John Achila Mukumwa
Senior Member
- Jan 4, 2024
- 111
- 214
Sala ya Bwana ni nini
Sala ya Bwana
Sala ya Bwana ni sala ambayo Yesu Kristo aliwafundisha wanafunzi wake, kabla ya kuondoka kwake. Na kwa kupitia sala ile, hakuwafundisha tu wanafunzi wake bali alitufundisha na sisi pia. Maana yake ni kwamba, nasi pia tunapaswa tuombe kama vile Bwana alivyowaelekeza wanafunzi wake.
Sala ya Bwana imegawanyika katika vipengele vikuu 8. Vipengele hivyo siyo sala yenyewe, bali ni kama “maelekezo ya sala”. Sala yenyewe hatuwezi kuandikiwa, bali ni kila mtu kulingana na anavyoongozwa au kujaliwa na Roho Mtakatifu.
Hebu tuisome sala yenyewe kipengele kimoja baada ya kingine.
Mathayo 6:7: “Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi.
8 Basi msifanane na hao; maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba.
9 Basi ninyi salini hivi (kipengele kwa kipengele):
1. BABA YETU ULIYE MBINGUNI
Hiki ni kipengele cha kwanza, ambacho Bwana anatuelekeza tuanze nacho katika sala zetu. Kwamba maombi yetu tuyaelekeze kwa Baba aliye mbinguni, kwamba tumwite Baba asikie maombi yetu na haja zetu, na yeye ni mwaminifu atatupa kama tutakavyomwomba, ikiwa tutaomba sawasawa na mapenzi yake.
Jambo la kuzingatia hapo ni kwamba Bwana Yesu anatufundisha kuomba kwa “Baba” na siyo kwa “Mungu”. Sasa Baba ndiye huyo huyo Mungu, lakini cheo cha UBABA kinahubiri mahusiano mazuri zaidi kwetu na aliyetuumba kuliko cheo cha UMUNGU.
Viumbe vyote vinamwona muumba kama Mungu, lakini kwetu sisi wanadamu tumepewa heshima ya kipekee kwamba tumwite Mungu, Baba yetu (1Yohana 3:1). Kwa hiyo tunapoingia kwenye sala/maombi, ni vizuri sana kuomba kwa kumwita muumba wako Baba kuliko kumwita Mungu. Hiyo ni kwa sababu wewe ni zaidi ya kiumbe chake bali ni mtoto wake.
2. JINA LAKO LITUKUZWE
Baada ya kumwita Baba aliye mbinguni kwamba atege sikio lake na kusikia maombi yetu sisi watoto wake, hoja ya kwanza tunayopaswa tumpelekee ni kwamba JINA LAKE LITUKUZWE. Wengi hawajui kuwa jina la Mungu linachafuliwa kila siku kutokana na maovu watu wa Mungu wanayoyafanya.
Warumi 2:22 “Wewe usemaye kwamba mtu asizini, wazini mwenyewe? Wewe uchukiaye sanamu, wateka mahekalu? 23 Wewe ujisifuye katika torati, wamvunjia Mungu heshima kwa kuiasi torati? 24 KWA MAANA JINA LA MUNGU LATUKANWA KATIKA MATAIFA KWA AJILI YENU, kama ilivyoandikwa”.
Madhara ya jina la Mungu kutukanwa katika mataifa, ni watu wengi kupotea na kuifanya thamani ya msalaba isionekane. Hivyo basi, mwenye uwezo wa kulitakasa jina lake ni Mungu tu (mwenye jina). Hivyo, tunapochukua nafasi hiyo ya kuomba kwamba Bwana alitakase jina lake, maana yake tunaomba Mungu alete utukufu katika injili yake. Kwamba Bwana ajalie watu kuliogopa jina lake, kwa kuonesha matendo makuu na ya ajabu, na hivyo wengi kutubu na kumrudishia yeye utukufu. Kwa hiyo hii inapaswa iwe sehemu ya sala kwa kila mkristo kila mahali.
3. UFALME WAKO UJE
Siku ambayo Ufalme wa Mungu utakuja duniani ni siku ambayo mateso yatakuwa yameisha, tabu zitakuwa zimeisha, huzuni zitakuwa zimeisha, na maumivu yatakuwa yameisha. Dunia ya sasa imejaa tabu na mahangaiko na majaribu mengi. Hivyo, kila siku hatuna budi kuomba kwa Baba kwamba aharakishe kuileta ile siku ambayo tutapata pumziko la hakika, dhidi ya haya majaribu mengi ya ulimwengu.
