GE2025 Samia Suluhu ni wenu

GE2025 Samia Suluhu ni wenu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

SeliSelina

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2014
Posts
418
Reaction score
898
Kumekuwa na mgongano mkubwa sana sasa hivi, na wamekuwa wakilaumiwa wa zanzibari wote.

Tusichanganye uzanzibar na ubara. Kosa la mmoja lisiwe la wote.

Hoja ni kuwa cha kuzungumzia ni ccm hapa wapi imetufikisha, lakini kwa makusudi ya kujitoa fahamu, wanalaumiwa wa zanzibari

Nakamwambie hivi samia suluhu ni wenu.

Mtoto wenu wenyewe. Mmemlea na mkamlewesha. Mlimtengeneza wenyewe. Mkamnyanyua mpaka mkampa urais saivi.

Hivi samia kama samia, haya yote vipi anaweza kuyafanya pekee yake, kama sio nyie kuwa nae.

Kipi haswa kikubwa alichokinufaisha kwa wazanzibari, hatujakiona. Wa zanzibari wana raisi wao. Mwinyi aliyekuwepo kimabavu na yeye.

Samia huyu keshaendewa mara ngapi kwa manufaa ya wazanzibar kanyamaza kimya,

Sikilizeni kampeni ya mgombea wa act wazalendo, alifika kumwambia samia usituue mara hii, samia kakaa kimya, majeshi yaliletwa na serikali ya muungano siku ya tarehe 28 yakapiga kura, pesa za kampeni zilizetwa na serikali ya ccm, bara, vituoni kukawa vurugu mechi wanatia kura wanazotaka, wakaiba na kuiba tena, mwisho wakajitangazia.

Tuliona tubaki kimya, kwa sababu tuliposema tusiuliwa hatujajibiwa, tukaona yatakuwa yale yale mauaji ya kila wakati ya uchaguzi, tumeshapoteza sana,tukaendelea kuomba dua na letu lipo moyoni.

Kwenye kampeni zao ccm , walishasema, kuwa hawaitoi hawaitoi hawaitoi, na damu zimwagike, ushasikia hivyo baddo uende ukaangamize kizazi,

Mgombea urais wa zanzibar kwa ticket ya act wazalendo, alichowaambia wafuasi wake, kwa kuhofia watafyeka. Na wangefyeka.

Mnaposema samia katuua, mmeisahau system?

Samia angekuwa sio wenu mwana wa ccm, vipi angeweza kuruhusu uchafuzi huu kwao zanzibar uendelee,

Kafanya hivyo kwa sababu kuna itikadi ya kuwa zanzibar haiwezi kuwa pekee yake, na lukuvi alokuwa waziri wa ardhi aliyasema hayo kanisani, hawawezi kuiachia zanzibar, na bi samia ndio akaungana nao.

Kwa hivyo samia ni mwana wa ccm kindakindaki kwa maslahi ya ccm sio kwa maslahi ya wazanzibari.

Tusijitowe fahamu , la kukemewa ni chama cha ccm kikiongozwa na samia, sio mzanzibari, hapa kwa kweli mnataka kuleta ubaguzi wa hali ya juu tena,

Ni kundi zima sio mmoja mmoja, samia hana nguvu yoyote ya kujiweka alipokaa, anawezeshwa,

Hivi mnasema jeshi la bara na polisi hawajaua, waloua ni kmkm wa zanzibar, hao waliokuwepo ndio wameua maelfu, bila ya kushirikiana na bara?

Msitake kuwatia hatiani wazanzibar, hapa la kukemea ni chama cha ccm hakiko tayari kuondoka madarakani kwa gharama yoyote ile piga ua.

Wa zanizbari muungano hawautaki toka kwenye miaka ya 80 mpaka hii leo, ila ndio ccm umeushikilia kisawa sawa.

Sasa hapa tuanze kuzungumzi ccm, na wala sio mzanzibar

Samia ni wenu na mnajua hivo, msijitoe fahamu, asingefika mlipomfikisha.
 
Hivi mnasema jeshi la bara na polisi hawajaua, waloua ni kmkm wa zanzibar, hao waliokuwepo ndio wameua maelfu, bila ya kushirikiana na bara?
Hao kmkm wa Zanzibar wakishirikiana na wahuni ndani ya policcm wameua sana hata mitaani ambapo hakukuwa na mikusanyiko wala maandamano
 
Back
Top Bottom