Jamani, kwa watakaoguswa tu, wasali sala hii kwa siku tisa. Naomba radhi kwa wasiohusika na madhehebu ya aina hii.
Sala ya kuwaombea watanzania na Tundu Atipas Lisu ushindi dhidi ya mashambulizi ya kitengo cha wasiojulikana.
Kwa Jina la Yesu Kristu, Wajaze Roho mtakatifu watu wasiojulikana Watambue kuwa “Kutenda Haki na Hukummu Humpendeza Bwana kuliko kutoa sadaka” (mithali 21:3)
Mungu Baba, Katika Jina la Yesu Kristu wa Nazareti wape ufahamu watu wasiojulikana watambue kuwa “Azibaye masikio yake asisikie kilio cha maskini, mnyonge, yeye naye atalia, lakini hatasikiwa (Mithali 21:13)
Baba tunakuomba mtie nguvu Tundu Antipas Lisu, mjalie afya njema awezekupona haraka na kurudi katika mapambano. Wape faraja familia yake na watanzania woote.
Tunakuomba hayo kwa Jina la Yesu Kristu Bwana Wetu,
AMINA.
Sala ya kuwaombea watanzania na Tundu Atipas Lisu ushindi dhidi ya mashambulizi ya kitengo cha wasiojulikana.
- Ee Baba Mungu Mwenyezi, Mungu wa Ibrahim, Mungu wa Isaka Mungu wa Yakobo, Tunakuabudu, tunakutukuza. Tunakushukuru kwa zawadi ya uhai, tunakushukuru kwa mapaji mbalimbali liotujalia.
- Bwana Yesu Kristu alisema “Kweli nawaambieni chochote mtakachomuomba Baba kwa jina langu mtapewa”, akasema Ombeninanyi mtapewa kwa maana kila aombaye hupokea’ (Mathayo 7:7-8)
- Baba , Tazama Taifa letuTanzania linakabiliwa na tishio la amani, watu wasiojulikana wamejenga hofu miongoni mwa wana wa nchi hii. Taifa linapita katika kipindi kigumu. Matukio ya utekaji, mauaji, kukamatwa hovyo na haki za wananchi kuminywa vimetawala. Tunakuomba Ee Bwana, uturejeshehe amani na utulivu katika Jina la Yesu Kristu.
- Imendikwa kuwa Jina la” Bwana ni ngome Imara ambapo mwenye haki hukimbilia na kuwa salama” (Mithali 18:10) Bwana tunakushukuru kwa kumuhifadhi Tundu Lisu katika ngome yako, kwa maana ni mwenye haki na mtetezi wa haki za wanyonge. Tunakuomba uendelee kumuhifadhi katika ngome yako katika Jina la Yesu Kristu.
- Imeandikwa kuwa “Silaha zote zilizoundwa kunidhuru hazitafaa chochote kile” (Isaya 54:17) Bwana tunakushukuru kwa kutimiza maandiko hayo kwa kuyeyusha risasi zaidi ya 28 zilizolengwa kwa Tundu Lisu. Tunakuomba wateketeze wote waliokula nja kuandaa na kutumia silaha na kufyatua risasi hizo, katika Jina la Yesu Kristu.
- Imeandikwa kwamba” Nitakufanya kuwa kama ukuta wa boma la shaba juu ya watu hawa;nao watapigana nawe lakini hawatakushinda” (Yeremia15:20-21). Bwana Tunakushukuru kuwa umekwisha mfanya Tundu Antipasi Lisu kuwa ukuta wa Shaba. Watu wasiolijulikana wamepigana naye muda mrefu na wanaendelea kupigana naye. Tunawatangazia woote wanaojiita wasiojulikana kuwa hawatamshinda Tundu Antipasi Lisu, katika Jina a Yesu Kristu.
- Imeandikwa kwamba “Bwana atawafanya adui zako wainukao juu yako kupigwa mbele yako” (Kumb;28:7) Baba Mungu Mwenyezi, kwa njia mbalimbali, ni wakati sasa wa kuwapiga watu wasiojulikana pamoja na washirika wao mbele ya watanzania wapenda HAKI; katika Jina la Yesu Kristu wa Nazareti.
- Baba Mungu Mwenyezi, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, tunakuomba wawezeshe watanzania wapenda haki kuwatoa katika hofu ya mashambulizi ya watu wasiojulikana, wavushe bahari kiisha uirudishe iwafunike wasiojulikana wote wanaotaka kuwaangamiza watu wema kama ulivyo waokoa wana wa Israeli kwa uwaangamiza majeshi ya Farao katika bahari ya Sham (Kutoka14:28-29) Katika Jina la Yesu Kristu wa Nazareti. Baba Mkabidhi Fimbo ya Maajabu Tundu Antipasi Lisu ili aitumie kupambana wa watu wasiojulikana, kama uivyo mkabidhi Musa Fimbo aliyoenda nayo kwa Farao, (Kutoka 4:4) katika Jina la Yesu Kristu wa Nazareti.
- Mungu Baba, Katika Jina Yesu Kristu, wabadilishe hao wasiopenda kusikia mawazo ya wengine, wape fahamu watambue kuwa “WEWE NDIYE AMBAYE UKO” (KUTOKA 3:14) Watambue kwamba wewe
- umeumba vichwa vingi , na kila kichwa kina haki ya kufikiri na kutenda kadiri ya utaratibu wa tawala ulizo wapa. Wape moyo wa kupenda kusikiliza hoja tofauti na zao na hata wasiyoyaamini. Wape uwezo wa kuvumilia kuishi na jirani, ndugu, jamaa kwa uependo. Wajalie neema ya kuishika amri mpya uliyotupa kwamba “Mpendane kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyohivyo” (Yohana 13:34).
Kwa Jina la Yesu Kristu, Wajaze Roho mtakatifu watu wasiojulikana Watambue kuwa “Kutenda Haki na Hukummu Humpendeza Bwana kuliko kutoa sadaka” (mithali 21:3)
Mungu Baba, Katika Jina la Yesu Kristu wa Nazareti wape ufahamu watu wasiojulikana watambue kuwa “Azibaye masikio yake asisikie kilio cha maskini, mnyonge, yeye naye atalia, lakini hatasikiwa (Mithali 21:13)
Baba tunakuomba mtie nguvu Tundu Antipas Lisu, mjalie afya njema awezekupona haraka na kurudi katika mapambano. Wape faraja familia yake na watanzania woote.
Tunakuomba hayo kwa Jina la Yesu Kristu Bwana Wetu,
AMINA.