habari ya hapa
JF-Expert Member
- Dec 20, 2012
- 12,791
- 8,743
Ninamshukuru Mungu, muumba mbingu na ardhi, kwa upendo wake kwetu, ametupa uzima na hatimae tumeuona mwaka 2016, kwani wengi walitamani lkn hakuweza kuuona mwaka ila me na wewe tumefanikiwa hakika ni jambo LA kushukuru.
Namshukuru Mungu pia kwa sababu ni Mara yangu ya kwanza kuweka bandiko ktk jukwaaa hili, na kwakuwa tunaanza mwaka si mbaya kutoa salamu za mwaka mpya kwa kusema mawili matatu,
2015 ni mwaka ambao ulikuwa na matukio mengi ya kihistoria hasa ktk taifa letu Tanzania, pengine hata maisha binafsi, kifamilia Kuna mengi tumepitia hakika hautasahaulika.
Tunaanza mwaka mpya na mambo mapya kwa kuwaomba watanzania wote , bila kujali itikadi zetu za vyama, dini, rangi ama kabila, na kwakuwa sisi ni ndg wa taifa moja tupendane, tuheshimiane, tuthaminiane, tusameheane kwa sababu binadamu wote ni sawa na kila MTU anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake.
Kila MTU wa taifa hili anayo haki ya kuwa huru na kuishi km MTU huru, kila mmoja wetu anastahili kuwa huru na anayo haki ya kutoa maoni yake na kuelezea fikra zake, na pia kila RAIA wa Tanzania anayo haki na Uhuru wa kushiriki kikamilifu ktk kufikia maamuzi yake binafsi ama yanayohusu taifa.
Hivyo basi dini zetu, itikadi za vyama, kabila zetu zisitugawe badala take tudumishe umoja na mshikamano wetu, MTU yeyote ataekuja kwa mgongo wa dini, chama au kabila kwa lengo LA kutugawa tunamlaani na kumpinga kwa nguvu zote kwani ni adui wa taifa.
Mwisho ninawapenda wote na ninawaomba watanzania wenzangu kila mmoja kwa nafasi yake alonayo atende haki, asimamie haki na atetee haki.
Asanteni