mbona hii seems kama high end? Ila sitaki kuamini they want to switch from Android.
 
both are os. But i just want to know which one has been proven wealthy to the final user. my worry is that may be they want to switch to tizen basing on the market conflicts between them though technically it wont favour the customers
 
Mmmmmmmmmmmmmmhhhhhhhhhhhhhhhhh !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! kumbe huku ni- kitekinolojia zaidi ???????? ngoja n'toke mie
 
both are os. But i just want to know which one has been proven wealthy to the final user. my worry is that may be they want to switch to tizen basing on the market conflicts between them though technically it wont favour the customers

kwa fan wa linux wanajua kuwa android ni linux wannabe(based on linux) na sio pure linux yenyewe ndio maana os ni nzito sana. tizen inatokana na meego ya nokia na limo ya samsung kama itakua implemented vizuri basi ina nafasi ya kufanya vizuri.
800px-Mer_and_mobile_operating_systems.svg_.png


os za nokia/linux zinajulikana kwa uwezo wake wa multitasking na wepesi wake, ni kawaida kurun apps 40 kwa mpigo bila ku affect perfomance ya simu. na hii tizen inakubali apps za android na pia ina support ya here navigation. hivyo kama watazichanga karata zao vizuri soko la simu zao zipo hasa kwa simu za bei rahisi.

lakini wakati huo huo samsung kwenye android wana touchwiz ambayo ni skin nzito sana, kama wataport touchwiz yao kwenye tizen wataifanya os yao iwe nzito na ndio hapo itakua haina maana kuwa na simu ya tizen.

ila pia samsung anaweza kuship simu za tizen na touchwiz bila kuwaambia watu na watu wakajua ni simu zao za kawaida sababu tizen inakubali apps za android
 
Back
Top Bottom