Same kuajiri watumishi wapya 120

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
HALMASHAURI ya Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, inatarajia kuajiri zaidi ya watumishi 120 wa kada mbalimbali hadi kufikia Juni mwakani, lengo likiwa ni kuongeza ufanisi katika kazi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Joseph Mkude alikieleza kikao cha Baraza la Madiwani kwamba watumishi hao watasaidia idara mbalimbali kuanzia watumishi wa halmashauri hadi ngazi za vijiji.

“Pamoja na mipango hiyo lakini lengo la Halmashauri ni kuongeza watumishi wenye sifa kutoka asilimia 75 hadi kufikia asilimia 85 kufikia mwaka 2012,” alisema Mkude.

Alisema katika utekelezaji wa mpango huo, wanatarajia kutumia zaidi ya Sh milioni 11.7 hadi kufikia mwaka 2013/2014, lakini mwaka wa kwanza 2011/2012, watatumia Sh milioni 3.5, mwaka 2012/013, Sh milioni 3.6 mwaka 2013/204 watatumia Sh milioni 4.2.

Mkude alisema miongoni mwa watumishi watakaoajiriwa ni walimu, watendaji wa kata na vijiji kwani imebainika kuwa katika baadhi ya maeneo wilayani humo, kuna upungufu wa watumishi wa kada tofauti.

Aliwaeleza madiwani kwamba ili kuongeza tija kazini, Halmashauri hiyo imepanga kuwapandisha vyeo watumishi 389 wa idara mbalimbali ambao wamekuwa katika nafasi moja kwa muda mrefu.

Awali, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Christopher Irira aliwatahadharisha madiwani kushirikiana na watendaji mbalimbali katika kutekeleza miradi ya wananchi badala ya kutumia muda mrefu kuangalia upungufu wa watendaji husika.

Alisema pamoja na hilo, lakini pia baadhi ya fedha zitakazoelekezwa katika miradi mbalimbali zikibainika kutumika bila utaratibu zitahamishiwa katika kata nyingine zinazoweza kusimamia fedha hizo.
 
Kilimasera asante ila kimya saana kaka tuwekee mambo bwana au umetingwa sijakusona siku mingi,si wengine tuko huku bara hebe fanya mambo basi kwa nyie mlio na access,
regards
 
usihofu mzee kaa mkao wa kula
Kilimasera asante ila kimya saana kaka tuwekee mambo bwana au umetingwa sijakusona siku mingi,si wengine tuko huku bara hebe fanya mambo basi kwa nyie mlio na access,
regards
 
Back
Top Bottom