Salaam za Kisukuma: Eeng'washi, Eeminza, Ng'waguku, Ng'wanene... Msaada

Salaam za Kisukuma: Eeng'washi, Eeminza, Ng'waguku, Ng'wanene... Msaada

Bagalu bichane, aliyoneyo, nandje kwa kubagisha pye!

Salaam kwa wote. Samahani wakuu, inaniwia vigumu kuandika kwa kutumia lugha moja kuwasilisha hoja na maswali yangu. Ningelipenda sana lakini inanishinda.

Kwa waelewa na wataalam wa lugha ya Kisukuma, naomba msaada kufafanuliwa matumizi fasaha ya vitambulishi na vipokeo vya ukoo na ukubwa kiumri katika salaam.

Kuna mameno kama: eeng'washi na eminza, yananitatiza. Nambelejagi babehi, naduma geteh oukwelelwa. Nakoubiza nabona majonginjongi douhu!! Anguh lekaga nafunye mifano ahaseleleh ahah:

-- bibi na babu mzaa mama unamsalimia kwa vipokeo vipi?
-- bibi na babu mzaa baba unamsalimia kwa vipokeo vipi?

--mjomba unamsalimia kwa vipokeo vipi?
--shangazi unamsalimia kwa vipokeo vipi?

--mama mdogo/mkubwa unamsalimia kwa vipokeo vipi?
--baba mdogo/mkubwa unamsalimia kwa vipokeo vipi?

Na salaam nyinginezo mbalimbali ambazo utaweza kuzielezea. Akhsante.


Steve Dii
Kuishi kwingi kuona mengi...hizi lwimbo ni idols (miungu) ya kisukuma.

Hapo ndio kuna shida maana unajikuta kwenye mgogoro hasa unaposoma amri kumi za Musa. Hasa Ile amri ya kwanza
 
Mfano nimekutana na baba mkubwa/mdogo ,naanzaje kusalimiana nae ,tena ikiwa Mie ndo nimemkuta amekaa ??

Mtiririko wa salamu unakuaje mwenye kujua anisaidie?
 
Mfano nimekutana na baba mkubwa/mdogo ,naanzaje kusalimiana nae ,tena ikiwa Mie ndo nimemkuta amekaa ??

Mtiririko wa salamu unakuaje mwenye kujua anisaidie?
Mara nyingi anayemkuta mwenzie ndio huanza kusalimia kwa mtiririko wa umri mkubwa kwenda chini, salaam za kisukuma huchukua muda mrefu kwani hujumuisha na watu/Vitu vingine vya kijamii ambavyo havipo kama mvua, afya ya zizi la ng'ombe, mimea shambani na chochote kile kinacho trend kwa wakati huo hujadiliwa ndani ya salaam na ndani ya kusalimiana ndipo utagundua kuwa huyu " LWIMBO" wake Ni fulani na ikishindikana basi option ya mwisho utamwuliza babu yake
 
eng'washi ni salamu ya kitoto yani kama (HI) kwa wazungu, salamu mkato. inatumika sana mkoa wa Mwanza. hatahivyo wazee wengi ukimsalimia ukamwitikia eng'washi, bila kumuuliza lwembo(heshima yake) atakujibu mh'wamashi. yaani babuyako ni mavi(kinyesi)
Lwimbo ni heshima kwa wanawake ambao walikuwa viongozi kipindi hicho, ndo maana majina ya Ng'washi, Minza ni majina ya kike, kuna stori nilimsikia babu alikuwa anaongea na wanafunzi wa shule moja ya biblia ( Majahida) bariadi, nahisi walikuwa na project fulani wakaambiwa watafute wazee wa zamani, sema kipindi hicho nilikuwa nipo school, sikuwazingatia
 
Wasukuma Karibu wote wanalingana desturi miko tamaduni na kusikilizana bila kujali ni Wa eneo gani!
Ila kuna baadhi katika matamshi wanaweza pishana na Wa sehemu ingine! Kama ilivyo kiingereza cha Us na Uk na Australia! Lakini chote ni kiingereza!
Yote ni jamii moja iliyotoka "Africa ya kati na Mali, ukiangalia kwa umakini, mgawanyiko ulianza baada ya jamii hiyo iliyopo pembezoni mwa ziwa victoria kujiita wao ni wa Kaskazini( Sukuma) sukuma maana yake ni wa kaskazini wakijitenga kulingana na pande nne za dunia, hata hao wanaojiita wanyamwezi, watu tu walishindwa kuwaita Bhanang'weli, na kuna wa Kia na Dakama, zote hizo ni pande za dunia
 
Sasa kuna wale wana asili ya utusi, wanaitwa Wadushi, sema hiyo stori babu yangu alikuwa anawahadithia wanafunzi, kosa nililofanya sikuzingatia
 
Kuishi kwingi kuona mengi...hizi lwimbo ni idols (miungu) ya kisukuma.

Hapo ndio kuna shida maana unajikuta kwenye mgogoro hasa unaposoma amri kumi za Musa. Hasa Ile amri ya kwanza
Zilikuwa ni tawala za kale, zilizoongozwa na wanawake, Ndo maana babu anakupiga na "Ngwanene"
 
Yote ni jamii moja iliyotoka "Africa ya kati na Mali, ukiangalia kwa umakini, mgawanyiko ulianza baada ya jamii hiyo iliyopo pembezoni mwa ziwa victoria kujiita wao ni wa Kaskazini( Sukuma) sukuma maana yake ni wa kaskazini wakijitenga kulingana na pande nne za dunia, hata hao wanaojiita wanyamwezi, watu tu walishindwa kuwaita Bhanang'weli, na kuna wa Kia na Dakama, zote hizo ni pande za dunia
Una ushahidi wa kimaandiko kuwa Ethnics ya wasukuma walitoka Central Africa na Mali ?
 
Sehemu ya nadharia ya uhamiaji wa kale wa Bantu, ikitokana na tafiti za kisayansi za lugha na historia za kiasili
 
Pia tafuta kitabu hiki
Derek Nurse & Gérard Philippson – The Bantu Languages (2003)
Muhtasari: Ushahidi wa lugha unaonyesha mzunguko wa makabila ya Bantu kutoka Afrika ya Kati, na Wasukuma ni sehemu ya familia hii ya lugha.
 
Back
Top Bottom