Ezekiel Maige
Member
- Nov 10, 2013
- 11
- 17
Wapendwa ndugu na marafiki.
-
Nawasalimu na kuwatakia amani kwa jina la Bwana wetu Yesu -Mzaliwa!!
-
Tukio hioi la kuzaliwa Bwana wetu Yesu kristu -si tu kwamba ni msingi wa ukombozi, amani-na furaha -yetu sote, bali pia ni msingi wa mafanikio kwa Mambo yetu yote!!
-
Baada ya Wazazi wetu Adam na evan kutenda dhambi na kufukuzwa kwenye Bustani ya Eden, 'network' kati yetu wanaadamu na Muumba wetu ilipotea (Mwanzo 3:23-24)!
-
Ndipo Bwana Mungu, kwa huruma yake kwetu, akamtuma Mwanawe wa pekee, aje atukomboe.
-
Ni kupitia ukombozi huu sasa tuliompokea twafanyika kuwa wana wa Mungu, na kwa njia hiyo, twapata kujibiwa yote tuyaombayo kwani ni yeye aliyetufundisha kuwa"...ombeni mtapewa, bisheni hodi mtafunguliwa na tafuteni mtapewa.... Ni mzazi gani ambaye mwanaye akimuomba mkate atampa jiwe, au akimuomba samaki atampa nuoka?..."
-
Mwaka 2013 tumemuomba Mengi na hakika ametujibia.
-
Kwa ushuhuda wangu, nimemshuhudia akitenda mambo makubwa ya ajabu -ambayo wengi tusingeamini. Mwaka jana, baada ya Shetani kunichafua kwa fitna na uongo mwingi, Mungu aliniahidi--kwa neno lake -katika -Zaburi ya 72:7-9 na 12-kwamba -"...siku zake yeye , mtu mwenye Haki ATASITAWI, na wingi wa AMANI -hata mwezi utakapokoma. Na awe na enzi -toka Bahari hata Bahari, toka Mto hata mwisho wa -Dunia. -Wakaao jangwani -na wainame Mbele zake, -Adui zake na WARAMBE MAVUMBI. Kwa maana atamkomboa mhitaji aliapo, na mtu mwenye kuonewa - iwapo hana msaidizi".
-
Naam, tumeshuhudia haya, na kwa kuwa aliahidi kuwa atatenda kwa wakati wake, basi ataendelea kutenda. Kipekee namshukuru sana kwa AMANI aliyoniahidia na kunitimizia.-
-
Jiulize, ni -AMANI iliyoje utapata -ukiwasikia -"watesi wako" wakikiri kuwa ''...tulimuonea mtu huyu na tumuombe radhi...''-
-
Sote tuna mahitaji-yetu mengi, wengi wetu tukiomba -zaidi AMANI na FURAHA ya KWELI. -Basi na tuende mbele zake tena na kapu la mahitaji yetu 2014. Kwa kuwa sasa tuna kiunganishi cha uhakika baina yetu na Mungu mwenyewe kupitia ukombozi tulioupata kupitia kwa Mwanawe, basi tuombe kwa Imani-Na hakika tutapewa.
-
Na kwa jina lake, basi nawatakieni AMANI IWE KWENU. Baraka zake tele ziwashukie nyote.
-
Kwa wale tuliojitwisha zigo la kuwa watesi -wa wengine, basi na tuzaliwe naye Mkombozi wetu.
-
-Kama ilivyowezekana kwa Sauli aliyekuwa akiwatesa wana wa Mungu kuacha matenda hayo na kuungana nao na hatankuwa Mtume wake (Paulo), Inawezekana na kwako pia. Hujachelewa.
-
Ndugu yenu,
-
Ezekiel Maige-