Samatta Usikate Tamaa, Wewe ni Wa Kimataifa Kweli!!

Baba Kiki

JF-Expert Member
May 31, 2012
1,542
2,000
Leo ni siku ambayo nimemwona Samatta akiwa ametoka uwanjani kwa hasira kubwa baada ya mechi kati ya Taifa Stars na Lesotho. Pamoja na yeye kucheza vizuri na kujitoa kwa 100%, anahisi juhidi zake zilipaswa kuzawadiwa na pointi 3 muhimu kutoka kwa kibonde Lesotho.

Lakini haikuwa hivyo, wachezaji wenzake wamemwangusha, kocha kamwangusha na pia hata refa hakuwa akitoa adhabu sahihi kwa Lesotho ikiwa ni pamoja na kupoteza muda bila kuonywa, kucheza rafu mbaya na refa kutokutoa kadi, n.k

Yote kwa yote, anaonyesha jinsi yeye alivyo wa kimataifa wa kweli, kwa kuamini kuwa tulipaswa kushinda mechi hii. Wachezaji wenzake akili zao ni za hapahapa wanaona poa tu! Hata kocha yuko too passive. Kushinda kwao ni mwujiza zaidi na hii imekuwa saikolojia mbaya sana kwa wanasoka wetu. Hatuna wachezaji wanaojitoa kwa angalau 80% ya uwezo wao na hivyo tuna safari ndefu sana. Tukishindwa kufuzu kutoka kundi hili basi tuachane na Taifa Stars, tuwekeze kwa Serengeti Boys na timu ya wanawake!
 
kumteme

JF-Expert Member
Jun 6, 2017
285
250

hamna wachezaji wapo wazuri tu lakini nimegundua huyu kocha ana udini
 
The Great Emanuel

JF-Expert Member
Apr 3, 2015
2,903
2,000
Sijui msuva yule mnamuita hovyo kabisa jina kubwa uwanjani bashite huyo ulimwengu ndo daaah hafanani na Pro kabisa. Yani samata ukimuangalia unaona kabisa huyu ni PRO ulaya moja sema ndo hivyo atafanyaje.
 
Mr. MTUI

JF-Expert Member
Feb 18, 2013
7,870
2,000
Kila nikiangaliaga mechi ya timu za tanzania matokeo hwmuwa yanatoka vbaya.. Kuanzia sasa sitajihusisha tena na soka la Tanzania.. BBM
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom