Same mashariki 2015 lazima liende chadema

Fue Fue

Senior Member
Jan 6, 2013
107
128
Jimbo la Same Mashariki mwaka 2015 lazima liende CDM. Jimbo hili ndani ya wilaya ya same linamatatizo mengi kama lilivyo la Magharibi, kuna matatizo yanayosababishwa na geografia, watu, na matatizo makubwa yanasababishwa na kuwa na uwakilishi dhaifu bungeni na wilayani.

Ili Jimbo hili na wilaya ijikwamue kutoka kwenye tope, lazima kuongeza madiwani wa upinzani (CDM) ndani ya manispaa ya Same. Ilikuweza kusimamia vyema mapato na fedha za mgawo wa bajeti wilayani. Pili kuweza kuwa na wawakilishi wenye maono chanya na uwezo wa kushirikisha wananchi kujiletea maendeleo.

Ahadi hewa na upotevu mkubwa wa fedha za halmashauri ndio kikwazo kikubwa sana cha udidimivu wa maendeleo ya same. Wawakilishi wa jimbo hili wamekuwa vibaraka vya wabunge wa CCM na wabunge wamekuwa wakimbizi wamehama jimbo na kusau waliaomba kuwatumukia wananchi.

Jimbo la Same lina misitu kwa jili ya utalii, wanyama na mbuga ya wanayama kubwa. Lina milima mizuri, mabonde ya kilimo cha mpunga, miwa, kahawa na matunda. Ni jimbo ambalo likipata kiongozi mwenye mapenzi ya kweli kunauwezekano shule, chuo na ajaira vyote vikapatikana same na kuwa kitua kikubwa cha bidhaa na elimu.

Watalii wanakwama kufika kwenye vivutio vingi kwani barabara zake zimesahaulika kabisa, nyingi zikiwa hazipitiki hata kidogo. Shule zinatoa matokea ya kutisha na kuwaacha wazazi wahanga kwa kutumia fedha zao za shida kusomesha watoto na kuambulia sifuri.

Ile ari ya kujiletea maendeleo imeshuka kwani wanasiasa wamekuwa wongo na walaghai huku wakila kila michango ya maendeleo inayochangwa na wananchi.

Miaka 50 ya uhuru jimbo hili likiongozwa na wabunge tofauti wa CCM, limekuwa likizorota mwaka hadi mwaka.

Time to put a stop. This time change is must.
 
Wapare hawawezi kukubali kuburuzwa ni watu makini wanaojiamini.

Wewe ni ----- kweli, wapare si watu makini, ni watu waoga tu wanaogopa mabadiliko.. hili ni kabila la ajabu sana wasioweza hata kujifunza wanashikilia mambo ya ukale..kutokana na uwoga wao wa mabadiliko..
 
siamini kama kweli Wapare ni waoga, ni kati ya wilaya zenye shule nyingi za awali na sekondari mara baada ya uhuru. Kilichowaponza ni uaminifu wao kwa wale waliowaamini.

Daniel Nzira Yona, Chediel Yohana Mgonja, mama Mziray, na sasa Anna Kilango Mallecela- wamewasaliti kwa kiwango kikubwa. Watu wa same walikuwa wakiamini kauli zao, waliwapenda wakijua ni watu wao wote wanajua shida za kwao na wana sababu za kizipigania. Bahati mbaya kila aliyepewa rungu kulinda boma alihama na rungu na kuacha wezi kuiba ng'ombe.

Walifikiri labda usomi na ujana unasaidia wakampa kijana wao David Mathayo akiwa msomi na kijana chini ya miaka 40, ikapiga tsunami ya mwisho.

Wabunge karibu wote waliotoka CCM wamekuwa kupe, wamenyonya damu zao zote wakashindwa hata kuwasaidia. Naama nakubali kwa macho ya CCM wapare ni wapuuzi, naam kwa macho ya CCM wapare ni wajinga, Naam kwa macho ya CCM wapare hawajijui. Hizi ndizo kauli ambazo unampomkirimu mtu akafanikiwa anazitoa. Ni kauli nzuri sana aliyekivulini kiztoa kwani hajui jua lina sogea.

Mwaka 2015 tutajua je kweli wapare wanajijua au la! Tutakwenda , tutawaamsha wote, tutawaelelimisha wote. Watajua kweli watasimama na kamwe hawatarudi nyuma.

CCM imetumia hali duni za maisha, ugumu wa jiografia na barabara mbovu kushinda, kuna vijiji havififkiki kirahisi sehemu za pare bila mvua ikinyesha unakata mawasiliano kabisa.

2015 ni mtu na mtu, tunajua tunasema sema tunamaanisha . Hatujawahi kuona uongozi tangia uhuru. Mwisho wa ulaghai umefika. Karibuni buku saba na lundo la kebehi.
 
Back
Top Bottom