Sam Mahela wa ITV apewa vitisho baada ya kutoa habari ya abiria waliokwama na treni

Platnam

JF-Expert Member
Mar 1, 2011
767
1,213
Sam Mahela-ITV

 
Pole sana Sam Mahela na Mungu akupe nguvu ya kuendelea na hiyo kazi yako! Mimi nauliza swali moja tu, je kwa mfano Treni hiyo ingekuwa imepata ajali ni kwamba hao watu wasingetaka pia ndugu zao wasipate habari kupitia vyombo vya habari kama ITV na vituo vingine??

Dawa yao ni kuwaondoa madarakani na tunataka utawala mwingine!
 
tupe hizo namba na sisi tuwatishe!!!

infact hapo unawaharibia watu kazi zao...hiki ni kipindi cha kuandaa sahani tena kwa ajili ya Chakula, na wewe unaanza kufagia mavumbi, kwenye nyumba ya udongo!!
 
Mungu atawasambaratisha adui zako na utawatafuta hutawaona tena.ulinzi wa kimungu na uwe juu yako sam.
 
Na hakuna wengine Zaidi Ya CCM, watanzania wenzangu iambieni CCM basi imetosha.

Tunatamani kuziona na sisi Air Tanzania zikiruka kama zilivo ndege za Ethiopia, Rwanda na Kenya.

Jaman tunatamani kuiona TTCL ya Tanzania iking'aa zaidi ya Vodacom, Tigo na Airtel.

Jaman watanzania wenzangu mbona hatuipendi nchi yetu hivi? Au ninyi mnaoishabikia CCM ni wa Burundi?

Tunahtaji kuiona reli ya Kati na Tazara zikibeba watu kila siku na mizigo kupunguza malori barabarani, Watanzania tusife tena kwa ajali za barabarani.

Watanzania wenzangu CCM imewaloga na nini?
Mnahtaji Maombi?
Au mnaitaji kupelekwa kwa mganga ili ilo limbwata litoke?

Semeni basi tuwasaidie kabla ya October 25, tunahtaji Mabadiliko jaman, Tunahtaji nchi Mpya, tunahtaji watu watakaoiondoa nchi hapa ilipokwamia.

Natamani kusikia Mutex, Mwatex ikifanya kazi, watu wakibadilishana shift Usiku na mchana kuingia kazini. Natamani, natamani.

Natamani kuona Twiga hawapandi ndege mimi. Nataman kuona UMEME haukatiki siku 365 za mwaka, natamani.

Watanzania wenzangu tamanini basi kama mimi.

Uwezi panga nyumba moja baba mwenye nyumba anakusumbua unakomaa tu eti nikihama huko pia mwenye nyumba atakuwa kama huyu, mmh si kweli hama, watu hawafanani.

Hata CHADEMA na CCM havifanani. Ikomboe Tanzania. Lete kura yako UKAWA, wakishindwa miaka Mitano kuonesha njia, tuwawatoa kwani TATIZO LIPO WAPI?

Tanzania sio ya CCM, Tanzania sio ya CHADEMA, Tanzania sio ya CUF, Tanzania ni nyumbani kwangu mimi na wewe.

IPENDE TANZANIA WEWE MTANZANIA, HII NI NYUMBA YAKO, NI NYUMBA YA WANAO, NA VIZAZI VYAKO VYOTE VITAIJIVUNIA nyumbani TANZANIA milele

MABADILIKO NI SASA CHUKUA HATUA.
 
Njoo kwanza na verified user huchelewi kuja kukana bandiko hili.
 
Hatukupewa roho ya hofu, na pia Biblia inasema ni vyema kuteseka tukitenda mema ambayo ni mapenzi ya Mungu, maana tutapata thawabu kutoka kwa Mungu 1 Petro 3:17. Tunapotenda haki Mungu anakuwa upanda wetu na vita vinakuwa ni vyake YEYE, washindanao na BWANA watapondwa kabisa, Sisi tulio nuruni tunalindwa na nguvu ya MUNGU siku zote 1 Petro 1:5, Pia hatupaswi kuwaogopa wawezao kuua mwili tu, bali tunapaswa kumuhofu awezaye kuua roho na mwili. Kingine hutakufa bali utaishi kwa ajili ya BWANA. BWANA yuko upande wako, usihofu kamwe. Mwanadamu ni nani mbele za Mungu?
 
Mahela unaiumbua CCM wakati huu wa kampeni. Huoni kwa kuonesha madhila yale watu wa Tabora, Kigoma na Mwanza watazidi kuikacha CCM na kuchagua mabadiliko? Huoni kuwa ile habari imezidi kuwapa UKAWA big up? Haya bwana!
 
Umetoa taarifa polisi lakini?

Maanake JF utaishia kupewa pole tu Mkuu.
 
Pole sana Sam, Asante kwa ujasiri wa kutuonesha na yale magodoro wanayokalia na kulalia watu mpk Kigoma!
...lazma maCCM ayo maana umeyaumbua sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…