SALAM MAALUM KWA DR MAGUFULI

Dazzle 2

Senior Member
Oct 9, 2015
125
71
Kwanza nikutakie heri ya mwaka mpya rais wetu mpendwa. Pili nikutakie afya njema na ulinzi wa Mungu pamoja na Jeshi la malaika wa mbinguni maana kazi yako bila Mungu ni sawa na nchi bila jeshi imara.

Katika salamu hizi nakuombea mwaka huu uwe mwaka wa mafanikio kwako kama mjumbe uliyepewa dhamana kubwa ya kutuongoza watanzania ili kufika kule ambako Mungu alidhamiria tufike. Yawezekana tumechelewa kufika lakini Mungu akiwa upande wako na upande wetu nani awezaye kuwa juu yetu? Silaha za Mungu zina nguvu kuliko silaha za binadamu hivyo nakutakia ulinzi wa Mungu katika kipindi cha mwaka huu.

Rais wetu na mjumbe wetu kazi iliyo mbele yako ni kubwa na ngumu na inaweza kukuletea maadui wengi wa ndani na nje lakini tunaye Mungu na pia unao watanzania wakukuombea. Ni maombi yangu kuwa katika mwaka huu Mungu akufanyie yafuatayo

Mosi, Adui zako wakawe maadui wa Mungu. Yaani atakayekugusa au kukunenea mabaya Mungu ashughulike naye

Pili, njia zako na hatua zako ziongozwe na Mungu mwenyewe. Akupe hekima na maarifa ktk kutenda na kuamua kwa haki. Maana haki huinua taifa bali dhambi ni aibu kwa watu wote

Tatu, ni maombi yangu kuwa ukiwa kiongozi wa nchi hii Mungu akutumie kuinua uchumi wa nchi hii.Akutumie kuleta usawa na pia akusaidie katika kuokoa mali za taifa hili tajiri ambalo kwa muda mrefu wageni wamepora mali zetu.

Nne, nakuombea afya yako na familia yako.Maana naamini tutakapokuona una afya njema na tabasamu hata sisi unaotuongoza tutafarijika na kuendelea kuchapa kazi.

Tano, kwa muda mrefu wengi wetu tumekuwa wazembe, wazururaji, watu wasio na malengo ya wapi tunaenda au watu wasiojua kesho yetu. Hata wale tuliopewa dhamana ya kuwahudumia wananchi tumeingia katika mitengo ya rushwa na uvivu usioelezeka.Mwaka huu umeanza kutuamsha. Ni maombi yangu kuwa utaendelea mbele kwa msaada wa Mungu kuwahimiza na hata kuwaadabisha wale wanaozembea na kutokufwata taratibu za utumishi wao

Sita, Najua wapo tutakaoumia kwa sababu tulizoea kudeka lakini kama baba apendaye watoto wake usituonee aibu pale unapoona tunaenda pembeni.Faida yake tunaweza tusiione sasa lkn baada ya muda tutaiona.

Mwisho, nakutakia baraka za Mungu na utumishi uliotukuka. Rais wangu wenye dhambi wakikushawishi utende uovu usikubali,wakisema njoo tumuonee huyu au kutafuta faida kwa dhuluma Mungu wako akusaidie useme HAPANA maana mchungaji akipotea kondoo watafanyaje?

Basi amani ya Mungu ipitayo akili zote za wanadamu ikuhifadhi moyo, nia na mawazo yako katika kutenda, kusimamia na kuongoza ktk haki yote.
HERI YA MWAKA MPYA RAIS
DR JOHN POMBE MAGUFULI
 
Naungana nawe kuomba kwa ajili ya Raisi wetu apendae nchi yake na watu wote waishio ktk hii nchi Mungu amhifadhi na ampewe maarifa mema yatakayoleta maendeleo ktk hii nchi. Eee Mwenyezi Mungu Tubariki. Amen!
 
Back
Top Bottom