Samatta apishana na Man United

client

JF-Expert Member
Dec 13, 2015
619
1,000
SUPASTAA wa Tanzania, Mbwana Samatta ameikosa Manchester United katika hatua ya mtoano ya 32 bora kwenye Europa League baada ya kikosi chake cha Genk kupangwa kuchuana na Astra Giurgiu ya Romania.
Wakati Samatta akikosa nafasi ya kwenda kucheza Old Trafford katika raundi hii, wababe hao wanaonolewa na Kocha Jose Mourinho wamepangwa na Wafaransa, Saint-Etienne na hivyo kuonekana Man United kutokuwa na kazi ngumu katika kusonga mbele.
Mechi kali zaidi zinazotarajiwa kwenye michuano hiyo ni wakati Celta Vigo itakapokipiga na Shakhtar Donetsk, Villarreal na AS Roma, Anderlecht na Zenit, Legia Warsaw na Ajax na Tottenham Hotspur imepangwa na wapinzani wa Samatta kwenye Ligi Kuu Ubelgiji, Gent.
Droo hiyo ya Europa League inamfanya Paul Pogba kukutana na ndugu yake Florentin Pogba, ambaye ni beki wa Saint-Etienne inayoshiriki Ligi Kuu Ufaransa.
Mechi ya fainali ya msimu huu katika michuano hiyo itafanyika jijini Stockholm, Sweden.
 
  • Thanks
Reactions: CDG

mwasu

JF-Expert Member
Jul 13, 2011
10,203
2,000
Akaze buti tu huko na akumbuke kufungua miradi ya kujiongezea kipato mpira ukiisha awe mtu wa kujitegemea na kuheshimika, isije kuwa kama ngasa katoka huko badala ya kusonga mbele karudi mbeya site, mpira si kitu cha mchezomchezo kabisa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom