Samaki samaki Samora, itanivunjia ndoa yangu

Samaki samaki Samora, itanivunjia ndoa yangu

dickdickinyo

Senior Member
Joined
May 19, 2015
Posts
118
Reaction score
53
Aisee huyu Mzungu Mmasai ataniletea majanga kwa wife kitendo cha kufungua tawi hapa opposite na ofisini imekuwa shida kwangu.

Wakati wa lunch lazima nizimue kidogo.Jioni nikitoka ofisini ndiyo nakaa hapo hadi usiku napata vitu huku nikicheki watoto wazuri, wife akihoji kwanini nachelewa, namjibu nilkuwa nasubiria foleni ipungue.

Sasa Jana nimerudi akahoji, hiyo foleni nimeanza kusubiria wiki hii tu?Mbona siku za nyuma nilikuwa nawahi home. Nimetoka asubuhi Leo nimemwacha kanuna balaa.
 
kwa hiyo tumfanyeje mke wako? na sisi tukazugezuge kwa mkeo?
 
Siku zote unatakiwa kuwa Vague kwa mkeo!
 
ni samaki samaki ya diamond plaza kama ni hiyo tukutane hata leo tupate moja baridi
 
Sasa hapo samaki samaki inahusikaje na ndoa yako? Sema wewe ndio unaivunja ndoa yako.

Watu wengi wanafanya kazi posta tena wengine kwenye jengo hilohilo ilipo samaki samaki na bado haiwavunjii ndoa zao. Badilika mkuu!
 
Ulitaka mkeo akuchekee kwa kuchelewa kurudi home kwa sababu zisizo na msingi. Acha upuuzi wewe
 
Hapa ni wewe unatafuta sababu ya kula beer karibu na vimwana ,,,,,,,chaguo ni lako mkuu,
 
Ukimaliza kura bia utaanza kula warembo ili foleni ipungue
 
Aisee huyu Mzungu Mmasai ataniletea majanga kwa wife kitendo cha kufungua tawi hapa opposite na ofisini imekuwa shida kwangu.

Wakati wa lunch lazima nizimue kidogo.Jioni nikitoka ofisini ndiyo nakaa hapo hadi usiku napata vitu huku nikicheki watoto wazuri, wife akihoji kwanini nachelewa, namjibu nilkuwa nasubiria foleni ipungue.

Sasa Jana nimerudi akahoji, hiyo foleni nimeanza kusubiria wiki hii tu?Mbona siku za nyuma nilikuwa nawahi home. Nimetoka asubuhi Leo nimemwacha kanuna balaa.

Hvy vyuo vimefungwa nn
 
Tangu nimejiunga JF sijawahi kuona mada ya maana kama hii nje ya chit chat na vichekesho
 
Umemuacha kanuna....., na leo uchelewe tena.....!
 
Samaki Samaki ndo nini tena? Hawa hawa chakula au kuna kitendawili sijakielewa?
 
Back
Top Bottom