Salaam za CHADEMA toka Chalinze, watu hawamjui mgombea wenu

Salaam za CHADEMA toka Chalinze, watu hawamjui mgombea wenu

utaifakwanza

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2013
Posts
14,193
Reaction score
2,815
Makamanda .......
Pipoz power...!
Hapa mpaka kieleweke ..
Jamani huu uongozi wa Freeman Mbowe na Dkt Slaa hautufai .......
Leo nimejaribu kufanya tafiti ndogo sana kuhusu nguvu ya Chadema katika jimbo la Chalinze. .....

Nimeanza kwa kutembelea vijiji vifuatavyo;. ....

KIDOMOLE
FUKAYOSI
FITINA
BAGO
MSINUNE
MASUGURU
MSATA
MIONO
LUGOBA
VIGWAZA ......

Yaani hakuna hata mtu mmoja anayejua habari ama uwepo wa Chadema ......

Yaani huku Chalinze makamanda tunahali mbaya.

Yaani ukisema CHADEMA wanamjua Zitto Z Kabwe tu .... hata huyo mgombea wa Chadema hawamjui ........

Timua Mbowe na Slaa tuimarishe Chama ...
 
Mkuu salama, Mbona unafanya siasa za chuki na Uongo. Mimi ninafanya kazi maeneo hayo yote Kidomole, Fukayosi, Mkenge,Kiwangwa, Bago, Mwavi, Msinune Miono, Kikaro, (mbaya zaidi hakuna kijiji wala kitongoji kinaitwa Fitina ujue ulivyo muongo) n.k Kote huko uwepo wa CDM unajulikana ila hujuma ndio nyingi. Ukitaka kujua ongea na watu wakiwa wametulia bila hofu ya kujua wanaongea na nani ndio utatambua ukweli. Mfano kata ya Kiwangwa kulikua na uchaguzi wa Diwani 2012 unajua kilichotokea? na Mpaka sasa unajua hali ikoje. ni hayo tu.
 
mkuu, mbona wewe unatafsiri vibaya?? mimi nimeripoti ninachokijua kwa hakika ila wewe ndio unajaribu kuuficha ukweli....mficha uchi hazai.. muda na kura ndio vitasema kama chadema inafahamika chalinze ama laa. fanya utafiti
 
tatizo la machadema ni ujuaji mwingi, hayataki kuambiwa ukweli wa madhaifu yao
 
Utafiti umeanza asubuhi na umeweza kufikia kwenye kata zote kweli wewe ni mkali ulikuwa unatumia chopa nini?
 
vipi hawajampeleka mini kabang huko kuwa meneja wa kampeni?
 
yule mungu wao wa kuzimu waliyeanza nae aliyewatoroka kule kalenga na sasa anawaita huko kuzimu. mungu wa kuzimu alitoa na sasa anatwaa, jina la huko kuzimu lihimidiwe. Amen!
 
Watanzania mnachekesha kweli hivi bado hamjui kuwa palipo na wajinga wengi ndipo CCM upendwa sana ?
 
Acha kutukana watanzania jnuswe... kama CCM inapendwa na wajinga basi wote walioichagua ccm uchaguzi mkuu uliopita ni wajinga... sasa piga mahesabu ni watanzania wangapi walichagua hicho chama. Busara na hekima ni muhimu kabla hujasema chochote. Kuwa mstaarabu!
 
Makao Makuu wamegoma kutoa Chopa.

Hivi Chopa inatoka makao makuu au moshi? Hata hivyo naona kichapo cha kalenga kimewafunza adabu na hawajui tena namna ya ku-deal na Chama cha mapinduzi. Mbinu zote zimegonga mwamba.
 
Yericko Nyerere mbona siku hizi hatukusomi tena ukiripoti moja kwa moja kutoka uwanja wa ukombozi?
 
Last edited by a moderator:
Ama kweli nguvu ya cdm ni zitto,yamewakuta Slaa na mbowe,naona sasa mpo kimyaaaaaaaa.......................Zitto ni mkombozi wa wanyonge na cdm ni mkombozi wa wachaga.
 
Gasamcha, jnuswe amenena vema. Baadhi ya sababu za msingi zinazofanya CCM kushinda chaguzi kwa sasa ni 1) kuiba kura 2) wapinzani kutokuwa na shahada za kupigia kura. 2014 daftali la kupigia kura likiboreshwa ndio ukweli utajulikana kama kweli watanzania wanaipenda ccm au la
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom