Salamu za sikukuu ya Christmas kwa wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam

Egnecious

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
871
1,000
SALAMU ZA SIKUKUU YA CHRISTMAS KWA WANANCHI WA MKOA WA DAR ES SALAAM

Ndugu wana Dar es Salaam,

Kwa niaba ya serikali ya Mkoa wetu, napenda kuchukua fursa hii kwa dhati kabisa kuwatakia waumini wote wa kikristo na wana Dar es salaam kwa ujumla sikukuu njema ya Christmas yenye furaha, upendo, amani na utulivu.

Ni muhimu wana familia kuchukua tahadhari za kiusalama katika siku hii ikiwemo kuongeza umakini na uangalizi wa watoto maeneo ya fukwe (beach) ili kuondoa uwezekano wa maafa, kutoondoka nyumbani bila kuacha angalau mtu mmoja mzima wa kubaki kutazama usalama wa nyumba na kuzidisha umakini katika matumizi ya barabara.

Tusisite kutoa taarifa kwa jeshi letu la polisi pindi tunapoona viashiria vya uhalifu au kuvunjika amani katika maeneo tuliyopo.

Nawasihi tutumie siku hii kuiombea nchi yetu iendelee kuwa ya amani na utulivu, na tuwaombee viongozi wetu akiwemo Rais wetu mpendwa Dr. John Pombe Joseph Magufuli na wasaidizi wake wote ili waendelee kuitumikia nchi yetu vema.
Aidha tuwajali wagonjwa, walemavu, yatima na watu wasiojiweza katika maeneo yetu tunayoishi ili nao waweze kusherehekea siku hii kwa furaha.

Mwisho nawatakia heri, furaha na amani katika sikukuu hii ya Christmas.

ALLY HAPI
KAIMU MKUU WA MKOA
DAR ES SALAAM
1482647794609.jpg
 

Mwasita Moja

JF-Expert Member
Dec 31, 2015
2,906
2,000
Hivi waliotangaza kuwa maisha ni magumu sana mabasi yamepaki hamna abiria wa kusafiri, wanajisikiaje kuona watu wamekosa mabasi ,na wengine wakidandia coaster kwa nauli mara mbili.

Aibu ya kufungia mwaka hii.
 

busy bees

JF-Expert Member
Aug 26, 2016
2,251
2,000
Ally Hapi ... Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam .... wapi mh. Makonda?
 

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
28,777
2,000
Salamu za sikukuu au unatutaarifu kuwa unakaimu ukuu wa mkoa, acha ushamba dogo
 

Gut

JF-Expert Member
Jan 18, 2016
2,837
2,000
Hivi waliotangaza kuwa maisha ni magumu sana mabasi yamepaki hamna abiria wa kusafiri, wanajisikiaje kuona watu wamekosa mabasi ,na wengine wakidandia coaster kwa nauli mara mbili.

Aibu ya kufungia mwaka hii.
Huwezi kushindana na Wachaga piga kimya.
 
Sep 27, 2016
24
45
Udc & urc ni vyeo vitokanavyo na kumtaja mtukufu kwa kumsifia ujinga kila wakati so msimshangae Happi anapalilia udc wake maana akijisaha atetenguliwa
 

Nas Mapesa

JF-Expert Member
Jul 31, 2014
4,105
2,000
Angeiambia familia yake,kuna ulazima gani kututangazia ilhali mifukoni tumebaki vumbi tu.
 

Obama wa Bongo

JF-Expert Member
May 10, 2012
5,276
2,000
nafikiri ingekuwa bora tuwaombee wadogo zetu waliokosa mikopo ya elimu ya juu na waliokosa ajira hasa walimu wa sanaa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom