Salamu za Nusu mwaka

Msamiati

R I P
Joined
Mar 6, 2011
Posts
1,063
Reaction score
700
Hallow my Best Friends, Iam more than happy kutambua kuwa mola amenijalia kuingia ngwe ya pili ya mwaka huu(2014) nikiwa hai pamoja na wasomaji wangu wote. sijui kama ni utaratibu wa kawaida, ila naamini ni nidhamu na adabu yakipekee, kumshukuru mwenyezi mungu kwa kutuwezesha kumaliza nusu ya mwaka tukiwa salama.

Amini usiamini kama watu wangepiga kura kuwa nani atangulie mbele za haki kati yako na Marehemu Director George Tyson, safari yako ingeishia mwezi mei, ila kwa kuwa anayeamua hatma ya kila mmoja ni Mwenyezi Mungu, muamuzi wa haki na asiyekuwa na mshauri, This is another opportunity given to you, Mwenyezi Mungu anajua nini unataka kufanya na ameona nyota kubwa ndani yako, ndio maana amekupa fulsa hii.

Kwakuwa Mungu amekuthamini mpaka kufikia hatua ya kutoa fursa hii kwako, sasa unatakiwa kudhihirisha kuwa umestahili fulsa hii. Haijalishi hata kama bado vikwazo ni vingi mpaka kutimiza malengo yako mwaka huu, amini aliyekupa fulsa ya wewe kuendelea kuwepo ameona kwamba utavishinda vikwazo vyote na havita kuangusha.

Usijihoji kwa kasi ndogo ya kuelekea kutimiza malengo yako ya mwaka, Jihoji kwa mazuri machache ambayo umeshayafanikisha na mipango madhubuti ya kupasua mepesi yaliyobaki kabla mwaka haujakatika, Usitizame vikwazo vilivyotingisha mahusiano yako kwasabau umepewa fulsa kubwa zaidi ya kuyaimarisha. Usijihukumu kwa nafasi ulizozipoteza kwani nafasi na fulsa ulizonazo sasa ndizo zilizokuwa zinahitajika kwenye mafanikio yako.

Ungana na mimi kuamini usemi wa mwanafalsafa mmoja unaosema "Kama umeweza tamabaa Basi unaweza tembea". Mungu alieona ukubwa wa ndoto zako ndani ya mwaka huu, na uwezo wa ajabu ulio nao wa kutimiza Malengo yako yote, ana nguvu kuliko Bosi aliyekunyima kazi, kuliko adui anaekuwekea vikwazo, kulikojirani anaekutabilia mabaya, Kuliko Rafiki anaekuletea uadui.

Fumba macho kisha uitazame picha kubwa aliyoiona Mwenyezi Mungu picha ya malengo yako ya mwaka huu yakiwa yametimia, Mwenyezi Mungu ameiona na kuiwezesha taswira hiyo ndio maana amekutunuku kuingia nusu ya pili ya mwaka huu.

Mwisho fikiria kuingia mwaka 2015 bila upinzani kwa kushiriki katika kuifanya dunia iwe sehemu salama na yenye amani kwa maisha ya wanadamu. Usiwe kikwazo cha aina Yoyote wala Usisababishe Maumivu ya makusudi kwa kiumbe chochote. Toa Zaidi, Penda Zaidi, Jali Zaidi, Saidia Zaidi na Mwenyezi Mungu Atafanya Badala Yako Zaidi.

Nawatakia Mafanikio Mema. NAWAPENDA SANA.


From the Author of The Second Door
 
wenzio tunamiaka mi5 humu na hatujatuma salamu,
Asante
 
wenzio tunamiaka mi5 humu na hatujatuma salamu,
Asante

Nikitumia Account Yangu Ya Olevel nitakuwa nimekuzidi miaka 3 lakini nadhani kwa account hii tupo sawa kwa tofauti ya miezi kidoooooooooogo🙂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…