Kwa mtu ambaye anatamani kuondokana na haya maisha na kutamani kukaa na Mungu milele, basi atatumia muda wa kutosha kumwomba Bwana aulete ufalme wake. Na kwa kuomba hivi maana yake ni kwamba, tunaomba pia watu wengi waokolewe, kwa sababu ile siku haitakuja mpaka kondoo wa mwisho aliyekusudiwa uzima wa milele, aingie ndani ya zizi. Kwa kuomba ufalme wake uje, basi moja kwa moja pia tutakuwa tumeomba Bwana aharakishe kuwavuta watu wake ndani ya neema.
4. MAPENZI YAKO YATIMIZWE
Baada ya kuomba kwamba ufalme wake uje, basi hatua inayofuata ni kuomba kwamba mapenzi yake yatimizwe. Tunayo mapenzi yetu (yaani matakwa yetu), lakini pia yapo mapenzi ya Mungu ambayo huwenda sisi hatuyafahamu. Bwana Yesu kabla ya kuteswa alimwomba Baba na kusema, “kikombe hiki kiniepuke lakini si kama nitakavyo mimi bali utakavyo wewe (Mathayo 26:39).
Na sisi hatuna budi kuomba kuwa mapenzi ya Mungu yatimizwe hapa duniani, katika shughuli zetu, katika utendaji kazi wetu, na katika mambo yote yanayoendelea, mapenzi yake yatimizwe kama yanavyotimizwa huko mbinguni, mahali malaika walipo.
5. UTUPE LEO RIZIKI ZETU
Baada ya kuomba mapenzi yake yatimizwe, sasa ni wakati wa sisi kupeleka haja zetu, kama chakula, mavazi, makazi, fedha, na mambo yote tunayoyahitaji katika mwili na katika roho, Baba atupatie. Mungu anayesikia maombi atatupatia, kama ni fedha, au chakula au makazi au malazi. Vile vile, kipengele hiki ndicho pia cha kuwaombea wengine Bwana awape pia riziki. Hivyo, kinaweza kuchukua muda mrefu, kulingana na haja mtu alizonazo moyoni mwake.
6. UTUSAMEHE MAKOSA YETU
Kuna tofauti kati ya makosa na dhambi. Mtu anaweza kusamehewa dhambi lakini kosa la adhabu lipo palepale. Daudi alisamehewa dhambi yake ya kumtwaa mke wa Uria, lakini kosa la kuadhibiwa yeye na mtoto wake halikuondoka, na hapa sala ya Bwana inatuelekeza kwamba tumwombe Bwana atusamehe makosa yetu, huenda tumemkosa Mungu na tukamwomba msamaha na yeye akatusamehe lakini adhabu bado hajaiondoa. Hivyo, hatuna budi kumwomba Mungu kwa kuugua sana, kwamba atuondolee dhambi zetu pamoja na makosa yetu.
Hapa mtu anaweza kutumia muda mrefu, kujiombea mwenyewe na kuwaombea wengine. Lakini tunapoomba tusamehewe makosa ni sharti kwamba na sisi tuwasamehe waliotukosea, tusipowasamehe waliotukosea na Baba yetu aliye mbinguni hatatusamehe sisi.
7. USITUTIE MAJARIBUNI, BALI UTUOKOE NA YULE MWOVU
Shetani anatutafuta usiku na mchana, ili atuingize katika kukosa. Hila zote za shetani ili kutuangusha sisi ndiyo “majaribu yanayozungumziwa hapo”.
Bwana anatufundisha kumwomba Baba, atuepushe na mitego hiyo ya mwovu, ambayo kaiweka kila mahali ili kutuangusha. mitego hiyo shetani ameiweka makanisani, mashuleni, makazini na kila mahali. Hivyo lazima kuomba kwa muda mrefu kwa ajili ya mahali ulipo, au unapokwenda, ili kusudi usianguke katika mitego ya ibilisi. Pia, unapaswa kuombea na wengine (Wagalatia 6:2).
8. KWA KUWA UFALME NI WAKO, na Nguvu na Utukufu, hata Milele, Amina.
Hii ni hatua ya mwisho ya kumtukuza Mungu na kumwadhimisha, na kumshukuru. Hapa mtu anaweza kupaza sauti yake kama Daudi, kwa nyimbo au kwa kinywa na kusema Bwana ni mwenye nguvu, asikiaye maombi, ajibuye maombi. Bwana ni mwenye haki, Bwana ni mwenye enzi na mamlaka. Utukufu una yeye milele na milele.
Tukiomba namna hiyo, tutakuwa tumeomba sawa sawa na mapenzi ya Yesu Kristo.