SAME MASHARIKI + SAME MAGHARIBI wafanyiwa UTAPELI NA KIKWETE | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

SAME MASHARIKI + SAME MAGHARIBI wafanyiwa UTAPELI NA KIKWETE

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by kinepi_nepi, Sep 24, 2010.

 1. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #1
  Sep 24, 2010
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ahadi alizotoa JK kwamba atajenga barabara ya kiwango cha Lami kutoka same mjini kupitia Kisiwani, Ndugu, Kihurio na kutokea Mkomazi ni utapeli mkubwa, uongo na uzandiki. Barabara hii imepewa ahadi hizi kuanzia serikali ya Ali hasani mwinyi, Mkapa na sasa Kikwete. Wagombea wa CCM wametumia barabara hii kama mtaji wa kisiasa na huwa baada ya kuingia madarakani wanajifanya hawajui, kwani huwa hawarudi tena Same.

  Tukiwa na wabunge wa CCM tangia uhuru, Chedieli Mgonja aliihujumu same ikawa na hali mbaya ya elimu, afya, na miundo mbinu mbali mbali. Mwingine naye akaleta usanii, akaja mama mzirai naye akajitutmua akapatwa na kigugumizi akapotea, wakaona deal wakagawa Jimbo.

  Mbunge wa sasa Anne Kilango Malecela amekuwa Vuvuzela badala ya kuwaletea watu maendeleo, kweli kakiwanda ambako hakajaisha kako mamba miamba hakawezi kuajiri hata watu 50 anakatumia kuombea kura kwa watu zaidi ya 300000. Sehemu yote ya milimani ina barabara mbovu hazipitiki kukinyesha mvua. Same imejaliwa mbuga za wanyama ya Kambi ya simba na mkomazi iliyoungana na Savo nchini Kenya. Wakazi wa same wanapata sifuri.

  Kuna misitu mingi na mizuri inayoweza kutoa mazao ya mbao kama shengena, ila kinachopatikana ni sifuri kwani hakuna barabara madhubuti na miundo mbinu imara. Tangia uhuru tunapata ahadi zisizotekelezeka.

  Dr. Mathayo kawa bubu na utendaji wake ni bubu. Hedaru ni mji unaokuwa kwa kasi ila hauna maji ya uhakika, ukiachia mbali sekondari inayoendeshwa na Jimbo katoliki la same hakuna kitu. Makanya wao wameachwa wale vumbi la gypsum bila kujua hatima yao, hakuna maji wala huduma za jamii imara.

  Leo mwaka 2010 Jakaya Kikwete akisaidiana na matepeli hawa wanatoa ahadi za miaka 30 iliyopita . Nataka kuona mwisho wa viongozi hawa. Sera za CCM haziwezi fanyakazi tena Same. Hazina wasimamizi zina matapeli.

  We want to put stop on this now and for ever.
   
 2. M

  Mutu JF-Expert Member

  #2
  Sep 24, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  CCM Wazee wa ahadi,Ulimwengu amewaasha vyama kuhusu miahadi
   
Loading...